Mbunge
wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee (aliyesimama) akiwasilisha hoja yake
binafsi juu ya kusitishwa ugawaji wa ardhi kwa wa uwekezaji wageni hapa
Tanzania.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Profesa Anna Tibaijuka
ambaye aliunga mkono hoja ya Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee.
Na.Mwandishi wetu, Dodoma.
SERIKALI
imeunga mkono hoja binafsi ya Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee
juu ya kusitisha ugawaji wa Ardhi hadi tathmini ya kina itakapofanyika
kujua kiasi cha ardhi kilichoko mikononi mwa wawekezaji wageni hapa nchini.
Katika
kuwasilisha hoja yake binafssi Mbunge Mdee amedai kuwa kumekuwa na
usumbufu mkubwa kwa wananchi kwa kufukuzwa katika maeneo yao ya makazi
na ardhi yao kuuziwa wawekezaji wageni.
Amedai kuwa vitendo vya unyanyasaji vimeenea sana hapa nchini Tanzania na kuwafanya watanzania kuwa watumwa katika ardhi yao.
Hoja
ya Mbunge Halima Mdee imeungwa mkono na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi , Profesa Anna Tibaijuka na kusema kuwa mgawaji
halali wa ardhi ni wizara yake.
Profesa
Tibaijuka amedai kuwa kumekuwa na utapeli mkubwa wa uuzaji wa ardhi kwa
wawekezaji wageni hususani katika halmashauri za wilaya hapa nchini
Tibaijuka
amesema kuwa hoja hiyo ya Mdee ni lazima ifanyiwe maazimio mawili
kutoka serikali ambayo itawasilisha kauli ya serikali hapa baadaye.
No comments:
Post a Comment