ZANZIBAR
JUMANNE OKTOBA 2, 2012. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta
Jenerali Saidi Mwema, Ijumaa na Jumamosi wiki hii, atakuwa mgeni Rasmi
katika sherehe za kufunga mafunzo ya uongozi mdogo kwenye Chuo cha
Taaluma ya Polisi Zanzibar.
Taarifa
ya Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar (Zanzibar Police Academy) SSP
Raamadhani Mungi, imesema kuwa mafunzo hayo ya mwezi mmoja yatafungwa
katika awamu mbili tofauti.
Amesema
awamu ya kwanza, mafunzo hayo itafanyika katika chuo cha Mafaafisa wa
Mafunzo (Magereza) kilichopo eneo la Hanyengwa mkoa wa Kusini Unguja
ambapo yatafanyika maonyesho ya utayari na Medani za kivita.
Kamanda
Mungi amesema maonyesho hayo yatanza saa 9.00 Arasili siku ya Ijumaa
Oktoba 5, mwaka huu, kwa kuwashirikisha Wahitimu wa vyeo vya RSM na
Staf Sajent waliokuwa wakishiriki katika mafunzo hayo.
Amesema
sherehe hizo zitafuatiwa na zile zitakazofanyika kwenye Viwanja vya
Polisi Ziwani mjini Mjini Zanzibar zitakazoanza saa 2.30 asubuhi siku ya
Jumamoori Oktoba 6, 2012.
Kamanda
Mungi amesema siku hiyo asubuhi, IGP Mwema, atakagua gwaride kabla ya
gwaride hilo kupita mbele yake kwa mwendo wa pole na mwendo wa waharaka
kwa heshma.
Kamanda
Mungi ametoa wito kwa wananchi wa vijiji vya Jendele, Ndigani, Cheju,
Kwaka, Tunguu, Dunga na wenyeji Hanyegwa pamoja na wakazi wa mjini
Zanzibara na Viunga vyake, kufika kwa wingi katika Chuo hicho cha
Hanyegwa na Ziwani ili kujionea maonyesho mbalimbali.
Zaidi
ya Askari 920 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na
Visiwani waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya Sajenti, Staf Sajent na RSM
watahitimu mafunzo yao na kutunukiwa vyeo vipya.
No comments:
Post a Comment