Na Mohammed Mhina, wa Jeshio la Polisi zanzibar
Uwamuzi
huo umetangazwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi, wakati akipokea misaada ya fedha kutoka Mfuko wa Pensheni wa
watumishi wa Serikali za Mitaa na Radio Coconut.
Balozi
Iddi amesema kuwa pamoja na kuisimamisha meli hiyo kutoa huduma za
usafiri kwenye bahari ya Hindi, pia imewataka watu wote wanaotaka
kununua meli kuleta kwanza aina na muundo wa meli wanayotaka kuinunua
na imetumika kwa muda gani.
Lakini
amesema meli ambazo zimeshaingia na kusajiliwa, nazo zinafanyiwa
uchunguzi ili kubaini ubora na umri wake tangu ianze kufanya kazi kabla
ya kuingizwa nchini kwa biashara ya kusafirisha abiria.
Hata
hivyo amesema kuwa Serikali inajipanga kununua meli ya uhakika
itakayotoa huduma ya usafiri majini kati ya Zanzibar na Pemba na
Zanzibar na dar es Salaam ili kupunguza mashaka kwa wasafiri.
Mfuko
wa Pensheni ya Watumishi wa Serikali za Mitaa NLPF kupitia Mkurugenzi
wake Bw. Andrew Kuyeyama umetoa shilingi milioni 5 na Bw. Ali Khatibu
Dai wa Radio Coconut ametoa mchango wa shilingi milioni moja zote
zikiwa kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu na za mazishi kwa
wafiwa.
No comments:
Post a Comment