Walimu wa Shule za msingi na Sekondari walipovamia ofisi ya halmashauri Nzega wakishinikiza kulipwa haki zao
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Walimu Wilayani Nzega wakiwa katika kikao cha pamoja ofisini kwao kabla ya kuvamia kikao cha baraza la madiwani.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega wakisikiliza kwa makini walipovamiwa na viongozi wa Chama cha Walimu Nzega kueleza kilio chao.
Mwenyekiti wa CWT Nzega Komredi Peter Mipawa Kashindye akizungumza mbele ya baraza la madiwani.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Bw.Pelle Anthony akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Walimu Wilayani Nzega wakiwa katika kikao cha pamoja ofisini kwao kabla ya kuvamia kikao cha baraza la madiwani.
Mwenyekiti wa CWT Nzega Komredi Peter Mipawa Kashindye akizungumza mbele ya baraza la madiwani.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Bw.Pelle Anthony akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Komredi Peter Mipawa akiwa na walimu nje ya jengo la halmashauri wakisubiri tamko la madiwani kuhusu kero zao dhidi ya mkurugenzi.
ZAIDI YA WALIMU mia nne na hamsini wamelazimika kuvamia
kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega na kulitaka
baraza hilo kusitisha ajenda walizokuwa wakijadili ili watoe nafasi ya
kusikiliza matatizo na kero walizonazo zinazodaiwa kusababishwa na mkurugenzi
wa halmashauri hiyo.
Amini usiamini ilikuwa kama mchezo wa kuigiza hapo jana
katika ofisi za Chama cha Walimu wilayani Nzega ambapo walimu hao walikutana
kuzungumzia namna ya kudai haki zao kutoka kwa mwajiri ambaye ni mkurugenzi.
Moja kati ya haki muhimu ambazo ndio zilizua kizaazaa hicho
ni baadhi ya walimu waliandikiwa barua za kupandishwa madaraja(Promosheni)kasha
baada ya siku kadhaa ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw.Kyuza Kitundu ikaanza
kuwaita mwalimu mmoja baada ya mwingine kumtaka arejeshe barua aliyopatiwa kwa
kigezo kuwa serikali haina fedha za kuwalipa kutokana na kupandishwa kwa
madaraja hayo.
Hili lilikuwa tukio ambalo likazua hata madai ya baadhi ya
walimu waliokuwa wakidai marimbikizo ya mishahara na haki stahili nyingine
ambazo wamekuwa wakisumbuliwa kila kukicha.
Kwaupande mwingine siku hiyo ya kizaazaa hiki tarehe 11 Mei
2012 ilikuwa ni siku ya kikao cha baraza la madiwani hivyo walimu hao wakiwa
wanajadili ofisni kwao wakaazimia kufunga safari na kuvamia kikao hicho na ndipo bila kumumunya maneno viongozi wa CWT
Nzega walitamka mbele ya madiwani endapo kama watashindwa madiwani
kumuwajibisha mkurugenzi watakuwa tayari kumfikisha mahakamani haraka
iwezekanavyo.
Huku wakihusiana kupunguza jazba baadhi ya madiwani
wakaonesha kukerwa kwao na madudu ambayo halmashauri hiyo imekuwa ikiyafanya na
hivyo kufikia uamuzi wa kuitaka serikali imuondoe mkurugenzi huyo katika
halmashauri yao.
Hata hivyo pamoja na CWT kuwapa mzigo madiwani kuhusu madai
yao kuyashughulikia,walimu hao wamedai kupitia chama chao wataandamana hadi
ofisi ya mkurugenzi na kumfungia mlango ikiwa ni sehemu ya shinikizo la yeye
kuwajibika.










No comments:
Post a Comment