Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akiwa na mwakilishi wa balozi wa Japan nchini Tanzania Bw.Shuichilo Kawaguchi,mkurugenzi wa mawasiliano na ushirikiano Bw.Hidetoshi Osawa,viongozi wa mradi wa milenia Mbola,wakuu wa wilaya za uyui na Tabora manispaa wakiwa katika hafla fupi ya kupokea msaada wa kontena.
Kutoka kushoto:Bw.Shuichilo Kawaguchi,mwakilishi wa balozi wa Japan,Bw.Hidetoshi Osawa,mkurugenzi ushirikiano na mawasiliano wa Panasonic Japan,Bi.Fatma Mwassa,mkuu wa mkoa wa Tabora.
Bw.Osawa akitoa maelezo kwa kutumia televisheni kazi zinazofanywa na kampuni ya Panasonic.
Meneja mkuu mwasiliano na ushirikiano wa Panasonic,Michiko Ogawa akipiga wimbo wa Taifa la Tanzania kwa kutumia kinanda hicho kinachojulikana kama KALIMBA na PIANICA.
Mkuu wa mkoa akiwapokea wageni muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege wa Tabora wakitokea Dar-es-salaam kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea msaada huo.
Mkuu wa mkoa akiwa na wageni kutoka kampuni ya Panasonic na Serikali ya Japan wakiangalia maonesho ya kazi za mikono,utaalamu wa usindikaji matunda pori katika vijiji vya Milenia Mbola.
Wakazi wa vijiji vya Milenia Mbola wakicheza ngoma kukaribisha wageni ikiwa ni mambo yaliyojiri wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada huo.Kutoka kushoto:Bw.Shuichilo Kawaguchi,mwakilishi wa balozi wa Japan,Bw.Hidetoshi Osawa,mkurugenzi ushirikiano na mawasiliano wa Panasonic Japan,Bi.Fatma Mwassa,mkuu wa mkoa wa Tabora.
Bw.Osawa akitoa maelezo kwa kutumia televisheni kazi zinazofanywa na kampuni ya Panasonic.
Meneja mkuu mwasiliano na ushirikiano wa Panasonic,Michiko Ogawa akipiga wimbo wa Taifa la Tanzania kwa kutumia kinanda hicho kinachojulikana kama KALIMBA na PIANICA.
Mkuu wa mkoa akiwapokea wageni muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege wa Tabora wakitokea Dar-es-salaam kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea msaada huo.
MRADI WA
VIJIJI VYA MILENIA
MBOLA WAPATA MSAADA
WENYE THAMANI ZAIDI
YA SHILINGI MIL.300
TABORA.
Na Juma
Kapipi.
Uyui Tabora.
Kampuni ya
maarufu ulimwenguni ya
Panasonic imetoa msaada
wa kontena lenye
mifumo ya kielektroniki
kusaidia mradi wa
vijiji vya Milenia
Mbola ikiwa ni
hatua ya kuwawezesha
wakazi waishio vijiji
hivyo kutumia nishati
mbadala ya umeme
wa jua.
Msaada huo
ambao umekabidhiwa kwa
mkuu wa mkoa
wa Tabora Bi.Fatuma
Abubakar Mwasa katika
hafla fupi iliyofanyika
kijiji cha Mbola
Shuleni na kushuhudiwa
na wakazi wa
vijiji vya Milenia
Mbola pamoja na baadhi
ya maafisa kutoka
kampuni ya Panasonic
ya nchini Japan.
Akizungumza wakati
wa makabidhiano hayo
mkurugenzi ushirikiano na
mawasiliano wa kampuni
ya Panasonic Bw.Hidetoshi
Osawa alisema dhamira
ya kampuni yake
kutoa msaada huo
wenye thamani ya
zaidi ya shilingi
mil.300 kwa wakazi
wa vijiji vya
Milenia Mbola ni muendelezo
wa msaada ulioanza
kutolewa na kampuni
hiyo tangu mnamo
April mwaka jana.
Alisema tangu
mwaka jana kampuni
ya Panasonic ilianza
kufanya utafiti kushughulikia
namna ya kupata
nishati mbadala ya
umeme itakayokuwa rafiki
wa mazingira katika
maeneo ya vijiji
vya millennia ambako
nishati ya umeme
inatajwa ni tatizo kubwa
na hivyo kupata
ufumbuzi wa umeme
wa jua.
Bw.Osawa akifafanua
zaidi katika hafla
hiyo fupi iliyoambatana
na uzinduzi wa shughuli zitakazokuwa
zikifanyika baada ya
kupatikana kwa kontena
hilo ambalo limepangiwa
kutumika kutoa mafunzo
ya elimu ya
komputa kwa wanafunzi
wa shule za
msingi na sekondari,kutoa elimu
ya biashara kwa
wananchi pamoja na huduma ya
kupata habari kupitia
televisheni iliyoko kwenye
kontena hilo.
Aidha Bw.Osawa
ambaye katika ziara
yake ya siku
moja kwenye vijiji
vya millennia Mbola
ambapo alifuatana na
mwakilishi wa balozi
wa Japan nchini
Bw.Shuichilo
Kawaguchi,alisema kampuni ya
Panasonic ambayo imeanza
kufanyakazi nchini kwa
zaidi ya miaka
43 iliyopita imepata ushirikiano
mkubwa kutoka serikali
ya Tanzania na
hivyo haina budi
kuunga mkono juhudi
mbalimbali za kuleta
maendeleo nchini.
Kwa upande
wake mwakilishi huyo
wa balozi wa
Japan nchini Bw.Kawaguchi
alisema serikali ya
Japani tangu mwaka 2006
tayari imekwisha changia
zaidi ya dola
mil. 20 za kimarekani
kwa mradi wa
vijiji vya millennia
Mbola lengo likiwa
ni kusaidia harakati
za kupambana na
umasikini nchini.
Akitoa shukrani
kwa uongozi wa
kampuni ya Panasonic
na mwakilishi wa
serikali ya Japan
kwa niaba ya
wananchi mkuu wa
mkoa wa Tabora
Bi.Fatma Mwassa alisema
msaada huo pamoja
na mambo mengine
pia utasaidia katika
sekta ya afya
kutokana na baadhi
ya vifaa vilivyomo
ndani ya kontena
hilo kuwa na
mahusiano na sekta
hiyo muhimu.
‘’kutokana na
Jokofu hilo lililopo
ndani ya kontena
litatusadia hata kuhifadhia
dawa kama vile
zile zinazotumika kwa
chanjo mbalimbali za
watoto kwa msaada
huu tunaupokea kwa
heshima kubwa’’alisema Bi
Fatma Mwassa huku
akitumia fursa hiyo
kuwataka wananchi kuwa
mabalozi wazuri katika
kulilinda kontena hilo.
Katika hatua
hiyohiyo mratibu wa mradi
wa vijiji vya
Milenia Mbola Dr.Gerson
Nyadzi na mkurugenzi
wa mradi wa
vijiji vya millennia
Tanzania Dr.George Sempeho
wamesema serikali ya
Japan imekuwa na
mchango mkubwa tangu
utekelezaji wa mradi
huo kwa awamu
ya kwanza katika
kufikia malengo manane
ya millennia ambayo
hadi sasa mafanikio
makubwa yamekwisha patikana
kwa sekta za
elimu,afya,kilimo na miundo mbinu
ya maji na
barabara.