Pages

KAPIPI TV

Thursday, February 9, 2012

AJALI MWANAFUNZI AGONGWA NA PIKIPIKI...''AMBULANCE ZA HOSPITALI YA KITETE KUMBE MAPAMBO TU''


 AJALI;Mwanafunzi wa shule ya msingi Isike mjini Tabora amegongwa na pikipiki mchana wakati akitokea shule,...alikuwa anavuka eneo la pundamilia hapo shuleni kwao jirani na Posta Tabora...(Pichani Mwandishi wa habari wa gazeti la Majira Moses Mabula alipokuwa akimlaza kwenye kitanda hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete....Imeelezwa kuwa Moses akiwa na mwalimu wa Chuo cha Teofilo Kisanji Bi. Caroline pamoja na msamalia mwema mwingine walifika eneo la tukio na kumsaidia mwanafunzi huyo kumkimbiza hospitalini.


 
 
  Pikipiki iliyogonga  mara baada  ya kukamatwa



GARI MBILI ZA KUBEBEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA  MKOA  WA  TABORA  KITETE..........''KUMBE HIZI AMBULANCE NI MAPAMBO TU''

Iliwashangaza  baadhi  ya  watu  waliokuwepo katika hospitali hii  wakati ndugu wa mtoto Shafii Mashoka walipokuwa wakihitaji usafiri  wa kumpeleka mtoto huyu hospitali ya Nkinga kwa matibabu zaidi lakini juhudi  hizi ziligonga mwamba baada ya kuambiwa gari hizi hazitumiki kwa madai kuwa ni mbovu kwasasa.

Hali hii ilizua gumzo na hata kufikia baadhi ya watu kutoa matamko kuwa huenda gari  hizo zimeegeshwa kama zipo SHOW ROOM na si kwa ajili ya kusaidia wagonjwa kama ilivyo lengo kuu.



No comments: