UBUNGO KWENDA TEGETA.BASI LILIPOFIKA MWENGE ABIRIA WALIONGEZEKA NA
WENGINE WAKAWA WAMESIMAMA,KATI YA WALIOSIMAMA ALIKUWAPO MZEE MMOJA
ALIYEKUWA NA HAND BAG KAMA TUNAZOBEBEA LAPTOP HIVI, YULE MZEE
ALIMUOMBA MJOMBA WANGU AMSAIDIE KUMSHIKIA BAG LAKE KWA KUWA YEYE
ALIKOSA SITI, BILA YA KUSITA AKAAMUA MUMSAIDIA KALE KA BAG" BAADA YA
VITUO VIWILI YULE JAMAA MWENYE KA BAG; ALITEREMKA BILA MJOMBA WANGU
KUMUONA NA YEYE HAKUWA NA WASIWASI KWA KUWA ALIJUA MWENYE MZIGO
AKITAKA KUSHUKA ATAUCHUKUA TU MZIGO WAKE.
KABLA GARI HAIJAFIKA KITUO CHA TATU ILISIMAMISHWA NA WATU
WALIOJITAMBULISHA KWAMBA WAO NI ASKARI POLISI WAPELELEZI KWAMBA KUNA
KITU WANAPELELEZA,WAKAWAAMURU ABIRIA WOTE WATEREMKE KWENYE
GARI,WALIFANYA HIVYO MMOJA WA WALE POLISI, WALIMFUATA MJOMBA WANGU NA
KUMUULIZA 'NA WEWE KWENYE BAG LAKO KUNA NINI? AKAWAJIBU BAGI SIYO
LANGU KWA HIYO SIWEZI JUA NDANI KUNA NINI!! WAKAMUULIZA TENA, MWENYEWE
YUKO WAPI TUONESHE" AKAANGALIA KATI YA WALE ABIRIA WENZAKE HAKUMUONA.
WAKASEMA FUNGUA TUONE KUNA NINI NDANI, WALIPOFUNGUA WAKAKUTA KUNA
SILAHA AINA YA PISTO.ALIPOJARIBU KUJITETEA WAKAMWAMBIA TWENDE KITUONI
UTAENDA KUJIELEZA HUKO. BASI LIKARUHUSIWA NA YEYE WAKAMPELEKA POLISI,
WAKIWA NJIA WAKAMWAMBIA KAMA ANATAKA WAMWACHIE ATOE LAKI NANE
800,000/= VINGINEVYO WATAMUUNGANISHA KATIKA KESI YA WIZI WA KUTUMIA
SILAHA,AKAWAAMBIA SINA HIZO PESA NA SIWEZI KUTOA MPAKA SASA BADO YUPO
NDANI.HII INATUKUMBUSHA KWAMBA NI KWELI TUNAPENDA KUWASAIDIA WATU ILA
TUWE MAKINI NA MISAADA TUNAYOITOA. MZEE ALIKUWA NA NIA NJEMA KABISA YA
KUTOA MSAADA ILA MSAADA UMEMGHARIMU MAISHA. Mwisho napenda
kuwatahadharisha watu wote tuwe makini na watu tusiowajua,
Anna Mungai
Sales Coordinator
C&TM Operations
+255 22 216 6502
anna.mungai@jti.com
Tanzania Cigarette Company Ltd
A member of the JTI Group of Companies
20 Nyerere Road, P.O. Box 40114, Dar es Salaam
jti.com


No comments:
Post a Comment