
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi vyeti kwa viongozi wa SACCOS saba za mikoa ya Singida na
Manyara. Vyeti hivyo vimetolewa na mfuko wa uwezeshaji (Wananchi
Empowement Fund) baada ya SACCOS hizo kufanikiwa mikopo ya thamani ya
zaidi ya shilingi bilioni 1.4.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt.Parseko Kone akikabidhi cheti kwa viongozi wa
SACCOS ya Jipe Moyo ya kata ya Kinyangiri wilayani Mkalama.
Katibu
Mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Dk.
Anacleti Kashuliza akitoa taarifa yake kwenye hafla ya kukabidhi vyeti
kwa SACCOS saba za mkoa wa Singida na Manyara. Wa kwanza kushoto ni mkuu
wa mkoa wa Singida na wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida
Queen Mlozi.
Meneja
mikopo wa CRDB tawi la mkoa wa Singida Mbwana Hemed akitoa salamu zake
kwenye hafla ya kukabidhi vyeti kwa SACCOAS saba za mkoa wa Singida na
Manyara.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya kukabidhi vyeti kwa
SACCOS za mkoa wa Singida na Manayara. Wa kwanza kushoto ni Halima Jamal
wa gazeti la Tanzania Daima akifuatiwa na Abbya Nkungu wa Habari Leo na
Daily News pia ni Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Singida. Wa kwanza kulia ni Elisante John wa Radio Cluods na Nipashe na
wa pili kulia ni Awilla Sila wa Mwananchi na The Citizen.
Baadhi
ya viongozi wa SACCOS za mkoa wa Manyara na Singida, wakipata ‘msosi’
muda mfupi baada ya kukabidhiwa vyeti na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt.
Parseko Kone.(Picha na Nathaniel Limu).
Na. Nathaniel Limu
Benki
ya CRDB tawi la mkoa wa Singida imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya
shilingi biloni 1.4 kwa SACCOS saba za mkoa wa Singida na Manyara.
Akizungumza
kwenye hafla ya utoaji wa vyeti kwa SACCOS za mikoa ya Manyara na
Singida zilizopta mikopo kutoka mfuko wa uwezeshaji (Mwananchi
Empowerment Fund), Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amesema
SACCOS nne za mkoa wa Singida, zimekopeshwa zaidi ya shilingi milioni
255.5 sawa na aslimia 3.32 ya fedha hizo, wakati SACCOS tatu za mkoa wa
Manyara zenyewe zimekopeshwa zaidi ya shilingi bilioni 1.2.
Kuhusu
marejesho, Dkt. Kone amesema hadi kufikia Julai 31 mwaka huu, kiwango
cha urejeshaji kilifikia aslimia 94.4.Kwa upande wa mkoa wa Singida
pekee, kilifikia asilimia 91.7.
Amesema
hata hivyo ipo tatizo la urejeshaji kwa SACCOS ya Kumekucha ya Itigi
Manyoni ambayo ilikopeshwa jumla ya shilingi 84,472,000.
Fedha
hizo zilipaswa ziwe zimerejeshwa kabla ya Agosti 31 mwaka huu, lakini
hadi sasa SACCOS hii inadaiwa shilingi 21,168,000 ambazo ni asilimia 25
ya mikopo iliyotolewa kwa mkoa wa Singida.
Dkt .Kone amesema mbaya zaidi ni kwamba wengi wa viongozi wa SACCOS hiyo ni miongoni mwa wadaiwa sugu wa mikopo hiyo.
SACCOS za Lusilille na Tumaini za Manyoni na Jipe moyo ya Iramba zilishamaliza kurejesha mikopo yao.
Kwa
upande wao viongozi wa SACCOS hizo wameomba muda wa kurejesha mikopo
uongezwe zaidi ili waweze kupata muda wa kutosha kupata faida ya
itakayotosheleza kulipa mikopo na kubakiwa na akiba ya kukidhi
mahitaji.







No comments:
Post a Comment