Mmoja
wa wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria mafunzo juu uchimbaji
wenye tija KALAEL IGUMI akionyesha cheti chake alichotunukiwa baada ya
kumaliza mafunzo.
Baadhi
ya wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Singida waliohudhuria mafunzo ya
siku tatu yaliyohusu pamoja na mambo mengine kuboresha uchimbaji wao na
kuwa na tija zaidi. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na.Nathaniel Limu-Singida
Wizara
ya nishati na madini, imeombwa kuwachukulia hatua kali za kisheria
wachimbaji wote wadogo, wasiofukia mashimo wanayoyachimba wakati
wakitafuta madini.
Rai
hiyo imetolewa na wachimbaji wadogo 50 wa madini, waliomaliza mafunzo
yao juzi ambayo pamoja na mambo mengine utafutaji na uchimbaji salama
wa madini migodini.
Wamesema
wachimbaji wengi wadogo wa madini, wamekuwa na utamaduni wa kuchimba
mashimo wakati wakitafuta madini, lakini mashimo hayo huyaacha bila
kuyafukia kama sheria inavyowataka na hivyo husababisha ajali ambazo
wakati mwingine, huchangia binadamu kupoteza maisha yao na mali zao.
Akielezea
mipango madhubuti serikali kuimarisha sekta hiyo Mjiolojia Sophia Omari
amesema “Uzalishaji wa madini, unaleta mapato kwa serikali, unasaidia
kupatikana kwa ajira na mapato kwa wakazi wa vijijini na unapunguza
umaskini”.





No comments:
Post a Comment