Pages

KAPIPI TV

Thursday, September 20, 2012

MBUNGE ADAIWA KUMFANYIA KAMPENI MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA UYUI

Na Hastin Liumba,Uyui

MBUNGE wa jimbo la Tabora Kaskazini,mkoani hapa,Shaffin Sumar,amedaiwa
kumfanyia kampeni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui,Abdalah
Kazwika,ili aweze kurejea kwenye nafasi hiyo katika uchaguzi wa ngazi
ya wilaya mapema mwezi septemba 29,2012.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa mbunge huyo kwa
tiketi ya CCM aliwaagiza kwa barua, makatibu kata 14 kuandaa vikao vya
halmashauri kuu za kata ili azungumze nao ilihali akitambua kuwa
mwenye jukumu hilo ni katibu wa CCM wilaya.

Katika barua yake kwa makatibu kata hao,ameomba kufanya ziara katika
kata 14 za jimbo hilo,huku akiambatana na mwenyekiti wa sasa ambaye
anamalizia muda wake Abdalah Kazwika, hali ambayo wanachama kadhaa
wanahoji ni vipi katibu wa CCM wilaya hiyo Flavian Wangwe amekaa
kimya.

Chanzo cha taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo,
kimebaini kuwa mbunge Shaffin Sumar,ameanza kumfanyika kampeni
mwenyekiti wa sasa anayemaliza muda wake Abdalah Kazwika,kwani ni
maswahiba toka uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwani walisaidiana sana.

Kwa mujibu wa barua hiyo kwa makatibu kata hao,(gazeti hili ina kopi
yake),mbunge Sumar ameandika kuomba aandaliwe halmashauri kuu katika
kata 14 akianza na ziara hiyo mwezi septemba 19 atakuwa kata ya
Ibelamilundi na Isikizya.

Aidha katika ziara hiyo pia mwezi septemba 20 kata ya Magiri na
Nsimbo,mwezi septemba 21, kata za Upuge na Ikongolo,mwezi septemba 22,
kata ya Mabama na Ilolangulu.

Aidha ratiba hiyo ya ziara inaonyesha mwezi septemba 23, Ufuluma na
Ndono na septemba 24 kata za Usagali na Ibiri atapumzika kidogo na
mwezi septemba 28, kata za Shitage na Bukumbi ikiwa ni ziara ya siku
10.
 

Mtandao  huu ulimtafuta mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini,Shaffin
Sumar,kuzungumzia madai hayo  ambapo alisema na kukanusha kuwa hakuna
kitu cha namna hiyo ni uzushi tu.
’’Siyo kweli madai hayo na kwamba alikiri kuwa yuko ziara ya kawaida
tu kama mbunge na siyo vinginevyo.”

Aidha baada ya hapo mbunge huyo alituma ujumbe mfupi katika simu yake
uliosomeka hivi,”Sijafanya lolote wala sijui majina yatakayorudishwa
na NEC .’’ulisomeka hivyo ujumbe huo kwa njia ya SMS.
 

Mtandao huu pia ulimtafuta mwenyekiti wa wilaya anayemaliza muda
wake,Abdalah Kazwika,hakupatikana ofisini kwake baada ya kujibiwa kuwa
yuko ziarani akiambatana na mbunge Shaffin Sumar.

Aidha mtandao ulifanya juhudi kumtafuta mwenyekiti huyo kwa njia
ya simu ya kiganjani,lakini ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa na hata
alipotumiwa ujumbe mfupi SMS hakujibu chochote.

Katibu wa chama cha mapinduzi,(CCM),wilaya ya Uyui,Flavian Wangwe,ili
kuthibitisha na kuzungumzia hayo,alisema ni kweli ana taarifa hizo na
anafatilia kubaini ukweli.

Wangwe aliueleza mtandao huu ofisini kwake kuwa kama mbunge amefanya
hayo kuandika barua kwa makatibu kata kuwaeleza wamuandalie vikao vya
halmashauri za kata ni batili kanuni haziruhusu hasa kipindi hiki cha
uchaguzi.

“Aaaa!ndugu yangu una taarifa ya ziara hiyo katika kata ambazo hata
mimi nimesikia…..nafatilia sana nikibaini vikao vitaamua,na ni kinyume
cha taratibu na kanuni za chama, kwa kipindi hiki cha uchaguzi.”
alisema Wangwe.

Aidha katibu huyo alisema licha ya  mbunge huyo kuandaaliwa vikao vya
halmashauri kuu za kata ni batili kwani kanuni zinampa madaraka yeye
kama katibu wa wilaya na siyo mbunge.

Alisema kipindi hiki cha uchaguzi haipaswi vikao wala ziara yoyote
kufanyika kwani taratibu lazima zifuatwe na yeye kama katibu wa wilaya
hatokubali kanuni zipindishwe.
 

Katika kinyang`anyro hicho waliochukua fomu kuwania nafasi ya
mwenyekiti ni Abdalah Kazwika anayetetea nafasi yake,Musa
Ntimizi,Hamis Bundala.

No comments: