Pages

KAPIPI TV

Friday, January 27, 2012

MAJI TATIZO TABORA.

                                                                                                                                       
 Tatizo la maji mjini Tabora na namna wanawake na wakazi wa mjini humo wanavyosota kutafuta maji ya kunywa




Baadhi ya kinamama wakipata huduma ya maji katika moja ya visima vilivyochimbwa  na mbunge wa jimbo la Tabora mjini aliyemaliza  muda wake Mh.Siraju Kaboyonga,kisima ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi mil.14.



 Kufa kufaana!.......Biashara ya maji pia imepamba moto,wake kwa waume.

Ni karibu siku nane leo hii,Maji yamekuwa ni tatizo linalowasumbua wakazi wa manispaa ya Tabora....

Katika zunguuka yangu maeneo mbalimbali ya mji huu wenye historia ya kupatikana kwa uhuru wa nchi ya Tanzania lakini cha ajabu kila kona ninayopita nashuhudia watu wanavyohangaikia maji na hususani wanawake.....

Nimejaribu kujiuliza hivi hili tatizo la maji litakuja kuwa ni historia kama wanavyodai baadhi ya wanasiasa?...

Lakini nakubaliana na mpango aliouanzisha Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Tabora mjini aliyemaliza muda wake Mh.Siraju Kaboyonga ambaye alijaribu kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo na kuamua kujenga visima sita katika kata mbalimbali hatua ambayo kwasasa  ndio imekuwa ni kimbilio la wakazi wa manispaa ya Tabora katika kupata huduma hiyo muhimu.

Alaaa kumbe tatizo hili sugu linaweza kupungua au kuondoka kabisa endapo kama tungekuwa na mwakilishi wa wananchi bungeni ambaye anakifikisha vema kilio chetu na wakati mwingine kulazimika hata kutumia mfuko wake kutusaidia!!!




 
   

No comments: