WANANCHI
wa kijiji cha mbutu na kata ya mbutu katika wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wameitaka serikali wilayani humo
kuharakisha ujenzi wa Daraja la mto mbutu kabla ya msimu wa mvua za masika hazija
anza kunyesha ,ikiwa na kuwapatiwa kivuko endapo Daraja hilo litachukua muda
mrefu kukamilika.
Wakizungumuza
na gazeti hili lilipo tembelea Daraja hilo wa
lisema kuwa Daraja hilo
limekuwa nitatizo kubwa kwa wananchi wa Igunga hasa katika kipindi cha masika.
Wameiomba
serikali kuharakisha ujenzi huo wa daraja kwa muda uliopangwa ikiwa na
kuwapatia kivuko cha dharula ili kuwa epushia adha ambazo walikuwa wakizipata.
Evalist
Juma ni mmoja ya wananchi wa kata ya Mbutu akizungumuza kwa nyakati tofauti
alisema kuwa Daraja hilo
ni kiungo muhimu kwa wananchi wa igunga katika shuguli mbalimbali za kijamii na
biashara.
Alisema
kuwa kwakipindi hiki ujenzi unaendelea serikali iwapatie kivuko cha dharula
ambacho kitaweza kuwa saidia kuvuka wakati shuguli za ujenzi huo zinaendelea.
Evalist
alisema katika Daraja hilo
watu wengi wamepoteza maisha wakati wa mvua za masika hali ambayo imekuwa
tishio kubwa kwa wananchi wa igunga pamoja na kwa wanasiasa.
‘’Daraja
hili nitishio kubwa sana
kwa wananchi watu wengi wamekufa hapa kutokana na kubebwa na maji wakati wa
mvua za masika tunaiomba serikali ifuatilie suala hili mapema hata viongozi wa
siasa wanalijua hili’’alisema Evalist.
Mkuu
wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu aliwaha kikishia wananchi wa Igunga kuwa
serikali inaendelea na ujenzi huo wa Daraja kwa viwango vikubwa ili kuhakikisha
linatumika mapema.
Alisema
kuwa Mkandarasi wa ujenzi huo yupo kazini anaendelea na kazi hata hivyo kuhusu
suala la kivuko mkuu huyo hakuweza kuzungumzia suala hilo.
Aliwataka
wananchi wa Jimbo hilo kuwa watulivu kwa kipindi
hiki na kuwataka kuwa kazi zote za kimaendeleo zitaendelea kufanyika kama hapo awari jinsi zilivyo kuwa zikifanyika.
No comments:
Post a Comment