Na Hastin Liumba,Tabora
MWENYEKITI
wa chama cha mapinduzi,(CCM),Hassan Wakasuvi,amesema kilimo cha tumbaku
mkoani Tabora,wakulima wake wataendelea kuumia kufuatia baadhi ya
watumishi wa serikali, na askari polisi kujiingiza katika ulanguzi wa
zao hilo katika kipindi cha masoko.
Wakasuvi
alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake hivi
karibuni baada ya mkutano mkuu wa chama kikuu cha wakulima wa tumbaku
kanda ya magharibi,(WETCU),mkoani humo.
Alisema
hali ikiendelea itafikia mahali zao la kumnufaisha mkulima itakuwa
ndoto hivyo ni vyema serikali ya mkoa ikafuatilia hilo na kulifanyika
kazi ili haki za wakulima zionekane na siyo ilivyo sasa.
“Katika
mkutano mkuu wa WETCU ambao uliambatana na uchaguzi,mkuu wa uongozi
wake, wapo wakulima waliotoa kero ya baadhi ya watumishi wa serikali na
askari polisi wanajihusisha na ulanguzi wa zao la tumbaku.” Alisema.
Mwenyekiti
huyo aliongeza kuwa kufuatia wakulima hao kulalamika hayo,hata yeye
ameshafanyika kazi lalamiko hilo na kuona ipo haja ya kuweka wazi tatizo
hilo ili kuondoa dhuluma iliyopo ikiwezekana kuwataja kwa majina endapo
wataendelea na biashara hiyo.
Alisema
amewasilisha kilio hicho kwa mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma Mwassa ili
aweze chukua hatua stahiki dhidi ya watumishi wa serikali na serikali
wanaojihusha na ulanguzi wa tumbaku ambapo mkuu huyo wa mkoa amesema
atafuatilia kwa ukaribu na kuchukua hatua.
Wakasuvi
aliongeza kuwa yupo tayari kumtetea mkulima yoyote kati ya wale
waliotoa malalamiko yao mbele ya mwenyekiti wa WETCU Alcard Iragila kuwa
kuna watumishi wa serikali na askari polisi wanalangua tumbaku kipindi
cha mauzo na masoko.
“Tuhuma
hizi ni za kweli wala hakuna haja ya kusingizia mtumishi wa serikali
ama askari polisi……siyo majungu ni tuhuma za ukweli na tutapigania hili
hadi mwisho na tabia hii ya dhuluma kukomeshwa kabisa.”alisema
Alisema
kuwa anajua kuwa wakulima waliothubutu kutamka kuwa askari polisi na
baadhi ya vigogo wa serikali wanalangua tumbaku kipindi cha masoko ya
zao hilo watasumbuliwa, lakini anaamini kuwa anawatetea kwa nguvu zote
hadi pale haki inapatikana.
No comments:
Post a Comment