Pages

KAPIPI TV

Wednesday, October 26, 2011

PANASONIC YATOA MSAADA MIL.300


Mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora Bi.Fatma Mwassa akiwa  na  mwakilishi   wa  balozi wa Japan nchini Tanzania Bw.Shuichilo Kawaguchi,mkurugenzi wa mawasiliano na ushirikiano Bw.Hidetoshi Osawa,viongozi  wa mradi  wa milenia Mbola,wakuu  wa wilaya  za uyui na Tabora manispaa wakiwa  katika hafla fupi ya  kupokea msaada  wa kontena.
 Mkuu  wa  mkoa  akiwa na wageni kutoka kampuni ya Panasonic na Serikali  ya Japan wakiangalia maonesho  ya  kazi  za mikono,utaalamu wa usindikaji matunda pori katika vijiji vya Milenia Mbola.
  Wakazi wa vijiji vya Milenia Mbola wakicheza ngoma kukaribisha wageni ikiwa ni  mambo yaliyojiri wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada huo.
Kutoka kushoto:Bw.Shuichilo Kawaguchi,mwakilishi  wa balozi wa  Japan,Bw.Hidetoshi Osawa,mkurugenzi ushirikiano na mawasiliano wa Panasonic Japan,Bi.Fatma Mwassa,mkuu  wa  mkoa wa Tabora.
  Bw.Osawa akitoa maelezo kwa kutumia televisheni kazi zinazofanywa na kampuni  ya Panasonic.
 Meneja mkuu mwasiliano na ushirikiano wa Panasonic,Michiko Ogawa akipiga wimbo wa Taifa la Tanzania kwa kutumia kinanda hicho kinachojulikana  kama KALIMBA na PIANICA.
Mkuu wa mkoa akiwapokea wageni muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege wa Tabora wakitokea Dar-es-salaam kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea msaada huo.



MRADI  WA  VIJIJI  VYA  MILENIA  MBOLA  WAPATA  MSAADA  WENYE  THAMANI  ZAIDI   YA  SHILINGI  MIL.300  TABORA.


Na  Juma  Kapipi.
Uyui  Tabora.

Kampuni  ya  maarufu  ulimwenguni  ya  Panasonic  imetoa  msaada  wa  kontena  lenye  mifumo  ya  kielektroniki  kusaidia  mradi  wa  vijiji  vya  Milenia  Mbola  ikiwa  ni  hatua  ya  kuwawezesha  wakazi  waishio  vijiji  hivyo  kutumia  nishati  mbadala  ya  umeme  wa  jua.

Msaada  huo  ambao  umekabidhiwa  kwa  mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora  Bi.Fatuma  Abubakar  Mwasa  katika  hafla  fupi  iliyofanyika  kijiji  cha  Mbola  Shuleni  na  kushuhudiwa  na  wakazi  wa  vijiji  vya  Milenia  Mbola pamoja  na  baadhi  ya  maafisa  kutoka  kampuni  ya  Panasonic  ya  nchini  Japan.

Akizungumza  wakati  wa  makabidhiano   hayo  mkurugenzi   ushirikiano  na  mawasiliano  wa  kampuni  ya  Panasonic  Bw.Hidetoshi  Osawa  alisema  dhamira  ya  kampuni  yake  kutoa  msaada  huo  wenye  thamani  ya  zaidi  ya  shilingi  mil.300  kwa  wakazi  wa  vijiji  vya  Milenia  Mbola  ni muendelezo  wa  msaada  ulioanza  kutolewa  na  kampuni  hiyo  tangu  mnamo  April  mwaka  jana.

Alisema  tangu  mwaka  jana  kampuni  ya  Panasonic  ilianza  kufanya  utafiti  kushughulikia  namna  ya  kupata  nishati  mbadala  ya  umeme  itakayokuwa  rafiki  wa  mazingira  katika  maeneo  ya  vijiji  vya  millennia  ambako  nishati  ya  umeme  inatajwa  ni   tatizo kubwa  na  hivyo  kupata  ufumbuzi  wa  umeme  wa  jua.

Bw.Osawa  akifafanua  zaidi  katika  hafla  hiyo  fupi  iliyoambatana  na  uzinduzi  wa  shughuli  zitakazokuwa  zikifanyika  baada  ya  kupatikana  kwa  kontena  hilo  ambalo  limepangiwa  kutumika  kutoa  mafunzo  ya  elimu  ya  komputa  kwa  wanafunzi  wa  shule  za  msingi  na  sekondari,kutoa  elimu  ya  biashara  kwa  wananchi  pamoja  na  huduma  ya  kupata  habari  kupitia  televisheni  iliyoko  kwenye  kontena  hilo.

Aidha  Bw.Osawa  ambaye  katika  ziara  yake  ya  siku  moja  kwenye  vijiji  vya  millennia  Mbola  ambapo  alifuatana  na  mwakilishi  wa  balozi  wa  Japan  nchini  Bw.Shuichilo  Kawaguchi,alisema  kampuni  ya  Panasonic  ambayo  imeanza  kufanyakazi  nchini  kwa  zaidi  ya  miaka  43 iliyopita  imepata  ushirikiano  mkubwa  kutoka  serikali  ya  Tanzania  na  hivyo  haina  budi  kuunga  mkono  juhudi  mbalimbali  za  kuleta  maendeleo  nchini.

Kwa  upande  wake  mwakilishi  huyo  wa  balozi  wa  Japan  nchini  Bw.Kawaguchi  alisema  serikali  ya  Japani  tangu  mwaka  2006 tayari  imekwisha  changia  zaidi  ya  dola  mil. 20  za  kimarekani  kwa  mradi  wa  vijiji  vya  millennia  Mbola  lengo  likiwa  ni  kusaidia  harakati  za  kupambana  na  umasikini  nchini.

Akitoa  shukrani  kwa  uongozi  wa  kampuni  ya  Panasonic  na  mwakilishi  wa  serikali  ya  Japan  kwa  niaba  ya  wananchi  mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora  Bi.Fatma  Mwassa  alisema  msaada  huo  pamoja  na  mambo  mengine  pia  utasaidia  katika  sekta  ya  afya  kutokana  na  baadhi  ya  vifaa  vilivyomo  ndani  ya  kontena  hilo  kuwa  na  mahusiano  na  sekta  hiyo  muhimu.

‘’kutokana  na  Jokofu  hilo  lililopo  ndani  ya  kontena  litatusadia  hata  kuhifadhia  dawa  kama  vile  zile  zinazotumika  kwa  chanjo  mbalimbali  za  watoto  kwa  msaada  huu  tunaupokea  kwa  heshima  kubwa’’alisema  Bi  Fatma  Mwassa  huku  akitumia  fursa  hiyo  kuwataka  wananchi  kuwa  mabalozi  wazuri  katika  kulilinda  kontena  hilo.

Katika  hatua  hiyohiyo  mratibu  wa mradi  wa  vijiji  vya  Milenia  Mbola  Dr.Gerson  Nyadzi  na  mkurugenzi  wa  mradi  wa  vijiji  vya  millennia  Tanzania  Dr.George  Sempeho  wamesema  serikali  ya  Japan  imekuwa  na  mchango  mkubwa  tangu  utekelezaji  wa  mradi  huo  kwa  awamu  ya  kwanza  katika  kufikia  malengo  manane  ya  millennia  ambayo  hadi  sasa  mafanikio  makubwa  yamekwisha  patikana   kwa  sekta  za  elimu,afya,kilimo  na  miundo mbinu  ya  maji  na  barabara.



No comments: