Pages

KAPIPI TV

Wednesday, January 25, 2012

''Mtoto ageuka kuwa muuguzi....azidisha dozi usiku Baba mahututi alazwa Kitete''"

BABA HOI KWA DAWA NA POMBE
''Mtoto ageuka kuwa muuguzi....azidisha dozi usiku"
 Mtoto Moody Hamisi (8)akionesha vidonge alivyompa baba yake Bw.Hamisi Tadeo wakati alipokuwa akihisi homa kabla na baada ya kunywa pombe za kienyeji katika kata ya Kiloleni manispaa ya Tabora.


 Moody akisubiri msaada kwa wasamalia wema,lakini kwa wakati huu alikuwa hajui la kufanya kwakuwa hapo nyumbani kwao alikuwa anaishi yeye na baba yake Bw.Hamisi(45). 
Wasamalia wema baadaye wakajitokeza na kumpeleka hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ambako kwasasa amelazwa akiwa hajitambui.

Ni huzuni kubwa niliyomkuta nayo mtoto Moody Hamisi mapema asubuhi!......
Pamoja na kubaini umri huu wa miaka minane aliyokuwa nayo Moody,lakini pia akikabiliwa na kadhia aliyoipata usiku kucha bila hata chembe ya kusinzia akifanya kazi ya uuguzi nyumbani kwao Kiloleni Tabora mjini.

Swali langu la kwanza kwa Moody ambaye kwa wakati huu alikuwa amezunguukwa na baadhi  ya  watu wachache wakiwa wanamtazama yeye pamoja na baba yake kana kwamba ni kioja,lilikuwa ni kutaka kujua kulikoni...

Mtoto Moody akionekana pia kwa asubuhi hii macho  yake yameelemewa na usingizi,alianza kwa kunieleza yafuatayo huku nikibaini kuwa mtoto huyu alikuwa anauwezo mzuri wa kuelezea jambo nikilinganisha na umri wake.

''Baba alirudi mchana kutoka kazini kwake huko station ya reli (Tabora)akiwa na rafiki yake ambaye alisema amemuokota baada ya kuzidiwa na ugojwa lakini mkononi baba alikuwa na vidonge,.....Aliniomba maji ya kunywa  ili ameze dawa hizo,nikafanya hivyo akameza dawa akalala ndani hadi jioni saa kumi akaamka...

Moody aliendelea kunieleza ''Jioni hiyo kama kawaida yake baba aliondoka kuelekea kwenye pombe hapo kilabuni"akionesha baa ya pombe za kienyeji iliyopo jirani na nyumbani kwao.

"Baadaye baba alirudi akiwa tayari amelewa lakini alikuwa anasema anaumwa sana ikabidi nimpe vidonge tena kwa mara nyingine baada ya muda akapata nafuu akaondoka tena pamoja na kuwa nilimkataza aling'ang'ania tu kuondoka"

Nilitaka kujua huko ambako baba yake alielekea,Moody hakusita akasema alirudi tena kilabuni,...''nilikuwa na wasiwasi nikashindwa kupata usingizi nikimsubiri hadi arudi,....akarudi usiku sana akawa analalamika tena kuwa anaumwa ikabidi nimpikie ugali na dagaa mboga ambayo ilikuwa imebaki mchana...akala nikampa na dawa  tena akameza akalala huko ndani chini kwenye godoro''.

Moody akiwa anaelezea huku machozi yakimtiririka akasema ''baadae kidogo tu baba  alianza kulalamika nikashindwa kulala,.....akaamka  alfajiri akatoka  nje,nilipoona hajarudi kwa muda mrefu nikaamua kumfuata huko nje lakini sikumuona,.....nikaendelea tena hadi barabarani nikaona kama kuna mtu ameanguka katika ya barabara,''

''Nilisogea  karibu kuangalia vizuri nikamuona  baba,..alikuwa anakoroma huku akigalagala,..nilipiga kelele huku nikiwa nalia wakati huu wa giza lakini hakuna mtu alikuja kunisaidi hadi ilipofika asubuhi hii''alieleza Moody

''Hawa watu ndio wamekuja hapa wamenisaidia kumtoa baba barabarani na kumuweka hapa chini''alieleza Moody huku akijibu swali kuhusu mama  yake kwa wakati huu alikuwa wapi?...''Mimi sina  mama,...Mama yangu alikwisha kufa.

Kwakweli ni hadithi ndefu na inatia uchungu sana,...ama  kwa hakika hujafa hujaumbika maelezo ya Moody na maisha anayoishi sidhani kama atafanikiwa hata kuendelea na masomo ingawa kwasasa  ndio kwanza yupo darasa  la kwanza katika shule ya msingi Jamhuri iliyopo kata ya Kiloleni Tabora  mjini.             



No comments: