Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Acp Anthony Rutha akimkabidhi Pikipiki mkaguzi msaidizi wa Polisi Joseph Matui katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi ya Jeshi la Polisi mkoani Tabora.
Na Beatrice Masaki - Tabora 
Jeshi la polisi mkoani Tabora limepokea pikipiki  13 kutoka kwa Inspekta Jenerali  Said Mwema zitakazosaidia harakati za
kukabiliana na vitendo vya uhalifu  
katika mkoa huo.
Akikabidhi pikipiki hizo kamanda wa polisi mkoa wa Tabora,
ACP Anthon Rutha amesema kuwa,pikipiki hizo zitagawiwa kwa wakaguzi wa kila
tarafa wa wilaya za Igunga ,Uyui,Urambo ,Sikonge,Nzega na Tabora mjini  kwa lengo la kusaidia ulinzi  na usalama wa wananchi.
 Kamanda huyo wa
polisi wa mkoa wa Tabora ametoa  wito kwa
wakaguzi wa kila tarafa kuzitumia pikipiki hizo  kwa malengo yaliyokusudiwa na si kuzitumia kwa
matumizi binafsi na kuwataka wazitunze 
vizuri kwani kwa kufanya hivyo , kunaweza kusaidia kudhibit uhalifu kwa
wakati na kuimarsha amani mkoani hapa.
Akipokea pikipiki hizo kwa niaba ya  wakaguzi wa tarafa mkoani hapa mkaguzi wa
polisi Joseph Matui wa tarafa ya Tabora kaskazini amesema kuwa, pikipiki hizo
zitawasaidia kufika maeneo ambayo wananchi wanahitaji kujua mambo  mbalimbali ikiwa ni pamoja na  juu ya ulinzi na usalama wa mali zao.
 Matui  amewataka wananchi kuonesha ushirikiano kwa
askari  jeshi la polisi  pindi wanapofika katika maeneo yao  na pika wawe tayari  kuwafichua wahalifu.
 







 
 
No comments:
Post a Comment