Pages

KAPIPI TV

Tuesday, September 18, 2012

SANGOMA ADAIWA KUUA BAADA YA KUTOLIPIWA BIA MOJA .


Na Anthony Mayunga-Serengeti.
Septemba 18,2012.

MGANGA mmoja wa kienyeji(Sangoma) anatafutwa kwa tuhuma za kumpiga na
kumsababishia kifo mkazi mmoja wa kijiji cha Rung’abure wilayani
Serengeti baada ya kukataa kumlipia bia moja yenye thamani  ya
tsh,2,000=

Tukio hilo linadaiwa kutokea septemba 12,majira ya saa 11 jioni mwaka
huu katika kijiji cha Rung’abure  limethibitishwa na polisi wilayani
hapa ambao wanadai wanamtafuta ,na uongozi wa kijiji cha Rung’abure.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Charles Augustino amemtaja
mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Hamisi (42)mwenyeji wa Singida ambaye
alikuwa kijijini hapo kwa hawala yake akishughulika na shughuli za
uganga.

Aliyekufa amemtaja kuwa ni  Samweli Mwita Mkirya(38)mkazi wa kitongoji
cha Kwa nina kijijini hapo ambaye alikuwa rafiki ya mtuhumiwa .

Akielezea tukio zima alisema kabla ya kutokea tukio
Mkirya(marehemu)alimwita mtuhumiwa  wakaenda baa ya Chacha Mweri
amnunulie bia .

“Mtuhumiwa alikunywa bia moja wakati anaondoka akabanwa alipe lakini
akadai yeye ameagiziwa na Samweli,alipoulizwa akakana kumwagizia
akimtaka lipe mwenyewe ndipo pakatokea vurugu kati ya
Samweli(Marehemu)na Mtuhumiwa,”alisema.

Alisema Mtuhumiwa kwa kuwa alikuwa hajaelewa alimpiga kirahisi Samweli
Kichwa usoni kisha teke akaanguka chini nay eye akaondoka na kumwacha
hapo chini akivuja damu mdomoni,masikioni na puani.

“Samweli(Marehemu)kabla ya hapo inasemekana alikuwa amekunywa
viroba,alilala hapo hadi ndugu zake wakajitokeza,na kumchukua hadi
hospitali teule ya Nyerere ddh,hata hivyo alifia mapokezi na taarifa
za madaktari zinadai damu ilivujia kwenye ubongo ndiyo chanzo cha
kifo”alisema Mwenyekiti.

Kuhusu  Mtuhumiwa alisema inasemekana alitaarifiwa na rafiki zake kuwa
ameua akachukua bod boda na kukimbilia mjini Mugumu ambapo inasemekana
ndugu yake ni askari polisi na kufanikiwa kutoroka.

Wakati huo huo mkazi mmoja wa kijiji cha Gesarya wilayani hapa Magape
Kenda (42)amekufa baada ya kunywa pombe aina ya gongo bila kula ,tukio

ambalo limethibitishwa na polisi.

No comments: