Pages

KAPIPI TV

Monday, February 8, 2016

WATOTO 53,581 WAANDIKISHWA ELIMU YA AWALI TABORA

Na Allan Ntana, Tabora 

 MKOA wa Tabora umefanikiwa kuandikisha jumla ya watoto 53,581 wa kuanza elimu ya awali katika mwaka wa masomo 2016 . 

 Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia elimu mkoani Tabora Juma Mhina ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mkoa huo katika kikao cha wadau wa elimu kilichoketi hivi karibuni mjini hapa kikishirikisha maofisa kutoka halmashauri zote 7 za mkoa huo. 

 Alisema idadi hiyo ni ya watoto wote walioandikishwa katika halmashauri zote za mkoa huo ambapo idadi halisi ya watoto waliotarajiwa kuandikishwa ni 74,773 wavulana wakiwa 37,581 na wasichana 37,192. 

 Katika makisio hayo alisema wavulana walioandikishwa ni 21,664 sawa na asilimia 57.6 na wasichana ni 21,917 sawa na asilimia 58.9 ambapo jumla ya watoto wote walioandikishwa katika wilaya zote ni 53,581 sawa na asilimia 71.6. 

 Alifafanua kuwa halmashauri ya Manispaa ya Tabora imefanikiwa kuvuka lengo la makisio yake ambapo watoto waliotarajiwa kuandikishwa ni 4881 lakini walioandikishwa ni 5099 sawa na asilimia 104.5. 

 Mbali na Manispaa, alitaja takwimu za makisio ya kila halmashauri na idadi halisi ya watoto walioandikishwa ikiwa kwenye mabano kama ifuatavyo Igunga 17,844 (11,675), Nzega 16,643 (7,586), Urambo 8,433 (4,517), Sikonge 6,446 (2,227), Uyui 8,206 (4,801), Kaliua 9,944 (5,758) na Nzega Mji 2,376 (1,916). 

 Akizungumzia zoezi la uandikishwaji watoto wa kuanza darasa la kwanza Mhina alisema Mkoa huo umefanikiwa kuandikisha jumla ya watoto 64,642 sawa na asilimia 70.6 wakati matarajio ilikuwa kuandikisha watoto 91,506. 

 Aliipongeza halmashauri ya Manispaa Tabora kwa kufanikiwa kuvuka lengo la uandikishaji ambapo iliandikisha watoto 7,644 sawa na asilimia 110 wakati matarajio yalikuwa kuandikisha watoto 6,924. 

Alitaja takwimu za watoto walioandikishwa darasa la kwanza kwa kila halmashauri idadi iliyotarajiwa ikiwa kwenye mabano kama ifuatavyo Sikonge 2,569 (5,288), Kaliua 10,522 (16,042), Uyui 10,217 (16,571), Urambo 7,301 (8,844), Manispaa 7,644 (6,924), Igunga 11,675 (17,844), Nzega 12,678 (16,898) na Nzega Mji 2,036 (2,111).

HALMASHAURI KALIUA YASHINDA KESI DHIDI YA MKANDARASI

Na Allan Ntana, Kaliua 
 MAHAKAMA ya wilaya ya Urambo Mkoani Tabora imetupilia mbali shauri lililofunguliwa mahakamani hapo na Mkandarasi (Kampuni ya SARAM ya jijini Dar es salaam) ikipinga kusimamishwa na halmashauri ya wilaya ya Kaliua kuendelea na mkataba wake wa ujenzi wa miradi 4 ya halmashauri hiyo. 

 Akitoa taarifa kwa madiwani katika kikao kilichoketi jana katika ukumbi wa Milenia mjini Kaliua Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Athuman Kihamia alisema mahakama imesikiliza shauri hilo na kujiridhisha pasipo shaka kuwa Mkandarasi huyo alikiuka makubaliano ya mkataba wake na hivyo kutupilia mbali pingamizi lake. 

 Alisema baada ya Mkandarasi huyo kusimamishwa na halmashauri kuendelea na mkataba wake katika miradi 4 alifungua shauri katika mahakama hiyo akipinga maamuzi hayo ikiwemo kuweka zuio kwa halmashauri hiyo kutofanya shughuli yoyote ile katika miradi iliyokuwa inatekelezwa kwa mujibu wa mkataba. 

