Polisi
wakiwa tayari kuwadhibiti wananchi wakiofurika katika Hospitali ya
Temeke jana ili kushuhudia watu wawili waliodaiwa kupelwekwa hospitali
wakiwa wamenasana katika tendo la ndoa.Picha na Fidelis Felix.
HEKAHEKA ya aina yake, ilitokea jana kwenye Hospitali ya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, baada ya kudaiwa kuwapo na watu waliokuwa wamefanya uzinzi na kushindwa kutengana.
Tukio
hilo lililozusha sintofahamu, lilidaiwa kutokea kwenye nyumba moja ya
kulala wageni (jina tunalo) iliyopo Temeke na wahusika walipoona
wanashindwa kujinasua baada ya kumaliza haja zao, waliomba msaada wa
kufikishwa hospitalini hapo.
Habari
hizo zilizoanza kuenea majira ya asubuhi zilisambaa kwa kasi katika
mitandao ya kijamii na mikoa mbalimbali jambo lililosababisha baadhi ya
wasomaji kupiga simu katika chumba cha habari kutaka kujua nini hasa
kilichotokea.
Mashuhuda
wa tukio hilo, waliliambia Mwananchi kuwa watu hao walifikishwa
hospitalini hapo wakiwa kwenye gari aina ya Canter kwa ajili ya kupatiwa
huduma baada ya kila mmoja kumng'ang'ania mwenzake huku wakiwa
wamejifunika shuka za nyumba hiyo ya kulala wageni.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alipofuatwa kuzungumzia tukio
hilo lililotokea mita takriban 300 kutoka ofisini kwake, ilielezwa kuwa
yuko kwenye kikao.
Hata
hivyo, alipotafutwa baadaye jioni alisema: “Habari hizo ni uongo,
hazina ukweli wowote, na polisi imeanza uchunguzi kufahamu nani
aliyeanzisha uvumi huo.”
Kwa
mujibu wa Kamanda Misiime, ambaye anahamia Dodoma kuchukua nafasi ya
Kamanda Zelothe Steven anayestaafu, alisema polisi wanaendelea na doria
hadi hapo hali itakapotengemaa katika hospitali hiyo.
Kinachodaiwa kutokea Hospitali ya Temeke.
"Muda wa saa 4:00 asubuhi liliingia
gari aina ya Canter hospitalini huku likiwa na watu wawili ambao
walifunikwa shuka na kupelekwa katika ofisi zilizopo kwenye jengo la
kuhifadhiwa maiti," alisema mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa
jina la Khamis Ramadhani.
Alisema:
"Habari hizi zilienea kwa kasi na kuvuta hisia za wengi na walifika
hospitalini hapo kwa ajili ya kuwashuhudia watu hao.
"Baada
ya kutokea hali hiyo, Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) walifika kwa
ajili ya kuwatawanya baada ya kuanza ghasia huku wengine wakitumia
nafasi hiyo kupora mali kwa watu wengine."
Mwandishi wa habari hizi, alishuhudia Polisi ikiwatangazia watu kuondoka eneo hilo vinginevyo watatumia nguvu.
Baada ya watu kutotii amri ya kuondoka, polisi hao walianza kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya watu hao.
Hata
hivyo, watu hao waliondoka eneo la tukio, lakini baadaye walirudi tena
na askari kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Baada
ya kuona hali inazidi kuwa ngumu, uongozi wa hospitali hiyo ulifunga
milango na kuzuia watu kuingia ndani wakiwamo wagonjwa wa nje waliofika
kwa ajili ya kutibiwa.
No comments:
Post a Comment