Pages

KAPIPI TV

Friday, February 17, 2012

"POLISI KAENI PEMBENI TUNAITOA WENYEWE MAITI HII"-WANANCHI

"POLISI KAENI PEMBENI"Wakazi wa kata ya Kiloleni waliamua kuwasaidia Polisi kuopoa maiti iliyokuwa imezama katika kisima cha maji Bombamzinga Kiloleni manispaa ya Tabora.

 Wakazi wa Kiloleni pamoja na askari Polisi wakiwa wanaangalia maiti ya mtu mmoja aliyekuwa amezama katika kisima cha maji Bombamzinga Kiloleni wakishauriana kati ya askari Polisi na wananchi ni nani aingie ndani ya kisima kuitoa maiti hiyo.

MAITI NDANI YA KISIMA KABLA YA KUOPOLEWA.

 Ilikuwa ni hali ya mshangao kwa wakazi wa kata ya Kiloleni manispaa ya Tabora,wengine wakasikika wakilaumu na wengine kusikitishwa si kwa kifo cha mtu huyo pekee aliyepoteza maisha humo ndani ya kisima lakini zaidi ilikuwa ni ile hali ya ujio wa askari Polisi eneo la tukio.

Baada ya wananchi kusubiri kwa muda wa zaidi ya saa sita,askari Polisi walifika wakiwa na lengo la kutaka kuitoa maiti hiyo ili hatua ya uchunguzi ifanyike.

Lakini wananchi wengi waliofika hapo walishtushwa na ujio  huo ambapo askari hawakuwa hata na chembe ya kifaa kimoja ambacho kingewawezesha kuingia ndani ya kisima hicho na kibaya zaidi askari walikuwa ni wa kike na hata nguo walizokuwa wamevaa hazikuwa ni vazi rasmi la kikazi ambayo waliyokuwa wameifuata. 

Hali hii niliishuhudia kwa macho na pengine kuwasikia kabisa wananchi wakinung'unika na baadaye hatimaye waliamua wengine hata kuvua nguo na kubaki na nguo za ndani bila kujali umati mkubwa wake kwa waume uliokuwa umefurika eneo hilo kwa lengo la kuingia ndani ya kisima na kuanza shughuli ya kuitoa maiti hiyo.

Ukiachilia mbali na yote yaliyofanyika hapo naweza kusema dhana ya Polisi jamii imeanza kuingia miongoni mwa wananchi ingawa sina uhakika kama ni kweli wananchi waliokuwepo hapo wanaelewa hivyo au laa.

Hata hivyo kuhusu maiti ya mtu huyo inasemekana kuwa ni kijana mwenye umri wa miaka kati ya 32 hadi 35 anaitwa Maganga na hivi karibuni alikuwa ametoka jela na pia alionekana maeneo ya Kiloleni.

No comments: