Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 9, 2012

MAKAMU WA RAIS DK.BILALI AFUNGA MAANDALIZI YA SENSA AWAMU YA KWANZA - TABORA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa Ramani ya makazi itakayotumika na Makarani katika zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na makazi, na kusikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sensa, Hajat Amina Said Mrisho, wakati Makamu alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Picha ya Ramani ya Tanzania, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Vincent Mugaya, baada ya kufunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuhakiki Ramani ya iliyoandaliwa kwa zoezi la kuhesabu Sensa ya watu linalotarajia kuanza Tarehe  26 Mwezi Agosti, mwaka huu, wakati alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Mkoani Tabora wakati akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu akiwasili kwenye uwanja wa chipukizi mkoani tabora kufunga awamu ya kwanza ya maandalizi ya  sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Kutoka kushoto;Katibu Tawala mkoa wa Tabora Bi.Kudra Mwinyimvua akiwa na Mkurugenzi mkuu ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa.
 Ngoma ya wenyeji wa mkoa wa Tabora maarufu Maswezi.
 Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Tabora ambao walihudhuria katika Sherehe hizo uwanja wa Chipukizi Tabora mjini.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akisoma taarifa fupi ya maendeleo ya mchakato wa uhamasishaji wa Sensa ya watu na makazi.
 Baadhi ya viongozi wa dini kutoka kushoto ni Sheikh wa mkoa wa Tabora Shaban Salum,Mwenyekiti wa Bakwata mkoa Haruna Mbeyu,Baba Askofu jimbo kuu katoliki Tabora Paul Ruzoka,Askofu Chakupewa Anglikana Tabora na meya wa manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewji

Askari wa Jadi maarufu Sungusungu

No comments: