Pages

KAPIPI TV

Monday, March 5, 2012

POLISI WANNE WALIOFANYA MAUAJI URAMBO WAFUKUZWA KAZI

SSP YUSUPH MRUMA:Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora
HALI HALISI YA MAUAJI YA HASSAN MGALULA:Askari Polisi hao wakati wakimchukua kwenye usafiri wa Bajaji ya mizigo huku wakiwa  wamemkanyaga bila kujali hali mahututi aliyokuwanayo marehemu Hassan Mgalula mara baada ya kipigo kikali kilichosababisha kifo chake hapo baadaye,INASEMEKANA KUWA  WALIPOFIKA  KITUONI  WALIFUNGUA  JALADA  LILILOONESHA  KUWA HASSAN  AMEPIGWA  NA  WANANCHI  WENYE  HASIRA  KALI......(Picha hii kwa hisani ya Nassor Wazambi-Mwenyekiti UVCCM wilaya ya Tabora mjini.) 

POLISI wanne waliokuwa wanashikiliwa Wilayani Urambo kwa tuhuma za kumuua mwananchi kwa kumpiga wamefukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora S.S.P Yusuf Mruma ametoa maelezo hayo ikiwa ni hatua za mwanzo za jeshi hilo kukabiliana na vitendo vilivyo kinyume cha sheria huku akisisitiza hatua hiyo inakwenda sambamba na kufikishwa mahakamani.

Polisi hao wanne inadaiwa kuwa walimpiga na kusababisha kifo chake mwananchi huyo aliyefahamika kwa jina la Hassan Mgalula,mkazi wa Mjini Urambo.

Amewataja Polisi hao kuwa ni  namba  G 3037 Pc Aidano, namba G 3836 Pc Jonathan, namba G 4836 Pc Mohamed na mwingine ni namba G 5382 Pc Khakimu.

Aidha Diwani wa kata ya Urambo mjini,Amatus Ilumba,amesema chanzo cha kipigo kwa kijana huyo ni ugomvi uliotokea baina yake na polisi mmoja wiki zipatazo  mbili zilizopita na  Jumatano walipokutana polisi na huyo aliwaita wenzake na kuanza kumpiga na baadaye kusababisha kifo chake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,Polisi hao walimpiga Mgalula pasipo kujali hadi kumfanya awe hoi huku akijisaidia haja ndogo na kubwa pasipo kupenda.

Mashuhuda hao walizidi kueleza kuwa Mgalula alifariki hata kabla hajafikishwa Hospitalini kutokana na hali yake aliyokuwa nayo huku wakiongeza kuwa hata Polisi wenyewe walijua kuwa tayari alikuwa amekwisha fariki.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira walikuwa na mpango wa kukivamia kituo cha Polisi Urambo ili kuhakikisha kuwa kama kweli uongozi wa juu wa jeshi hilo ngazi ya mkoa umechukua hatua ya kuwashikilia askari hao ili baadaye sheria iweze kuchukua mkondo wake.

No comments: