Pages

KAPIPI TV

Wednesday, February 29, 2012

"FISI WA KISHIRIKINA AMNG'ATA MKONO MWENYEKITI WA KITONGOJI MBOLA"Baada ya kumpiga risasi alipambananaye kwa zaidi ya saa tisa.

 Mwenyekiti wa kitongoji cha Mbola C eneo la vijiji vya Milenia Mbola Bw.Julias Bundala Njota akiwa amelazwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete muda mfupi mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo kufuatia kujeruhiwa na Fisi anayedaiwa kuhusishwa na imani za kishirikina.


Kufuatia mapambano makali kati ya  mwenyekiti huyo wa kitongoji cha Mbola C Ilolangulu wilayani Uyui mkoani Tabora,Bw.Bundala  na  Fisi huyo anayedaiwa kuhusishwa na imani za kishirikina,Bw.Bundala alifanikiwa kumfyatulia risasi Fisi huyo iliyompata kwenye eneo la kiunoni lakini cha ajabu aliendelea kukimbia hatua chache na kusimama.

Akizungumza na mtandao huu katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ambako amelazwa kwa sasa kufuatia majeraha aliyoyapata baada ya kuumwa na Fisi huyo katika mkono wa kulia,Bw.Bundala alisema Fisi huyo alivamia nyumbani kwake majira ya usiku wa saa nne akihofia kuwa alikuwa amekuja kwa nia ya kutaka kula mifugo yake ambayo ni mbuzi ndipo alitoka nje ya nyumba na kuanza kumfukuza hata kufikia hatua ya kumfyatulia risasi ingawa haikuwa rahisi kwa Fisi huyo kuondoka kwa haraka eneo hilo.

Alisema mapambano na Fisi huyo yalidumu kwa muda mrefu licha ya kuwa Fisi huyo tayari alikuwa amejeruhiwa na risasi  hadi hapo Bw.Bundala akiwa na kijana wake waliamua kuingia kulala na Fisi huyo kuingia kwenye kichaka cha jirani na nyumbani kwake huku akiendelea kutoa sauti kana kwamba anafoka hadi ilipofika asubuhi ya siku ya pili.

Bw.Bundala mapema asubuhi hiyo aliamka na kuanza tena juhudi za kupambana na Fisi huyo akiwa sasa na vijana wengine wawili wakitumia silaha za marungu na fimbo.

Baada ya kumfuatilia Fisi huyo kwenye kichaka alikojificha walimkuta na kuanza kumshambulia tena lakini safari hii sasa Fisi aliamua kujibu mapigo kwa kumvaa Bw.Bundala peke yake na kuanza kumng'ata mkono wa kulia na hata kufikia hatua ya kuangushana chini.

Wakati tukio hilo likiendelea vijana hawa wawili waliokuwa na Bw.Bundala pamoja na kumsaidia kwa kumpiga kwa fimbo Fisi huyo lakini haikuwa rahisi hadi Bw.Bundala alipopata nafasi ya kukimbia.

Fisi huyo ambaye sasa kwa muda huo alionekana kuwa na king'ang'anizi na kuwashangaza watu wa kitongoji hicho waliokuwa wamefika baadaye,walichukua jukumu la kuanza  kupambana naye hadi kufikia hatua ya kumuua kwa risasi baada ya kukimbilia kwenye chumba cha kukaushia tumbaku(BURN).         

No comments: