KLABU ya Chelsea imetwaa Kombe la FA hivi
punde tu, kwenye Uwanja wa Wembley baada ya kuifunga mabao 2-1 Liverpool.
Shukrani kwao, Ramires na Didier Drogba
walioifungia mabao hayo Uwanja wa Wembley
jioni hii, wakijiandaa kuwa mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
dhidi ya Bayern Munich, Ujerumani.
Ramires alifunga bao la kwanza baada ya
makosa ya Jay Spearing kabla ya Drogba kufunga la pili na Andy Carroll aliyetokea
benchi kuifungia Liverpool la kufutia machozi kwa kutumia makosa ya John Terry.
Lakini Liverpool ni kama walinyimwa bao la
kusawazisha na refa baada ya mpira uliopigwa na Carroll kuonekana kabisa
umevuka mstari wa goli, lakini refa akachomoa.
No comments:
Post a Comment