Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akisalimiana na mmoja wa wadau waliohudhuria hafla ya kifungua kinywa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, ambayo imeandaliwa na Benki hiyo kwa pamoja na Benki ya PTA ya Kenya ikiwashirikisha wateja wake.
Pichani juu na Chini ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akizungumza na wageni waalikwa katika hafla iliyoandaliwa kwa pamoja na Benki hiyo na Benki ya PTA ya Kenya ambapo amesema benki hiyo inafaraja kuwa moja wapo ya benki inayochangia kukuza maendeleo ya kiuchumi hapa nchini.
Moja ya meza za wadau waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya washiriki hao wakifuatilia kwa makini hotuba ya kuwakaribisha iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Kimei.
Benki ya CRDB leo imewakutanisha pamoja jumuiya ya wafanyabiashara kwa kushirikiana na wadau wao Benki ya PTA ya jijini Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza leo na wadau na wateja wa benki ya CRDB, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei amesema lengo la kuandaa kifungua kinywa kwa pamoja na washirika wao Benki ya PTA kutoka Kenya, ni kubadilishana mawazo na kuangalia fursa muhimu za kibiashara zilizopo.
Amesema mkusanyiko huo wa kibiashara unalenga kuanzisha mazingira mazuri ya kibiashara ya kuwaweka pamoja wafanyabishara ili kupeana uzoefu kuhusiana na uandikaji wa michanganuo itakayopelekea kupata mikopo.
No comments:
Post a Comment