Pages

KAPIPI TV

Thursday, January 24, 2013

KITUMBO ALIA NA WADAU ILI KUINUA KIWANGO CHA SOKA TABORA



Na Hastin Liumba,Tabora

MARA zote mimi huwa naamini kuwa mchezo wowote duniani,hususani soka
kwa dunia ya leo ni ajira yenye pato zuri,na kwamba serikali,wadau na
viongozi wa vyama vya michezo, tukishikamana pamoja tunaweza kuwa na
taifa la wanamichezo,licha ya kuwa na watu wenye vipaji vingi nchini.

Lakini hayo yatafikiwa malengo yake endapo viongozi wa vyama wataacha
ubinafsi,ubadhirifu na migogoro isiyoisha kama ilivyo katika baadhi ya
vyama vilivyowahi kukumbwa na migogoro mingi.

“Tunataka Tabora ifikie mahali tuwena na timu nzuri na kuondokana na
kuitwa kichwa cha mwendawzimu ama wasindikizaji kiwenye mashindano
kadhaa.” Aliongeza.

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora, (TAREFA),Yusuph Hamis
Kitumbo alisema hayo wakati akiongea
na mwandishi wa makala hii,ofisi za TAREFA, akibainisha mikakati
iliyopo chini ya uongozi wake ikiwemo mikakati ya kurejesha Tabora
inarejesha hadhi ya mchezo wa soka kama kipindi cha timu ya Mirambo.

“Nina imani kuwa sisi kama TAREFA,serikali ya mkoa,wadau na wapenzi
tukishikamana nina imani kubwa soka ya Tabora inakuwa kwa kasi kwani
kuna vipaji vingi sana mitaani ambavyo vijana waliopo wanapaswa
kuendelezwa katika michezo mbalimbali.” Alisema Kitumbo.

Kitumbo ambaye pia ameweka wazi kuwa ana nia ya kugombea nafasi ya
kamati ya utendaji shirikisho la soka Tanzania ,(TFF),amesema haya
yatafanikiwa zaidi endapo kutakuwa na mshikamano ngazi ya vilabu,vyama
vya michezo ngazi ya wilaya,mkoa na serikali, kwa kuweka uzalendo
mbele na kuunga mkono jitihada zinaazofanyika kuhakikisha timu ziliopo
daraja kwanza mkoani hapa zinafanikiwa
kuingia ligi kuu.

Kitumbo alifafanua kuwa hivi sasa kwa kushirikiana na viongozi
wenzake,wanaweka mipango mizuri ili kupandisha timu moja ambayo
itawakilisha mkoa kwenye ligi kuu na kurejesha makali ya kipindi cha
miaka ya 1988.

Hata hivyo anabanisha kuwa anataka Tabora irejee katika medani ya soka
kama ilivyo kwenye historia ya miaka ya 1936 kipindi nyuma ambacho
kulikuwa na timu 4
maarufu.

Aidha mwenyekiti huyo aliongeza kuwa hivi sasa kuna timu mbili za
Rhino Rangers,na Polisi,na kwamba wanaweka mikakati mikubwa
kuhakikisha timu hizo zinzcheza ligi kuu mwakani.

“Nawaomba wapenzi na wadau wa mchezo wa soka mkoani Tabora,yakiwemo
mashirika na taasisi za fedha kuungana katika kufaniukisha malengo ya
uongozi wa TAREFA ili hapo baadaye mkoa wetu unakuwa na timu zaidi ya
moja ligi kuu.”alisema.

Alisema haya yote hayatafanikiwa endapo kutakuwa hakuna uzalendo
kuanzia ngazi ya uongozi wa soka wenyewe,wapenzi na wadau katika
kuinua soka mkoani Tabora.

Kitumbo aliongeza kuwa chini ya uongozi wake wamejipanga vyema ikiwemo
kualika timu kadhaa kuja Tabora kucheza na timu za Polisi Tabora na Rhino
Rangers, ili kujenga uwezo wa timu hizo.