 ‘Waheshimiwa madiwani napenda kuwataarifu kuwa Januari 20 mwaka huu mahakama imetengua pingamizi lililowekwa na Mkandarasi SARAM na ilituagiza Mkurugenzi (mwajiri) na Mkandarasi (mwajiriwa) tukae pamoja na kufanya tathmini ili kujiridhisha kama ana madai yoyote kwetu na tutoe taarifa ndani ya siku 14’, alisema Kihamia. 

 Alifafanua kuwa licha ya Mahakama kutoa maelekezo hayo ya kukutana pande zote mbili, Mkandarasi huyo hajaonekana hadi sasa na siku 14 zimeshaisha hivyo akabainisha kuwa watakachofanya sasa ni kufanya tathmini wao wenyewe na kupeleka taarifa mahakamani ili mchakato wa kutafuta mkandarasi mwingine uanze mara moja. ‘Ukweli mahakama imetenda haki kwani kuzuia miradi ya maendeleo isiendelee kisa tu mkandarasi katimuliwa ni kuchelewesha maendeleo ya wananchi, nimepokea uamuzi wa mahakama kwa furaha kubwa’, aliongeza. 

 Miradi iliyokuwa inatekelezwa na mkandarasi huyo ni ujenzi wa ofisi ya 
Mkurugenzi wa halmashauri, jengo la wagonjwa wan je (OPD), nyumba 4 za watumishi na jengo la maonyesho ya nane nane eneo la Ipuli katika manispaa ya Tabora. Akizungumzia hukumu hiyo Mwanasheria wa Mkoa wa Tabora Richard Lugomela aliyesimamia kesi hiyo alisema mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa pingamizi la mkandarasi huyo halina tija kwa maendeleo ya halmashauri kwani alishindwa kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika mkataba wake wa awali. ‘Mkandarasi yeyote anayepewa mkataba wa kutekeleza mradi fulani anapaswa kuwajibika ipasavyo kama mkataba unavyotaka, katika miradi ya maendeleo tunahitaji mkandarasi mwenye uwezo na kasi na amalize kwa wakati si vinginevyo’, alibainisha.

KAMPUNI YA MAWASILIANO YA TIGO YAHAMASISHA WATANZANIA KUJALI AFYA ZAO

Katika ni Robert Paul ambae ni Meneja Masoko ya Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO Kanda ya Ziwa, akizungumza katika zoezi la Utoaji bure wa huduma mbalimbali za Afya ikiwemo upimaji wa Magonjwa ya Moyo, Utoaji wa Matibabu kwenye majeraha(Vidonda) pamoja na Uchangiaji damu lililofanyika juzi jumamosi February 06,2016 katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

"Tigo tumeamua kushiriki zoezi hili ili kuonyesha mfano katika jamii namna tunavyojumuika na Watanzania katika shughuli za Kijamii, hivyo kupitia fursa hii ningependa kuwaasa Watanzania kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ikiwemo kupima shinikizo la damu, saratani lakini kubwa zaidi kuwa na moyo wa kujitolea kuchangia damu ili kuwasaidia wenye uhitaji wa damu. Alisema Paul.

Nae Cassim Aziz (Kushoto) ambae ni Meneja Masoko wa Tigo Mkoani Mwanza, alizishauri taasisi pamoja na makampuni mbalimbali nchini kuwa na desturi ya kushiriki katika shughuli za kijamii hususani kuhamasisha watanzania kupima afya zao mara kwa mara ili kuepuka athari za kiafya zinazoweza kuzuilika.

Zoezi hilo liliandaliwa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Udaktari Hubert Kairuki cha Jijini Dar es salaam wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kuenzi Miaka 17 tangu mwasisi wa chuo hicho afariki dunia (Februa 06,1999) ikiwa ni miaka miwili baada ya kuanzisha chuo hicho.
Dkt.Emmanuel Chacha ambae ni Mkurugenzi wa Hospital ya CJ Jijini Mwanza akizungumza katika shughuli hiyo ya upimaji wa afya bure ambapo Hospital ya CF ilikuwa miongoni mwa wadau waliofanikisha shughulio hiyo.
Mwenye Kinasa Sauti ni Dkt.Francis Tegete ambae ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Profesa Paschalis Rugarabamu ambae ni Mlezi wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Picha ya Pamoja ya wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Wadau waliofanikisha zoezi la Upimaji afya bure wakiwa katika Picha ya Pamoja ya wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Kampuni ya Mawasiliano Tigo ikiendelea na Utoaji wa Huduma zake za Simu kwa wateja
Mmoja wa Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo akipatiwa huduma na wahudumu wa Kampuni hiyo.
Wanafunzi na Wananchi mbalimbali walijitokeza kupima bure afya zao
Zoezi la Upimaji na utoaji huduma za afya bure likiwa linaendelea
Bank ya Damu salama Kanda ya Ziwa ikiendelea na zoezi la ukusanyaji damu kutoka kwa wananchi waliokuwa wanajitolea damu.
Katikati ni Alfredy Chibuae ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Taaisi ya Tanzania Rural Health Movement akifuatilia utoaji wa huduma unavyoendelea. Taasisi hiyo inashughulika na utoaji wa huduma za afya bure kwa watu wasiojiweza hususani watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (mitaani) pamoja na utoaji wa huduma za dharura ikiwemo wale wanaopata ajali. Taasisi hiyo inapatikana Bugando Jijini Mwanza.

TANZANIA KUENDELEZA UTAFITI WA BIOTEKNOLOJIA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Uvuvi, Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa Wema wa siku tatu wa watafiti kutoka nchi za Afrika wa kutathimini utendaji kazi wa Wema kwa mwaka uliopitaKushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Uharishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Dk. Denis Kyetere na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda.
Mkurugenzi wa Ushirikiano Mradi wa Wema, Kampuni ya Monsanto, Mark Edge (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Mkuu wa Programu, Taasisi ya Bill and Melinda Gates Dk.Lawrence Kent (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mradi wa Wema, Shirika la Kimataifa la Uhaurishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Sylvester Oikeh akizungumza katika mkutano huo.
Mtafiti wa Mahindi, Shirika la Kimataifa la utafiti wa ngano na mahindi (CIMMYT), Yoseph Beyene akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mfumo na Uzalishaji wa Mbegu (AATF), Gospel Omanya akitoa mada katika mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Hapa ni kazi tu za utafiti.
Watafiti na washiriki wakiwa Busy na nyaraka.
Watafiti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza utafiti wa bioteknojia pamoja na kutekeleza mradi wa WEMA kwa hatua. Mradi huo unajishughulisha na utafiti wa mbegu za mahindi nchini.


Turuka ameyasema hayo kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi  yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa WEMA, leo asubuhi jijini Dar es salaam. Mkutano huo wasiku tatu umewaleta pamoja watafiti kutoka nchi za Afrika, kutathimini utendaji kazi wa mradi kwa mwaka uliopita.


Alisema awamu ya utafiti wa njia ya kawaida wa mahindi imekamilika na aina  sita mpya za mahindi zimepatikana na kuwa hivi sasa kwa kufuata kanuni za usalama wa viumbe, itaanza utafiti wa mahindi kwa njia ya  uhandisi jeni.


"Sera na kanuni zipo, tutafanya utafiti wa GMO na matokeo ya utafiti yatatoa mwongozo wa dira yetu ya kilimo" alisema Dk. Turuka.


Katika hatua nyingine Dk. Turuka amewataka watafiti wa mbegu za mahindi nchini kuhakikisha mbegu bora walizozifanyia utafiti zinawafikia wakulima kwa wakati.


"Serikali inafurahishwa na mradi huu wa WEMA kwani unamsaidia mkulima kupata mbegu bora ambazo zinahimili ukame na haziwezi kushambuliwa na magonjwa" alisema Dk.Turuka.


Alisema kwa kutumia mbegu bora zilizotokana na utafiti huo mkulima anaweza kupata tani 8.5 za mahindi kwa ekari moja na kusisitiza kuwa mbegu hizo zisipo mfikia mkulima kwa wakati mradi huo utakuwa haujaisaidia serikali.


Dk. Turuka alisema serikali inaangalia kwa karibu sheria na kanuni za kuwapa uwanja mpana watafiti bila ya kuharibu mazingira na kuhatarisha maisha ya wananchi wakati wa kufanya tafiti zao.


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda alisema tafiti hizo za mbegu zinatoa nafasi kwa wakulima kupata mbegu bora na kuwa utafiti huo uliofanywa kwa kushirikiana na watafiti kutoka nchi mbalimbali umeonesha mafanikio makubwa.


Mratibu wa mradi huo wa WEMA, Dk.Alois Kullaya alisema mradi huo ulianza mwaka 2008 na kuwa wamekuwa wakitumia mbinu za kisasa kupata mbegu bora.


Alisema Tanzania na nchi nyingine tayari zimepasisha mbegu 59 ambapo kwa hapa nchini zipo mbegu sita tu ambazo zinazalishwa.



Aliongeza kuwa kwa nchi ya Afrika Kusini wao tayari wameidhinisha matumizi ya mbegu za GMO.


Saturday, January 30, 2016

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TANZANIA STANDARD NEWSPAPERS LIMITED CHAFANYIKA LEO JIJINI DAR

tsn4
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, Gabriel Nderumaki akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi jijini Dar es Salaam jana kilichokuwa kinajadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016.Kulia ni Katibu wa baraza hilo, Shafii Mpenda.
tsn1
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
tsn2
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
tsn3
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.

WATANZANIA WENGI WANAKOSA FURSA ZA KIMAENDELEO KUTOKANA NA KUTOJUA LUGHA

Charles Mombeki (Kulia) ambae ni Mkurugenzi wa International Language Training Centre akizungumza na George Binagi kuhusiana na Umhimu wa Watanzania kujifunza lugha za Kimataifa hususani Kiingereza kwa ajili ya kuendana na muingiliano wa Kimataifa uliopo katika shughuli mbalimbali ikiwemo biashara.
"Watanzania wengi wanakosa fursa mbalimbali zilizopo. Wengine wanakosa fursa za kibiashara pamoja na kazi kutoka katika Mashirika na Makampuni mbalimbali duniani kutokana na kushindwa kufahamu lugha za Kimataifa hususani kiingereza, Kijerumani, Kifarasa, Kichina na hata lugha nyingine. Hivyo niwasihi waamue kujifunza lugha, kwa kuwa lugha inafungua milango ya mafanikio maishani". Anasema Mombeki.

Anasema, Watanzania wawaandae watoto wao katika lugha ya Kiingereza katika kupata elimu, akiunga mkono shule za watu ama Mashirika binafsi kutumia lugha ya Kiingereza kufundishia, tofauti na ilivyo kwa shule za Serikali kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia katika shule za msingi akitanabaisha kwamba bado kiswahili hakijawa na nafasi kubwa kutumika kimataifa kama ilivyo kiingereza ambayo ni lugha inayowaunganisha watu wote Kimataifa. 

Mombeki anadokeza kuwa wanafunzi waliofundishwa kwa misingi ya kiingereza tangu wakiwa wadogo wana nafasi kubwa ya kufikia malengo yao ikilinganishwa na wale walioanza elimu yao ya  awali na msingi kwa lugha ya kiswahili.

Anabainisha kuwa kuna wanafunzi wengi kutoka Mataifa ya Afrika, Amerika na Ulaya wanapenda kufika katika Centre hiyo ambayo ilianza kutoa elimu ya lugha mbalimbali tangu mwaka 1998. Pia inafundisha lugha ya Kiswahili pamoja na lugha za asili ikiwemo Kisukuma pamoja na Mila na Desturi za Tanzania.
Imeandaliwa na George Binagi

UNILEVER YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI TUMAINI-JIJINI DAR

 Balozi wa Blue Band Ayubu Athumani akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa darasa la sita Joseph Deogratius wa shule ya msingi Tumaini iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka mshindi katika shindano la Band ‘Kula Tano’, jana. Wapili kulia ni mwalimu wa michezo Naelijwa Shaidi.

WAKABIDHIWA JENGO LA MAFUNZO NA MADAWATI KILOMBERO

 Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi  jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa  5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
 Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero
Mke wa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Louise Bainbridge akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilombero, Muungano, Kantui, Ujirani, Lyahira na Mapinduzi (hapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati  jana, Kilombero. Katiakti ni Meneja Mkuu wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mark Roe-Scott na kulia ni meneja utawala wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Allawi Mdee.

KAMPUNI YA MAGARI YA ALLIANCE AUTOS WAFANYA MAONYESHO NDANI YA JENGO LA GOLDEN JUBILEE TOWERS(PSPF)

DSC_1573
Gari aina ya Amarok Pick up ikiwa katika maonyesho ya mauzo ndani ya jengo la Golden Jubilee Towers ambapo maonyesho hayo ambayo yanaenda sambamba na uuzwaji wa magari hayo yanaendelea hadi hapo kesho jioni kwa 'showroom' hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).
DSC_1562
Amarok Pick up inavyoonekana kwa ubavuni..
DSC_1563
Amarok Pick up inavyoonekana upande wa nyuma..
DSC_1566
Gari aina ya Touareg ambayo katika 'showroom' hiyo ya jengo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam kama inavyoonekana.
Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa kampuni ya magari ya Alliance Autos, ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen Tanzania (VW), Sheikha Said amebainisha kuwa, maonyesho hayo ya magari na mauzo yaliyoanza jana 26 Januari, yanatarajiwa kufikia tamati siku ya kesho 28 katika jengo hilo la Golden Jubilee Towers.
"Magari yaliyo kwenye 'showroom' hii ya ndani ya jengo la Golden Jubilee Towers ni pamoja na Amarok Pick up na Touareg. Tumeyaleta karibu zaidi na wateja wetu wapate kuyaona na kujua uhalisia wa 'German Engineering'. Na pia waweze kujibiwa maswali yao yote yanayowatatiza, kujua uwezo wa VW katika barabara zote" ameeleza Meneja masoko huyo.

NYOTA YA KIKAPU WA MALAWI KUZIKABILI TIMU ZA DAR

 Mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi. Wa kwanza kulia waliokaa ni mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo, wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.


 Mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo  kiongeana waandishi wa  wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu  mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi wa Sprite BBall Kitaa. Wa kwanza kushoto waliokaa ni mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani na wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
*************************
Miamba miwili ya mpira wa kikapu kutoka nchini Malawi imewasili jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu za bigwigs Jogoo, East Zone One, Mbezi na West Zone Three. Mechi hizo zenye hamasa ya aina yake zitachezwa kwenye uwanja Bball Kitaa Park, karibu na Ukumbi wa Gymkhana.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na mratibu wa Bball Kitaa Karabani Karabani pazia la michezo hiyo litafunguliwa kesho ambapo East Zone One watakipiga na Bricks, mchezo unaotabiriwa kuwa ni mgumu na wa kusisimua. Siku hiyo hiyo Mbezi watacheza na Associate Team, mchezo ambao pia unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Michezo hiyo bado itaendelea kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo West Zone Three watapambana na Bricks kabla ya Jogoo kuwakaribisha Associate team. “Tuna furaha kubwa kuandaa michezo hii ya kirafiki. Ni moja ya sehemu muhimu katika kudumisha mahusiano, vile vile kuendeleza vipaji vinavyochipukia”, Karabani alisema.
Ujio wa Bricks na Associate teams jijini Dar es Salaam imeonekana si jambo geni baada ya timu za East Zone One na West Zone Three kwenda Malawi mwaka jana. Zikiwa nchini humo, timu hizo zilishinda mechi zao kadhaa.
Karabani ambaye michuano yake ya mpira wa kikapu iko chini ya udhamini wa Sprite, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibua na kukuza vipaji  vya vijana kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo michuano hiyo imekuwa ikifanyika. Vilevile michuano hii inatoa fursa ya kuendeleza ushirikiano baina ya maeneo mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi.
 “Lengo letu ni kuanzisha michuano ngazi ya kanda mwishoni mwa mwaka huu, ambapo mabingwa kutoka Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe”, Karabani alisema na kuongeza kuwa uzinduzi wa michuano hiyo utafanyika nchini Malawi
Kwa upande wake, Meneja Biashara wa Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka alisema anajisikia furaha kubwa kutokana na heshima waliopewa kuisapoti michuano hiyo hapa nchini na kusisitiza kuwa kampuni yake itaendeleza ushirikiano wake na wadau wa mchezo wa kikapu kuzidi kuutangaza mchezo huo.
 “Sote tunafahamu kuwa mpira wa kikapu ni moja ya michezo maarufu na yenye nguvu nchini, hasa miongoni mwa vijana ambao wanahitaji aina hii ya msaada ili kuhamasika na kuweza kuendeleza vipaji vyao”, Njowoka alisema.

UNESCO YAFANYA KONGAMANO LA KUJADILI MPANGO WA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU (ESDP)KWA MWAKA 2017-2021

IMG_1467
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu, Prof. Eustella Bhalalusesa akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP). Kushoto ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_1499
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na kongamano hilo la siku mbili linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NACTE jijini Dar es Salaam.
Na Rabi Hume wa Modewjiblog
Katika kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua yenye ubora zaidi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limepanga kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuandaa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), mpango ambao umelenga kusaidia serikali ya Tanzania kutengeneza maudhui na mikakati ya kuendeleza elimu kwa upande wa Tanzania bara.
Akizungumzia mpango huo katika kongamano la siku mbili la kutambua vipaumbele vinavyotakiwa katika kuandaa mpango huo wa elimu, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila alisema mpango huo unatarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano kwa kuanzia mwaka 2017 – 2021 ili kuona ni jinsi gani utabadili elimu ya Tanzania.
Alisema kupitia kongamano hilo wanataraji kuchagua baadhi ya vipaumbele ambavyo wataona vinaumuhimu zaidi kuanza navyo kwa miaka mitano ya kwanza kwa mpango huo na baadae wataanza utekelezaji wa vipaumbele ambavyo vitakuwa vimepewa kipaumbele na washiriki wa kongamano hilo.
“Tupo hapa kufanya tathimini ya vipaumbele ambavyo vimeletwa mbele yetu ili tufanyie uchambuzi na tuone ni vipaumbele vipi tutaviweka kwenye mpango wa miaka mitano katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” alisema Mnjagila.
Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Makuru Petro ambaye ameshiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO alisema katika kuchambua elimu ya Tanzania wamegundua kuwa elimu imekuwa ikishuka na hilo linatokana na kuongezeka kwa wanafunzi wanaosajiliwa kuanza shule huku kukiwa hakuna maboresho ambayo yanafanyika ili kuboresha elimu hiyo.
Alisema baada ya uchambuzi kufanyika wanafanya tathmini ili kupata matokeo ambayo watajadili kwa pamoja kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka mashirika ya kiserikali na yasiyo ya serikali ili kupitisha vipaumbele ambavyo vitafanyiwa kazi kati ya vipaumbele ambavyo wao waliwasilisha kwa washiriki hao.
“Elimu ya Tanzania hali sio nzuri tumefanya uchambuzi hata mashuleni hakuna hali nzuri mfano hata Geita tumekuta darasa moja linatumiwa na wanafunzi 80 hadi 100 na hilo ni tatizo na baada ya kuchambua changamoto na kuzifanyia tathmini tunazileta hapa ili tuchague vipaumbele vya kuanza kuvifanyia kazi,” alisema Petro.
Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa shirika hilo nchini, Zulmira Rodrigues alisema lengo la kuweka mpango huo ni kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuifanya kuwa bora na iliyo na usawa kwa makundi yote ya jamii kwa matokeo mazuri ya baadae.
Alisema kuna mambo ambayo yanatakiwa kupewa vipaumbele ikiwepo ni pamoja na ubora wa elimu, fursa za elimu kwa makundi yote katika jamii na kujenga uwezo kwa watendaji ambao wanatoa hiyo elimu kama ni walimu basi wawe wanapewa mafunzo kuendana na wakati uliopo ili kuwa na kitu kipya ambacho kinahitajika kwa wanafunzi kwa wakati huo.
IMG_1506
Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Ufaransa, Anton De Grauwe akiwasilisha vipengele mbalimbali vinavyotakiwa kujadiliwa na washiriki wa kongamano hilo katika kuandaa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021.
IMG_1683
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akiwasilisha mambo mbalimbali muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa kwenye Ajenda 2030 ya elimu na mpango wa utekelezaji katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).
IMG_1666 IMG_1683 IMG_1591
Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta (kushoto) akiteta jambo na Maofisa wenzake kutoka UNESCO, Faith Shayo (katikati) na Leonard Kisenha (kulia) wakati kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 likendelea.
IMG_1570
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Bw. Makuru Petro ambaye akishiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO kwenye kongamano hilo.
IMG_1642
Mshauri wa Taasisi ya kimataifa ya mipango ya elimu (IIEP)/UNESCO, Barnaby Rooke akielekeza vipaumbele kwenye bajeti ya sekta ya elimu ambayo inahitaji maboresho makubwa ili kuleta mabadiliko kwenye sekta elimu nchini.
IMG_1596
Moja ya 'Papers' zilizowasilisha kwa washiriki.
IMG_1615
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akishiriki kwenye kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za NACTE jijini Dar es Salaam.
IMG_1738
Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Joseph Sekiku akitoa maoni kuhusiana na udhaifu wa mipango ya sekta elimu nchini ambayo haitekelezeki wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).
IMG_1784
Bi. Helena Reutersward, kutoka Ubalozi wa Sweden kitengo cha Elimu akitoa maoni wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) nchini linaloendelea katika ukumbi wa mikutano NACTE jijini Dar es Salaam.
IMG_1654
Pichani juu na chini ni wajumbe walioshiriki kongamano hilo kutoka taasisi mbalimbali za serikali, Wizara ya Elimu, Taasisi za Elimu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
IMG_1539
IMG_1515 IMG_1533