MAMA MAGRETH:Akiwa na mtoto wake Wadi namba kumi na moja hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete
MAGRETH MASANJA:Mtoto mwenye umri wa miaka sita akiwa amelazwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kusukumizwa kwenye moto na mtu ambaye bado hajatambulika huko kijiji cha Mwakashindye Umanda wilaya ya Uyui.
Matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora yameendelea kushika kasi siku hadi siku.
Ingawa yapo baadhi ya matukio yamekuwa yakiripotiwa kwenye vyombo vya dola na kufanyiwa kazi na mengine kuachwa kama yalivyojitokeza, lakini kwa sehemu kubwa yapo ambayo hayaripotiwi popote na kwa maana moja ama nyingine yamekuwa pia yakisababisha madhara makubwa kwa binadamu na hata kusababisha vifo.
Ni matukio mawili ya wiki hii ambayo nayaweka bayana mbele ya mtandao huu ambayo ukiyatizama sura yake utaona kuwa ni matukio ya kinyama kwa watu wenye akili timamu na wala hayastahili kuachwa au kupewa mwanya wa kuwa endelevu.
Kwa mfano mtoto mdogo mwenye umri wa miaka sita anakumbana na dhoruba la kusukumiwa kwenye moto na hatimaye nguo zake kushika moto,..pamoja na kupiga kelele ya kutaka msaada lakini hakufanikiwa hadi hapo alipoanza kujiokoa mwenyewe ndipo akapata msaada toka kwa mama yake mzazi.
Hivi ni kweli kwamba ugomvi au mahusiano mabaya baina ya majirani ndio kisasi chake afanyiwe au kulipizwa kwa mtoto?...Kwanini iwe hivyo?....
Mama mzazi wa Magreth anasema hajui ni kwanini mtoto wake kuhusishwa na mambo ya wakubwa,....Lakini kibaya zaidi anasema alimkuta mtoto wake katikati ya moto huku mtoto mwenzake alikuwa pembeni akiendelea kucheka kwa sauti na furaha ya hali ya juu.
Anachana na hilo fikiria hili nalo.....Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 54 jina ninalihifadhi mkazi wa Bukumbi wilayani Uyui amelawitiwa kwa nguvu na mwanaume mmoja maarufu huko eneo la Ishihimulwa kwa jina la Rasta ambaye anachezesha kamari aina ya kolokolo.
Mzee huyo alisema amefanyiwa kitendo hicho kwa zaidi ya saa saba mfululizo huku akiwa ameshikiwa kisu kwa tishio la kutaka kuchomwa.
Alisema kuwa alishikwa na Rasta akisaidiwa na wenzake na kupelekwa kwenye bani(nyumba ya kukaushia tumbaku)ndipo shughuli hiyo ikaanza kwa kasi kuanzia majira ya saa sita usiku hadi asubuhi.
YAANI LAANA TUPU......
No comments:
Post a Comment