MAWAZIRI MSIBWETEKE,MJIPANGE KUITUMIKIA NCHI YETU-Mh.HAMISI KIGWANGALLA
"Hongereni
Mawaziri wote mlioteuliwa na Rais wetu. Tunawatakieni kazi njema,
msibweteke, mjipange kuitumikia nchi yetu.
Heshima na imani tuliyonayo
kwenu ni kubwa sana. Binafsi siwategemei mfurahie sana maana ni mzigo
mzito mliobebeshwa, na kipindi tulichopo si rahisi sana, tupo kwenye
kipindi cha mpito na watanzania wanahitaji mabadiliko kwa kasi ya ajabu!
Ubunifu, uaminifu, uadilifu, uvumilivu, uchapakazi,
urafiki na uzalendo kwa Taifa unahitajika sana sasa kuliko kipindi
kingine chochote katika historia ya nchi yetu.
Sisi wabunge, I for one
at least, tutaendelea kuwasukuma mfanye kazi iliyotukuka kwa Taifa letu,
mkiiba, mkitafuna, mkizembea tutaendelea kuwafichua tu bila aibu wala
huruma. Mkishindwa kazi, msisubiri shinikizo la kujitoa, watendeeni
watanzania haki, mtendeeni Rais wetu haki, mjitoe wenyewe asubuhi na
mapema!"
No comments:
Post a Comment