Pages

KAPIPI TV

Monday, March 5, 2012

SERIKALI HAIWATENDEI HAKI WALIMU WA AJIRA MPYA - MGAYA

NICHOLAUS MGAYA:Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA akizungumza katika mkutano wa uchaguzi wa TUCTA tawi la mkoa wa  Tabora.
WILLIAM JOHN NTIBAHEZWA:Mwenyekiti mpya wa TUCTA mkoa wa Tabora akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo katika ukumbi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Tabora TUWASA.


Katibu mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA, Nicholaus Mgaya amesema bado serikalli haijawatendea haki walimu walioajiriwa hivi karibuni kufuatia kutowapatia malipo yao kwa wakati muafaka.

Mgaya alisema hayo wakati wa mahojiano mafupi  na mtandao huu mjini Tabora kufuatia kuwepo kwa  malalamiko kadhaa kwa walimu hao dhidi ya serikali kutokana na kutopatiwa haki stahili zao kwa wakati.

Alisema anashangazwa na kitendo cha serikali kuwaahidi walimu hao katika ajira mpya kuwalipa posho ya siku saba baada ya kuripoti katika vituo vyao vya kazi lakini wapo baadhi ya walimu hao wamepatiwa posho ya siku nne badala ya makubaliano yalivyokuwa hapo awali.

Kufuatia hali hiyo ameitaka serikali kurejea upya mikataba waliyoingia na walimu hao ambao kwasasa ajira waliyoipata imegeuka kuwa ni mateso.

"Kwakweli serikali hili suala la hawa walimu ingeliangalia kwa makini,hivi inakuaje unampatia mtu posho ya siku saba halafu anafanyakazi kwa zaidi ya siku thelathini kisha mshahara unamwambia asubiri pasipo kujua atapata lini"alisema Mgaya. 

Aidha kwa upande mwingine katibu mkuu huyo wa TUCTA amewaomba walimu kuvuta subira kwani Chama cha walimu C.W.T bado hakijashindwa kuwasaidia kudai haki stahili zao.

Hata hivyo ni hivi karibuni walimu hao ambao wameingia katika ajira mpya ya ualimu kwa mara ya kwanza wamekuwa na mikakati ya kutaka kuanzisha mgomo ambao hauna ukomo hadi hapo serikali itakapotekeleza madai yao. 

 

No comments: