Na Mohammed Mhina, Handeni
MKUU wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu, ameipiga
marufuku Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwauzia maji wafanyabiashara
wakubwa wa maji na kuongeza uhaba wa bidhaa hiyo kwa wananchi wa kawaida
katika mji wa Handeni.
Mkuu
huyo wa wilaya amesema kuwa wafanyabiashara hao ambao wanauziwa maji
kwa bei ya shilingi 18,000 kwa boza lente ujazo wa zaidi ya lita 12,000
sawa na ndoo 600 na huwalangua wananchi kwa kuwauzia maji hayohayo kwa
bei ya shilingi kati ya 300 na 500 kwa ndoo moja.
Bw.
Muhingo amesema kuwa wafanyabiashara hao kwa kutumia magari hayo yenye
maboza wamekuwa wakijipatia faida kubwa ya kati ya shilingi 180,000 na
300,000 kwa kila gari moja lenye boza la ujazo huo wa lita 12,000.
Hata
hivyo Bw. Mhingo amesema kuwa hatua ya wafanyabiashara hao kupeleka
magari yao hadi kwenye bwawa hilo kumekuwa kukiongeza uharibifu wa
mazingira kwenye chanzo hicho cha maji wilayani Handeni.
Bw.
Muhingo amesema amebaini kuwa, uhaba wa maji unaotangazwa kuwepo
wilayani humo kwa muda mrefu sasa ni wa bandia na kwamba bwawa lililopo
mjini Handeni likihudumiwa vizuri maji yake yanaweza kutosheleza kwa
msimu wa mwaka mzima bila ya kuwepo kwa shida ya maji katika mji huo.
Amesema
pamoja na uchakavu wa miundombinu ya maji kati mji huo, lakini maji ya
bwawa hilo yanaweza kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali ya mji
huo tofauti na inavyoelezwa na waliowengi kuwa Handeni kuna shida kubwa
ya maji.
Mkuu
huyo wa wilaya ya handeni amesema kuwa ingawa mashine ya maji iliyopo
katika Bwawa hilo ina uwezo wa kufanya kazi kwa muda wa saa 22 kwa kila
siku kwa kusukuma lita 45,000 za maji kwa saa moja, lakini amesema
katika hali ya kushangaza, maji hayo yalikuwa yakielekezwa katika maeneo
ya visiwa vya wafanyabiashara wakubwa huku wananchi waliowengi wa mji
huo wakikosa maji kwa muda mrefu ama kuyanunua maji hayo kwa bei ya juu
kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Amesema
baada ya kubaini hivyo, Mkuu huyo wa wilaya alitoa maelekezo kwa
wafanyakazi wa Idara ya maji kuhakikisha kuwa wanasambaza maji kwa watu
wote na katika mabomba ya umma ili yaweze kuwanufaisha wakazi wote wa
mji huon a vitongoji vyake.
Bw.
Muhingo amesema ili kukomesha kabisa tatizo la maji wilayani humo,
ofisi yake inaangalia uwezekano wa kuchimba mabwawa katika maeneo
mbalimbali yakiwemo yale ya vijiji ambayo yana uhitaji mkubwa wa maji
kwa wananchi pamoja na mifugo yao.
Hata
hivyo, Mkuu huyo wa wilaya ya Handeni pia ameutaja mkakati mwingine wa
kuipatia wilaya hiyo maji ya uhakika kuwa ni kuimarisha mradi wa HTM wa
kuvuta maji kutoka katika mto Pangani kwenda mjini Handeni.
Kwa
upande wao, baadhi ya wananchi wa wilaya ya Handeni wamepongeza juhudi
za Mkuu huyo wa wialaya na kusema kuwa uhaba wa maji kwenye mji huo
umekuwa ukisababishwa na watumishi wachache wa Idara ya maji ya mji huo
wenye uroho wa kujitajirisha huku wananchi wakihangaika na kuilaumu
serikali kwa ukosefu wa maji.
No comments:
Post a Comment