Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dr.Hussein Mwinyi na Balozi wa Ujerumani Bw. Klaus Brandes wakikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa jengo la Hospitali ya kisasa ya Milambo JWTZ Tabora.
Chumba maalum cha kisasa kwa ajili ya matibabu ya meno katika Hospitali ya Milambo.
Dr.Leslie Mhina:Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora akiangalia vitanda katika wadi ya kulazia wagonjwa katika hospitali hiyo.
CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI:katika hospitali ya Milambo
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dr.Hussein Mwinyi amefungua hospitali ya kisasa katika kambi ya jeshi la wananchi Milambo Tabora ambapo hospitali hiyo inatarajia kutoa huduma kwa askari,familia zao pamoja na wananchi waishio jirani na kambi hiyo.
Dr.Mwinyi pamoja na kupongeza serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la nchi hiyo kitengo cha Military Technical Advisory Group (GAFTAG) kwa kuwezesha msaada huo wa ujenzi pamoja na vifaa vya matibabu,lakini amesema changamoto iliyopo sasa ni upatikanaji wa madakatari bingwa.
Amesema ujenzi wa hospitali hiyo ya kanda ya magharibi na kati pamoja na vifaa umetekelezwa kwa gharama ya kiasi cha Euro milioni kumi huku ukiutaka uongozi wa ya jeshi Milambo kuitunza ili iweze kutoa huduma kwa ufanisi kwa askari,familia zao pamoja na wananchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment