Pages

KAPIPI TV

Friday, October 5, 2012

WENGI BADO HAWAJAAMINI MATOKEO YA UCHAGUZI WA CCM WILAYA YA TABORA MJINI

Na Mwandishi maalum,Tabora

UCHAGUZI wa CCM wilaya ya Tabora mjini umekamilika,huku mwenyekiti wa chama hicho,Moshi Abdulrahaman Nkonkota,akifanikiwa kutetea nafasi yake kwa kumbwaga mwenyekiti wa zamani Juma Abdalah.

Aidha nafasi ya ujumbe wa NEC uliangukia kwa mfanyabiashara na mwenyekiti wa TCCIA, mkoa wa Tabora,John Mchele akimshinda mbunge wa zamani CCM,Mwanne Mchemba ambapo kulikuwepo na marudio ya kupiga kura.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, Said Ntahondi,alisema nafasi ya mwenyekiti wa wilaya,Moshi Nkonkota,alipata kura 759,Juma Abdalah 210,Ali Mwantende 33,na Saimon Madulu 29.

Ntahondi aliongeza nafasi ya ujumbe wa NEC ilikwenda kwa John Mchele kura 489 ambapo awali walichuana na Mwanne 294,Mchemba na Deo Kahumbi kura 251.

Alisema kura haizkufikia nusu hivyo marudio ya upigji kura yalimpa ushindi John Mchele aliyepata kura 557 na Mwanne Mchemba akiammbulia kura 296.

Aidha wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa washindi ni Kisamba Tambwe kura 692,Nisalile Mwaipasi 322,William Chimaguli 312,Judith Mlela 289 na Rhoda Madaha 274.

Alimtangaza katibu mwenezi wa wilaya kuwa ni Rashid Ramadhan aliyepita kwa kura zote za ndiyo 138,na nafasi ya katibu wa uchumi na fedha wilaya ilikwenda kwa Frank Mgonja kura 88,mweka hazina wa zamani Yasin Mihambo 27,Kamaliza Kayaga 14,Amina Said 9 na Adolphina Masaba 0.

Ntahondi aliwataja washindi wajumbe kamati ya siasa kuwa ni Humud Nassor kura 102,Hamis Jabir 77,Vituko Salala 67,Ali Kazikupenda 61 na Rhoda Sangwa 61.

Alisema wajumbe 10 wa halmashauri ya wilaya kupitia jumuiya ya wazazi washindi ni Hamis Jabir kura 469 na Frank Mgonja 444.

No comments: