Pages

KAPIPI TV

Wednesday, September 19, 2012

RC AMCHONGEA MBUNGE KWA WAKULIMA

Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,akikaribishwa na wanachama wa Talanta SACCOS na baadhi ya wakazi wa Iguguno wilaya ya Mkalama.
Jumla ya matrekta 11 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 156 yaliyotolewa mkopo kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama.Picha zote na Nathaniel Limu.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama,Edward Ole Nalenga,akizungumza muda mfupi kabla hajamkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,kuzungumza na wanachama wa Talanta SACCOS na wananchi wa Iguguno kabla ya kukabidhi matrekta 11 makubwa.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi matrekta makubwa 11 kwa wanachama wa Talanta SACCOS.Matrekta hayo yametolewa mkopo na Benki ya rasilimali (TIB),mkopo huo una thamani ya zaidi ya shilingi milioni 156.

Mwenyekiti wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri,Mayasa Salum,akijaribisha kuwasha trekta lake alilokopeshwa na benki ya rasilimali (TIB).
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,akijaribisha kuwasha moja ya matrekta 11 yaliyotolewa mkopo kwa wanaSACCOS wa Talanta ya tarafa ya Kinyangiri.
  Na Nathael Limu,Singida. 
MKUU wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, amemchongea  mbunge mmoja wa mkoa huu kwa wananchi, kwa kitendo chake cha kupinga hadharani uanzishwaji  vyama vya msingi vya ushirika.
Dk. Kone alisema baada ya yeye kutoa amri ya kupiga marufuku wafanyabiashara binafsi kununua alizeti moja kwa moja kutoka kwa wakulima, kulitokea makundi ya wafanyabiashara na baadhi ya viongozi na hasa wakuchaguliwa na wananchi kupinga amri hiyo.
 
Alisema zilitumika nguvu nyingi sana zilizolenga amri hiyo halali, aidha yeye (RC) au viongozi wenginewa ngazi za juu, waifute haraka iwezekanavyo amri hiyo halali.
“Hawa wafanyabiashara na baadhi ya viongozi wakiwemo wabunge wawili, wamekuwa wakipotosha kwamba amri hiyo halali ambayo ipo kisheria, eti inanyanyasa na inawanyima uhuru wakulima na hasa wadogo kuuza alizeti yao”, alisema na kuongeza;
“Amri hii halali, pamoja na mambo mengine, inalenga kumwokoa mkulima asiendelee kunyonywa na walaguzi au wafanyabiashara binafsi kwa kupewa bei ndogo.Tunataka wafanyabiashara binafsi wanunue alizeti katika vyama vya ushirika, ambapo watapata alizeti nyingi kwenye eneo moja”.
“Wananchi,hivi ni nani hasa mtetezi wa wakulima ni serikali ya mkoa ambayo inakataza walaguzi wa mazao kuendelea kuwanyonya wakulima kwa kutoa bei ya chini au mbunge ambaye anataka mkulia aendelee kunyonywa kwa kupewa bei ndogo ya alizeti”,aliuliza Dk.Kone.
"Wewe mkuu wa Mkoa,ndio mwenye uchungu na wananchi wako unaowaoongoza.Tunakupongeza sana kwa juhudi zako za kuanzisha vyama vya ushirika vya wakulima,tumechoka kunyonywa nguvu zetu",walijibu kwa nguvu wakulima waliokuwepo kwenye mkutano huo wa hadhara.
Dk.Kone alipoombwa kumtaja mbunge huyo, alisema atawanong'oneza siku nyingine,lakini akasema kuwa mbunge huyo amepiga kelele sana kwamba Singida hakuna vyama vya ushirika na vyombo vya habari vimekuwa vinamtangaza sana.
 
Alisema kutokana na kutangazwa sana huko na vyombo vya habari,imani yake ni kwamba anafahamika kwa watu wengi kuwa kipaombele chake ni wananchi waendelee kunyonywa na walaguzi. 
Akifafanua zaidi, alisema mbunge huyo amekuwa kishupalia kuwa vyama vya msingi vya wakulima hvipo na vilivyopo, havina mtaji.
“Leo hii nachukua nafasi hii, nimchongee kwenu mbunge huyu ambaye anataka soko la alizeti liwe holela lisilokuwa na utaratibu wo wote au bei elekezi.  Anataka ninyi wakulima mwendelee kunyonywa na walaguzi na wafanyabiashara binafsi",alisema.
 
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Kone,alimchongea mbunge huyo mbele ya hafla ya kukabidhi matrekta 11 kwa wanachama wa SACCOS ya Talanta ya tarafa ya Kinyangiri wilaya ya wilaya mpya ya Mkalama.


No comments: