Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi
Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo
iliyofanyika leo Mei 10, 2012 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo upande wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Dkt. Mussa Juma (wa pili kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
(Utawala Bora) George Mkuchika na (kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Pius
Maneno. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Tuzo ya Heshima, Ibrahim
Mohamed Kaduma, kwa kuwa Mwanachama wa
Heshima wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT), wakati wa uzinduzi wa
Taasisi hiyo uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam
leo Mei 10, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na
Viongozi na baadhi ya wadau walioshiriki
katika hafla hiyo ya uzinduzi, baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi
Tanzania (IoDT) uliofanyika leo Mei 10 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar
es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo
vya habari mbalimbali, baada ya kuzindua Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT)
leo Mei 10, 2012, uzinduzi uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini
Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake wakati akizindua rasmi Taasisi
ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) alioizindua leo Mei 10, 2012, kwenye Hoteli ya
Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal amesema
kwamba Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania(IoDT) itasaidia kuboresha
utendaji kazi kwa wakurugenzi wa taaasisi na mashirika mbalimbali na kuboresha utawala bora .
Aidha amewataka wananachi kuiunga mkono taasisi hiyo kwa kuwa ni chombo muhimu cha kikachosaidia kutoa mafunzo kwa viongozi hao na kuwaunganisha ili kuboresha utawala bora.
Kauli hiyo ilitolewa na Dk. Bilal wakati akizindua taasisi hiyo leo (jana) kwenye hafla iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency jijini Dares Salaam.
“Taasisi hii itakuwa inawachukulia hatua baadhi ya wakurugenzi ambao hawatafuata maadili na kanuni za IoDT ,ikiwemo kubadilishna mwazo na kupata uzoefu,” alisema Dk. Bilal.
Naye Mwenye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania(IoDT), Pius Maneno alisema taasisi hiyo ina wanachama 19 ambao kila mmoja amechangia sh. milioni 10 kwa ajili ya uanzishaji.
Alisema lengo kuwa la taasisi hiyo ni kutoa mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi hao , kujenga mtandao na kuandaa mikutano mbalimbali.
Katika
uzinduzi huo , Profesa Geoffrey Mmari kutoka Chuo Kikuu cha
Tuamini(TUDARG) na Mwenyekiti wa African Life Assurance , Ibrahim
Mohamed walitunikiwa cheti cha uanachama wa heshima.







No comments:
Post a Comment