Pages

KAPIPI TV

Tuesday, September 18, 2012

WATU TISA WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA SINGIDA,

Baadhi ya miili ya watu tisa waliopata ajali mbili tofauti wakiwemo askari polisi wanne waliokuwa wakisindikiza mwili wa mwenzao kutoka Morogoro mjini kwenda kuzikwa mkoani Mara.Maiti zingine tano ni za wafanyabiashara wa minadani waliofariki wakienda mnada wa Mtavira kata ya Minyughe wilaya ya Singida.

Baadhi ya wakazi wa Singida mjini,wakijaribu kutambua  miili ya watu waliofariki kwenye ajali ya fuso wakati wakienda mnada wa kijiji cha Mtavira kata ya Minyughe wilaya ya Singida.
Mama mmoja ambaye hakuweza kutambuliwa jina lake,akilia kwa uchungu mkubwa baada ya mtoto wake kufariki dunia (jina halikuweza kutambulika mara moja) kwenye ajali fuso lililokuwa likienda mnada wa Matavira kata ta Minyughe wilaya ya Singida.
Baadhi ya umati ulikokuwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida,wakisubiri kuingia kutambua miili ya ndugu zao.
 Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa (wa pili kulia anayeshika simu) akiwa nje ya jengo la chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa baada ya kukagua miili ya watu tisa waliofariki kwenye ajali ya gari la polisi Morogoro na ile ya fuso.Wa kwanza kulia ni afisa upelelezi makosa ya jinai Ayubu Tega.Picha zote na Nathaniel Limu.


Na Nathaniel Limu,Singida

WATU nane  wamefariki dunia papo hapo katika matukio mawili tofauti ya ajali zilizohusisha magari mawili iliwemo landrover PT 1149 na kusababisha majeruhi 25.

Ajali hizo zimetokea jana (14/9/2012) kati ya sasa 5.30 na 6.30 asubuhi.

Landrover hiyo mali ya jeshi la polisi Morogoro mjini,ilikuwa na abiria 11 ambao walikuwa wanasindikiza mwili wa askari polisi Regu Kamamo, ambao ulikuwa unapelekwa mkoani Mara,kuzikwa.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa,alisema kuwa gari la polisi limepata ajali katika eneo la kambi ya Wachina iliyopo eneo la Manguajunki manispaa ya Singida.

Aliwataja walifariki kwenye ajali hiyo iliyohusisha gari la polisi kuwa ni,staff sajenti Rose Mary Nyaruzoki (53),Nyamwenda Juma, Rehema Juma.

Sinzuma alisema bado uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo ya kusikitisha.

Alisema majeruhi nane  wa ajali ya gari la polisi,wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya mjini Singida, na hali zao zinaendelea vizuri.

Katika tukio la pili,Kamanda huyo alisema kuwa fuso T.126 AEU lililokuwa limepakia wafanyabishara wa minada likitokea Singida mjini kwenda mnada wa Mtavira kata ya Minyunge wilaya ya Singida,lilipinduka na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo na kujeruhi 14.

Alisema ajali hiyo imetokea jana saa 6.30 huko katika kijiji cha Mtavira.

Sinzumwa aliwataja waliofariki dunia papo hapo ni Sarafina Ally, Pili Saida,Charles Thomas na wawili waliofahamika kwa majina ya Bakari na Bilali.

Alisema kwa upande wa maheruhi 17,wamelazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa na hali zao zinaendelea vizuri.

Alisema chanzo cha ajili ya fuso,bado hakijafahamika na uchunguzi zaidi bado unaendelea.

"Maiti zote tisa yaani za gari la polisi na zile za gari la fuso,zimehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa,kusubiri ndugu zao ili kuzitambua na kuzichukua kwenda kuzizika",alisema.

Kamanda Sinzuma,alisema kuwa taarifa zaidi kuhusiana na ajali hizo,atazitoa leo (kesho 15/9/2012) .

Kwa mijubu wa mmoja wa majeruhi wa fuso,Maulidi Mohammed,fuso hilo lilipinduka baada ya breki zake kukwama kufanya kazi.


Post a Comment