Timu ya Azam FC imeibuka kidedea kwa kuifunga mabao matatu kwa moja timu ya Simba ya Tanzania katika michuano ya Kombe la Kagame iliyokuwa ikichezwa jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam hatua ambayo imeipa nafasi ya kuingia nusu fainali ya mashindano hayo ya klabu bingwa ya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na kati.
Mchezaji wa Azam aliyeng'ara katika mtanange huo wa leo alikuwa John Raphael Bocco maarufu ‘Adebayor’ aliyefunga
mabao yote matatu, ambapo bao moja la kwanza alilifunga katika kipindi cha kwanza na mengine kipindi cha pili.
Aidha kwa upande wa mahasimu wao timu ya Simba ilijipatia bao la kufutia machozi kupitia mchezaji wake Shomari Kapombe ambaye alilifunga bao hilo kwa juhudi zake bina mnamo dakika ya 53.
Sasa Nusu Fainali zote katika mashindano hayo ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati zitafanyika keshokutwa Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, ambapo Azam wataanza na Vita na baadaye Yanga na APR saa 10:00 jioni.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam kilikuwa na wachezaji ; Deo
Munishi, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre
Michael Balou/Ramadhan Chombo, Kipre Herman Tcheche/George Odhiambo ‘Blackberry’,
Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo na Khamis Mcha ‘Vialli’/Jabir Aziz.
Wakati kikosi cha wekundu wa msimbazi
Simba SC kilikuwa na ; Juma
Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde,
Uhuru Suleiman/Kiggi Makassy, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na
Jonas Mkude/Amri Kiemba.
No comments:
Post a Comment