Pages

KAPIPI TV

Saturday, July 14, 2012

"NI BORA WANGENIUA MIMI KULIKO WALIVYOMUUA KIKATILI MTOTO WANGU"Ni matokeo ya kugombea ardhi ya urithi,majambazi yatumwa kuua mama yakaua mtoto wa mwaka mmoja na nusu.

Ndalo Emmanuel Msemakweli(39)akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kufuatia kujeruhiwa kwa mapanga pamoja na kuuawa kwa mtoto wake mdogo Lucas Paul mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu katika kijiji Kipya Mayombo wilayani Uyui mkoani Tabora.

Mahojiano kati ya mtanado huu na Bi.Ndalo Msemakweli:-

''Wakati nakwenda kuchuma mlenda huko chini mbugani,ghafla nilimuona shemeji yangu aitwaye Luchoma Kiyenye akiwa na vijana wawili,...na nilivyowapita nilisikia kwa nyuma yangu wakisema kuwa mume wake kwasasa hayupo kwahiyo mambo yatakwenda vizuri tu"alisema Ndalo.

Kwani walivyosema hivyo wewe ulielewa nini?

''Mi nilishikwa na hofu  kwakuwa huyo shemeji yangu tunaogmvi naye kwa muda mrefu na hata viongozi wa vijiji na vitongoji vilivyoko hapa jirani wanajua,ndio maana nilianza kuogopa hata nikashindwa kuchuma hiyo mboga niliokuwa nimekwenda kutafuta"

"Ilipofika usiku walikuja watu nyumbani kwangu na kuanza kuvunja mlango,nikawa nimezuia hapo mlangoni wakati na usukuma,...ndipo wakapata nafasi ya kupenyeza upanga wakaanza kunikatakata sana lakini sikuachia kabisa hadi hapo walipoamua kuupitisha upanga huo kwa juu na kuanza kukata tena na kwa bahati mbaya wakamkata mtoto wangu Lucas eneo la paji la uso......mtoto akali mara moja na kufa papo hapo"alisema Ndalo

"Nilipoona mtoto wangu amekufa nikazidisha kupiga kelele na kuufungua mlango nikawaona wale watu waliokuwa na Shemeji yangu Luchoma,....nikawa napiga kelele watu wakaja kunisaidia wakati huo watu hao majambazi wakakimbia"

Baada ya kuja majirani hao kuja kukusaidia nini kiliendelea?

"Nilikuwa nalia huku namtaja shemeji yangu Luchoma na hivyo majirani hao walifahamu nini kinachoendelea kwa kuwa walikuwa wanatambua ugomvi wa ardhi uliopo baina ya mimi na shemeji yangu Luchoma"

"Watu walinisaidia kumtoa mtoto wangu mgongoni nilikokuwa nimembeba kwakuwa nilikuwa siwezi hata kuifungua nguo(mbebeo)kutokana na nilivyokuwa nimekatwakatwa mikono nadamu inavuja kwa wingi sana".

Ndalo alichukuliwa na kufikishwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kwa matibabu zaidi wakati Jsehi la Polisi mkoani Tabora likiwa linamshikilia Luchoma Kiyennze(38)kuhusiana na tukio hilo ambalo inadaiwa kuwa alikodi waharifu wawili kuja kumdhuru shemeji yake kutokana na mzozo huo wa ardhi.           

No comments: