Pages

KAPIPI TV

Friday, October 5, 2012

ZAIDI YA WATUMISHI 75 WAPUNGUZWA KAZI MGODI WA NZEGA

 Na Mustapha Kapalata na Lucas Raphael, Nzega-Tabora.

ZAIDI ya Watumishi 75 wa kampuni ya Caspian inayofanya kazi katika mgodi wa dhahabu wa Resolute uliopo wilayani Nzega mkoani Tabora wamepunguzwa kazi kutokana na maandalizi ya ufungaji wa mgodi huo.

Wakizungumuza na mwananchi baadhi ya watumizi hao walisema kuwa tukio hilo limetokea September 27 mwaka huu katika kampuni hiyo.

Walieleza kuwa taarifa hizo za kupunguzwa kazi zilitolewa mapema lakini hawakutarajia kama tukio hilo lingeweza kutokea kwa nyakati kama hizi kwani baadhi yao wana halimbaya ya kiuchumi pamoja na kutojiandaa kwa suala hilo.


Walieleza kuwa sababu za kupunguzwa kazi watumishi hao ni pamoja na maandalizi ya ufungaji wa mgodi huo (mining closer) ikiwa na kupungua kwa uzalishaji mali.

Mmoja wa watumishi waliopitiwa na sakata hilo la  kupunguzwa kazi ambaye jina lake limehifadhiwa alisema kuwa kupunguzwa huko kumepitia kila idara ambazo ni idara ya uzalishaji,ufundi pamoja na sehemu mbalimbali kwa kampuni hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya kampuni hiyo zilisema kuwa kupunguzwa huko bado kuna endelea kwa nyakati tofauti ikiwa na malipo yao stahiki wakipatiwa kwa muda muafaka kulingana na muda wakazi alioutumikia  mfanyakazi husika.

Hata hivyo walisema kuwa malipo wanayolipwa na kampuni hiyo hayatoshi kulingana na muda waliofanya kazi na malipo wanayopatiwa.

Wameiomba serikali iingilie kati katika suala hilo ili waweze kulipwa stahiki zao kama jinsi walivyo kuwa wakitegemea.

‘’Hapa tumechakachuliwa malipo hayatoshi nimefanyakazi toka 2007 mpaka leo 2012 nimelipwa jasho langu laki tano kweli jamani tunaiomba serikali iingilie kati katika hili ilitupewe haki yetu stahiki kama makampuni mengine’’ alisema mtumishi huyo aliyepunguzwa kazi.

Ofisa utumishi wa kampuni hiyo ya Caspian aliyefahamika kwa jina moja la Mbaga alithibitisha kupunguzwa kazi kwa watumishi hao na kuongeza kuwa yeye sio msemaji wa kampuni hiyo na badala yake wasemaji wake ni kampuni mama ya Resolute.

‘’Kapalata(Mwandishi wetu) mimi sio msemaji wa hili kwani kampuni mama ni Resolute na hao ndio wenye mamlaka ya kuzungumza lakini ni kweli watumishi hao wamepunguzwa kazi mie sio mzungumuzaji wa hili’’ alisema Ofisa huyo mbaga.

Jitihada za kumpata msema wa kampuni ya uchimbaji ya Resolute ili aweze kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda kwani simu yake ya mkononi iliita na haikupokelewa jitihada za kupata ufafanuzi huo juu ya suala hili zinaendelea.

No comments: