Pages

KAPIPI TV

Thursday, February 9, 2012

MADIWANI KUWENI MACHO - RC FATMA MWASSA

 Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akisoma hotuba yake kwa mara ya kwanza tangu kushikilia wadhifa huo ambapo aliwaasa Madiwani kuwa macho katika kusimamia miradi ya maendeleo na hasa ya ujenzi kwakuwa miradi mingi imeonekana kufanyiwa ubadhirifu na baadhi ya watendaji katika halmashauri ya Manispaa ya Tabora.


 MADIWANI:Wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Tabora wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora kilichofanyika hivi karibuni.

Katika hotuba yake hiyo mkuu  wa mkoa Tabora Fatma Mwassa mbali ya kutoa mwongozo pia kwa kuwakumbusha madiwani kutimiza wajibu wao waliopewa dhamana na wananchi,lakini pia kwa upande mwingine ukawa ni mwiba kwa watendaji na wataalamu wa halmashauri hiyo kujiepusha na ubadhirifu wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Bi.Fatma Mwassa katika hotuba hiyo amewaonya watendaji watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo kuwa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

''Tunataka kuona halmashauri zilizotukuka kwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko katika mkoa wetu ambao kwasasa bado unaonekana kuwa nyuma sana kimaendeleo''kauli ya Fatma Mwassa katika kikao cha baraza hilo la madiwani.   



No comments: