Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya marehemu Khalid Said na mkewe Amina Ally yaliyotokea Kijiji cha Inala na mauaji ya aliyekuwa Afisa mifugo manispaa ya Tabora Severine Tesha yaliyotokea mjini Tabora katika siku za hivi karibuni.
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mume na mke yaliyotokea Kijiji cha Inala,kutoka kulia ni Mheshimiwa Sakalambi Maganga,wapili yake ni Mabula Masanja na anayefuata ni Jumanne Mohammed wakisubiri kusimama mizimbani kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mjini Tabora.
Jumanne Mohammed na Mabula Masanja wanaodaiwa kukodiwa na Mheshimiwa Sakalambi Maganga kufanya mauaji ya mume na mke Kijiji cha Inala manispaa ya Tabora
Mheshimiwa Sakalambi Mganga akiwa anarudishwa kwenye chumba maalumu cha watuhumiwa na waharifu wakati alipofikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Khalid Said na mkewe Amina Ally.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika mahakama hiyo.

JESHI LA POLISI LAWAFIKISHA MAHAKAMANI WAUAJI
Jeshi la Polisi mkoani Tabora leo limewafikisha mahakamani
watuhumiwa watano wa kesi za mauaji ya watu watatu yaliyototekea wiki hii
katika matukio mawili tofauti mkoani humo.
Watuhumiwa hao watano walifikiwa mahakamani wakiwa chini ya
ulinzi mkali wa askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa na silaha huku viwanja vya
mahakama hiyo vikigubikwa na wimbi la utulivu wa kutosha.
Kwa mara ya kwanza
watuhumiwa hao watatu kati yao Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Bw.Esmail
Ngaile,mkaguzi mwandamizi wa jeshi la Polisi Wilbrod Mwombeki akisoma maelezo ya
kesi ya mauaji ya watu wawili mke na mume ,watuhumiwa Jumanne Mohammed,Mabula Masanja na
Mheshimiwa Sakalambi Maganga, mnamo tarehe 9/7/2012 saa moja jioni huko katika
kijiji cha Inala waliwaua Khalid Said na mkewe Amina Ally kinyume cha sharia
kifungu 196 sura 16 kanuni ya adhabu.
Hata hivyo maelezo yaliyotolewa na hakimu mkazi
mfawidhi Bw.Ngaile alisema mahakama yake
kisheria haina uwezo wa kuanza kusikiliza shauri hilo na hivyo kuamuru kurudishwa rumande na
kwamba kesi haina dhamana.
Aidha kuhusu kesi ya mauaji ya aliyekuwa daktari wa mifugo
wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Severine Tesha aliyeuawa kwa kupigwa
risasi,watuhumiwa wawili Kawombwe Mahmudu wa Ally Hassan Mwinyi na Phosti
Anderson mkazi wa Chemchem hapa Tabora mjini,imedaiwa na mkaguzi huyo wa Polisi
kuwa watuhumiwa hao kinyume na kanuni ya adhabu kifungu 196 sura ya 16 wote kwa
pamoja walishirikiana kufanya mauaji ya daktari huyo wa mifugo kwa kumpiga risasi
iliyosababisha kifo chake.
Licha ya upelelezi kuwa
hauja kamilika watuhumiwa wote watano wa kesi zote mbili watafikishwa tena
mahakamani mnamo tarehe 26/7/2012 kwa ajili ya kutajwa kwa kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment