Pages

KAPIPI TV

Monday, March 5, 2012

TABORA YAKITHIRI KWA MAUAJI-RC FATMA MWASSA."Wastani watu wawili hadi wanne wanauawa kwa siku,Viongozi matumbo joto waogopa kutekeleza majukumu yao wahofia kuuawa"

MAZISHI;Safari ya mwisho ya aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui Bw.Mashaka Hassan Kalyuwa,mamia walihudhuria mazishi hayo yaliyoongozwa na mkuu wa mkoa wa Tabora huko kijijini nyumbani kwao Tutuo wilayani Sikonge. 
MADIWANI:Wakipokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri,Bw.Mashaka,nyumbani kwao,wakitutoa nje tayari kwa mazishi baada ya kufanya taratibu za kuuaga.
 Dr.GERSON NYADZI:Akitoa maelezo mafupi katika msiba huo na kuelezea mchango mkubwa alioutoa Marehemu Mashaka hasa katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika mradi wa Vijiji vya Milenia Mbola

MAJONZI:Baba mzazi wa marehemu Mashaka Kalyuwa,Mzee Hassan Kalyuwa akiwa na huzuni kubwa ya kuondokewa na mtoto wake mpendwa ambapo kwasasa inatajwa kuwa ni pigo kubwa ndani ya familia.   <> 
Mkuu wa mkoa akitoa pole kwa baba mzazi wa marehemu Mashaka,Mzee Hassani Kalyuwa wakati wa msiba huo. 
BI.FATMA  MWASSA:Mkuu wa mkoa wa Tabora wakati alipokuwa akitoa nasaha fupi kabla ya mazishi ya marehemu MASHAKA KALYUWA.  


 Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa aliongoza mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui marehemu Mashaka Kalyuwa aliyefariki kwa kipigwa risasi mnamo tarehe 2 marchi mwaka huu(2012) yaliyofanyika katika kata ya Tutuo wilayani Sikonge.

Katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo viongozi wa kada mbalimbali ndani ya  vyama vya siasa,serikali pamoja na taasisi mbalimbali,yalikugubikwa na wimbi la huzuni kwa waombolezaji hao kufuatia matokeo ya kifo hicho cha mauaji ya kinyama kwa njia za makusudi.

Kabla ya mkuu huyo wa mkoa kutaja rambirambi ya kiasi cha shilingi laki saba katika msiba huo,alikizungumzia kifo kilichomkuta marehemu Mashaka na namna kilivyoigusa serikali kwa kuwa marehemu Mashaka ni mmoja kati ya viongozi ambao watakumbukwa kwa mchango wao katika kuleta maendeleo ndani ya wilaya ya Uyui na mkoa mzima wa Tabora kwa ujumla.

Pamoja na kuzungumzia pengo kubwa aliloliacha marehemu Mashaka kwa kuondoka kwake,lakini tafsiri mbaya ikawa juu ya vitendo vya mauaji vinavyoendelea kujitokeza mkoa wa Tabora na pengine hata kuchafua taswira halisi ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

''Kwakweli jamani hili sasa imekuwa ni tatizo ambalo serikali haitalivumilia,haiwezekani vitendo vya mauaji kuendelea kila kukicha"alisema Bi.Fatma Mwassa huku akionesha kusikitishwa kwake na hali hiyo.

Pamoja na tamko hilo kwa upande mwingine mkuu huyo akafuatiza kauli nyingine ambayo ikabeba dhima juu ya kukithiri kwa vitendo hivyo vya mauaji Tabora,"KUANZIA SASA MTU YEYOTE ATAKAYE TOA TAARIFA ZA KUWAFICHUA WAUAJI TUTAMPATIA SHILINGI MILIONI MOJA,NA VIVYO HIVYO ATAKAYE TOA TAARIFA ZA KUTAKA KUFANYIKA MAUAJI MAPEMA KABLA ATAPATIWA LAKI TANO TASILIMU"

Kwa kauli hiyo ikawa ni sehemu ya kuwafariji baadhi ya viongozi hasa madiwani ambao kwasasa wamekuwa wakihofia maisha yao kila kukicha.

No comments: