Mkurugenzi
wa Kampuni ya Best Import Zanzibar Issa Kassim Issa kushoto
akimkabidhi Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Abadallah Ali
Abadallah dola 2000 za kimarekani kwa ajili ya kusaidia matibabu ya
Katibu wa Mufti Zanzibar Skeikh Fadhil Soraga katika Ofisi ya Makamo wa
Pili wa Rais Vuga mjini Zanzibar..
Picha na Yussuf Simai Maelezo Zanzibar.
Kampuni
ya Best Imports Zanzibar inayojishughulisha na biashara ya uuzaji Kuku
(Paja Nono) imetoa jumla ya Dola 2000 za kimarekani kwa ajili ya
kusaidia matibabu ya Katibu wa Mufti Zanzibar Skeikh Fadhil Soraga.
Akitoa
msaada huo leo kupitia kwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais
Zanzibar,Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Issa Kassim Issa amesema wameamua
kutoa mchango huo kutokana na kuguswa na kitendo cha kinyama
alichofanyiwa Sheikh Soraga na kwamba kiasi hicho cha pesa kitatumika
kusaidia matibabu yake.
Issa
amesema wamiliki wa Kampuni hiyo David Aloy na Carlos Ajala wamestushwa
na kitendo alichofanyiwa Sheikh Soraga ambaye ni mtu muhimu katika
jamii kutokana na mchango wake mkubwa.
Ameongeza
kuwa Shekh Soraga ni mtu mwenye heshima kubwa Zanzibar kutokana na
shughuli zake za kila siku na kwamba kitendo alichofanyiwa kinapaswa
kulaaniwa na kila mtu.
Kwa
upande wake Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Abadallah Ali
Abadallah aliishukuru Kampuni hiyo kwa kuwa wa kwanza kutoa msaada wa
kifedha na kuahidi kiasi hicho cha fedha kitapelekwa sehemu husika.
Aidha
Katibu huyo amewaomba wananchi kumuombea Shekh Soraga apone haraka na
wale wenye uwezo kuiga mfano wa Kampuni ya Best Import ili kufanikisha
matibabu hayo.
Sheikh Soraga ambaye anatarajiwa kupelekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi ameumia sehemu za usoni,mikononi na kifuani baada
ya kumwagiwa Tindikali na mtu asiyejulikana wakati alipokuwa akifanya
mazoezi viwanja vya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi Unguja.
No comments:
Post a Comment