Kuhusiana na mikakati ya kiuongozi mwenyekiti huyo alisema
watahakikisha wanawaunganisha wana Tabora katika michezo kadhaa
ikiwemo soka ya wanawake na kuweza kuweka timu ya wanawake inayocheza
soka la kisasa.

Aliongeza kuwa moja ya mipango yake kwa sasa ni kuweka mipango
endelevu ya soka ya vijana chini ya miaka 17,kwa kila wilaya,kuanzisha
mashindano ya vikombe mbalimbali ili vipaji vilivyo vispotee bure.

“Mimi kama mwenyekiti wa TAREFA bado nina nafasi nzuri ya kuunganisha
watu kwani licha uongozi nilioupata katika uchaguzi ulifanyyika mapema
mwaka jana,mchezo wa soka naujua kwani nimecheza mpira…..na zaidi
nitamtumia mbunge wa jimbo la Tabora mjini ndugu yangu Alhaj Ismail
Aden Rage kuchota busara zake,na uzoefu kwenye medani ya soka kuleta
mabadiliko ya mchezo wa soka.” Aliongeza Kitumbo.

Alisema hivi karibuni mapema mwaka jana alisikia kwenye vyombo vya
habari,kuwa kuna wadau,wawili wa mchezo wa soka,mkoani hapa akiwemo
Alhaj Ismail Aden Rage na mdau Godfrey Kasanga, walijitolea vifaa vya
michezo vya mamilioni ya fedha na kuanzisha ligi zilizoshirikisha kata zote za
manispaa Tabora na mashindano yake yalifana na kwamba hatua hiyo
inapaswa kusimamiwa kwa ukaribu zaidi kwani vipaji vipo.

Kitumbo aliongeza kuwa atafatilia ili kuona kama mashindano hayo
yamefikiwa wapi na kama ilivyokuwa washiriki walimaliza mashindano
hayo na kukawa na zawadi,basi ipo haja kuona kama kuna uwezekano wa
kuyaendeleza kwa ni hatua nzuri zaidi kimichezo.

Aidha aliongeza kuwa katika utafiti wake mkoa wa Tabora,una vipaji
vingi vya mchezo wa soka,mpira wa pete,mpira wa wavu na mingineyo na
zaidi vyuo viliyopo mkoani hapa kuna wachezaji wazuri wanaopaswa
kuendelezwa na hiyo ndiyo kazi atakayoipa kipaumbele.

Alisema lengo lake ni kutafuta timu ya mkoa nyingine zaidi ya Polisi
Tabora na Rhino Rangers,timu ambayo ataipata kupitia mashindano ya
vijana chini ya miaka 17 katika kila kata za wilaya zote 7 za mkoa wa
Tabora.

Aidha mwenyekiti huyo aliongeza kuwa atahakikisha timu ya vijana chini
ya miaka 17 inayoshiriki mashindano ya Copa Coca-Cola maandalizi yake
yanafanyika mapemba,sanjari ya yake ya kombe la taifa ili kuepuka
maandalizi ya zimamoto.

Hata hivyo Kitumbo aliongeza kuwa haya yote yatafanikiwa endapo
kutakuwa uongozi unaofanya kazi zake kama timu ngazi ya wilaya na
mkoa,uadilifu kwenye kazi,kutokuwepo na matumizi mabaya ya fedha hasa
michango ya wadau,serikali na taasisi mbalimbali zitakazochangia
michezo husika.

Aidha mambo mengine ni kuwa na ofisi za kisasa,kutunisha akaunti ya
TAREFA ili chama kisigeuke chama cha kuomba misaada kwa wadau na
serikali kila mara.

Aliongeza kwa upande mwingine atashirikiana na mwakilishi wa soka la
wanawake mkoani Tabora,Mwalimu Janeth Kabeho kuhakikisha timu za
wanawake zinapatikana kila wilaya na kushirikishwa kwenye mashindano
mbalimbali yakiwemo ya kata kama ilivyo kwa soka ya wanaume.

Alisema ana imani wanawake wengi watajitokeza zaidi kujiunga na timu
zitakazoanzishwa kwani licha ya michezo kuwa afya,furaha,pia ni ajira.

No comments: