Pages

KAPIPI TV

Wednesday, October 19, 2011

MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAM TANZANIA THRDs

Wanachama  wa  mtandao wa  THRDs na  EHAHRDP kutoka  Uganda,Kenya  na  Tanzania  wakati  wa  mkutano  uliofanyika  Ubungo  Plaza jijini  Dar-es-salaam.


 Wajumbe  wa mkutano  wa THRDs wakiwa katika mkutano  huo wakijadili namna  ya  kuimarisha mtandao huo.

 Mratibu  wa  mtandao  wa  THRDs Bw.Onesmo  Ole Ngulumwa akizungumza katika mkutano  na  wanachama  wa  THRDs na EHAHRDP katika  ukumbi  wa  Ubungo Plaza jijini  Dar-es-Salaam.
Afisa utetezi  EHAHRDP  Rachel Nicholaus akitoa maelezo kuhusu shughuli za mtandao  wa EHAHRDP  unaofanyakazi barani  Afrika kwa  kuwakinga watetezi  wa  haki za binadamu.   

MTANDAO  WA  WATETEZI  WA  HAKI  ZA  BINADAMU THRDs.
Na JUMA  KAPIPI
DAR-ES-SALAAM.

Mkutano  wa  jumuiko  la  watetezi  wa  haki  za  binadamu  nchini Tanzania  Human Rights Deffender  umefanyika   jijini  Dar-es-salaam  na  kupitia  masuala  kadhaa  ikiwemo  kusaini  katiba  na  kuhakiki  kazi  za  mtandao  huo  ambazo  kimsingi  zinalenga  kuwakinga  watetezi  dhidi  madhara  na  vitisho  wanavyovipata.

Mratibu  wa mtandao  huo  wa  THRD Bw.Onesmo  Ole  Ngulumwa  alisema  kuanzishwa  kwa  mtandao  huo  wa  kuwakinga  watetezi  wa  haki  za  binadamu  ni  hatua  madhubuti  itakayosaidia  kuimarika kwa  kazi  za  utetezi  wa  haki  za  binadamu  nchini.

Pamoja  na  kubainisha  matatizo  kadhaa  hasa  yanayowakumba  watetezi  wa  haki  za  binadamu  nchini  wakiwemo  baadhi  ya waandishi  wa  habari  ambao  wamejitoa  kupigania  haki  za  wanyonge  kwa  kuibua  maovu  mbalimbali  lakini  alieleeza  kuwa  kumekuwa  na changamoto  kubwa  katika  kuwakinga  watetezi  hao  hali  iliyotokana  na  kutokuwepo  kwa  mtandao  kama  huo  wa  THRDs hapa  nchini  ambao  kimsingi  umeundwa  kwa  ajili  ya  kukabiliana  na  hali  hiyo.

“Kwakweli  tumeshuhudia  watetezi  wa  haki  za  binadamu  wamekuwa  wakipata  vitisho  vya  aina  mbalimbali  ikiwa  ni  pamoja  na  kubambikizwa  kesi  na  hata  wengine  kufanyiwa  unyama ,kwa mfano  kwa  hapa  Tanzania  waandishi  wa  gazeti  la  Mwanahalisi  Said  Kubenea  na  Ndimala Tegambwage “alisema  mratibu  wa  THRDs Onesmo  Ngulumwa  wakati  akizungumza  na  waandishi  wa  habari  jijini  Dar-es-salaam.

Kwa upande  wake  kaimu  mkurugenzi  wa  kituo  cha  sheria  na  haki  za  binadamu  LHRC Bi,Imelda  Lulu  Urio  alisema  pamoja  na  kuwepo  kwa  mtandao  huo  wa  THRDs lakini  bado  kuna  haja  ya  kuwepo  kwa  sera  zitakazowakinga  na  kukubali  kazi  zinazofanywa  na  watetezi  wa  hakia za  binadamu  nchini.

Mkurugenzi  huyo Bi.Lulu  aliongeza  kwa  kusema  kuwa  bado  hata  jamii  na  baadhi  ya  viongozi  hawajatambua  umuhimu  wa  kazi  za  watetezi  wa  haki  za  binadamu  na  hata  baadhi  yao  wamewaona  kana  kwamba  ni  wachochezi .

‘’Tumeshuhudia  baadhi  ya  viongozi  wamekuwa  wakiwapatia  vitisho  watetezi  wa haki  za  binadamu na  hata  kuwaambia  kuwa  wanatumiwa  na  wanasiasa  kuchochea  na  kuwa  chanzo  cha  vurugu  nchini”alisema  Bi,Imelda  Lulu  Urio.

 Aidha  katika  mkutano  huo  wa  THRD ambao  pia  umejumuisha  wataalam  kutoka  mradi  wa  East  and  Horn of Africa  Human  Rights Defenders   EHAHRDP ambao  kwasasa  unafanya  kazi  katika  nchi  zaidi  ya  12,wataalam  hao  walipata  fursa  ya  kueleza  uzoefu  wao  katika  kuendesha  shughuli  za  utetezi  wa  haki  za  binadam na  huku  wakitamba  kufanikiwa  zaidi  katika  nyanja  mbalimbali.

Akiwasilisha  tamko  la  jumuiya  ya  ulaya  EU katika  mkutano  huo,mmoja  kati  ya  maafisa  wa  jumuiya  hiyo Bi.Leila  El Krekshi  alisema  jumuiya  ya  ulaya  inatambua  mchango  mkubwa  unaofanywa  na  asasi  zinazopigania  haki  za  binadamu  ulimwenguni  kote na  huku  akielezea  kuwa  jumuiya  hiyo  itaendelea  kufadhili  kwa  kadri  ya  mahitaji  ya  asasi hizo.

Mtandao  wa  THRDs ni  asasi  ya  kwanza  nchini  isiyo ya  kiserikali  ambayo  imeundwa  kwa  ajili  ya  kuwakinga  watetezi  wa  haki  za  binadamu  ambayo  pia  ni  inawakilisha Tanzania  kuwa mwanachama  wa  EHAHRDP ndani  ya  Afrika.


   

No comments: