Na Mohammed Mhina, Handeni
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku Galawa, amepiga marufuku shughuli zote za
uvunaji wa mazao ya misitu katika wilaya ya Handeni na kuunda tume ya
kuchunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na vitendo vya ukataji wa
miti ya mbao na mkaa.
Mkuu
huyo wa mkoa amechukua uwamuzi huo baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa
wa misitu ambapo aliwakamata watu wawili kwa uharibifu hao uliokuwa
ukifanyika kwa kisingizio cha kuanzisha mashamba mapya.
Bi.
Galawa amesema kuwa tume hiyo itawashirikisha watumishi wa Idara ya
Maliasi na miisitu, Jeshi la Polisi pamoja na watumishi wa halmashauri
ya Wilaya ya handeni.
Amesema
kwa vile baadhi ya watu wanaokamatwa katika maeneo ya misitu wamekuwa
wakidai kuwa wana vibali vya uvunaji wa mazao ya misitu, kwa hiyo timu
hiyo itachunguza uhalali wa vibali hivyo na mtoaji.
Bi
Galawa amesema amefikia uamuzi huo baada ya kushukudia uharibifu mkubwa
wa mazingira katika wilaya ya Handeni na kuwakamata watuhumiwa wawili
waliokuwa kwenye msitu wa Kang’ata wilayani humo wakiendelea na ukataji
miti ya uoto wa asili.
“Tume
hiyo itachunguza nani ana kibali, kimetolewa na nani na cha muda gani”.
Amesema Bi Galawa na kuongeza kuwa kimsingi serikali haiwezi kukaa
kimya huku ikiona kuna baadhi ya wananchi wanaoharibu misitu na kuongeza
upotevu wa mvua.
Watuhumiwa
waliokamatwa na mkuu huyo wa mkoa kwa uharibifu wa misitu ni Abraham
Yameti(50) na Augostine Jacob(42) wote wakazi wa Kang’ata wilayani humo.
Mara
baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Polisi kwa kushirikiana na
Maafisa Maliasili nao walianzisha operesheni kali na kuwakamata
watuhumiwa wengine pamoja na wamiliki wa maghala ya mazao ya misitu
yaliyovunwa kinyume cha sheria.
Mazao
yaliyokamatwa ni kiasi kikubwa cha mbao ambazi zilikamatwa katika
viwanda viwili vikubwa vinavyomilikiwa na watu binafsi mjini Handeni.
Watuhumiwa
waliokamatwa katika operesheni hiyo ni Paul benedict(52) na Ali
Mrisho(31) wote wakazi wa Vibaoni mjini Handeni ambao walip atikana na
mbao zitokanazo na ukatwaji ovyo wa misitu wilayani Handeni.
Mwanzoni
mwa wiki iliyopita Mkuu wa wilaya ya handeni mkoani humo Bw. Muhingo
Rweyemamu alimkamata mmoja wa watumishi wa Idara ya Misitu wilayani humo
akisafirisha magogo yaliyovunwa kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment