Pages

KAPIPI TV

Monday, February 8, 2016

WATOTO 53,581 WAANDIKISHWA ELIMU YA AWALI TABORA

Na Allan Ntana, Tabora 

 MKOA wa Tabora umefanikiwa kuandikisha jumla ya watoto 53,581 wa kuanza elimu ya awali katika mwaka wa masomo 2016 . 

 Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia elimu mkoani Tabora Juma Mhina ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mkoa huo katika kikao cha wadau wa elimu kilichoketi hivi karibuni mjini hapa kikishirikisha maofisa kutoka halmashauri zote 7 za mkoa huo. 

 Alisema idadi hiyo ni ya watoto wote walioandikishwa katika halmashauri zote za mkoa huo ambapo idadi halisi ya watoto waliotarajiwa kuandikishwa ni 74,773 wavulana wakiwa 37,581 na wasichana 37,192. 

 Katika makisio hayo alisema wavulana walioandikishwa ni 21,664 sawa na asilimia 57.6 na wasichana ni 21,917 sawa na asilimia 58.9 ambapo jumla ya watoto wote walioandikishwa katika wilaya zote ni 53,581 sawa na asilimia 71.6. 

 Alifafanua kuwa halmashauri ya Manispaa ya Tabora imefanikiwa kuvuka lengo la makisio yake ambapo watoto waliotarajiwa kuandikishwa ni 4881 lakini walioandikishwa ni 5099 sawa na asilimia 104.5. 

 Mbali na Manispaa, alitaja takwimu za makisio ya kila halmashauri na idadi halisi ya watoto walioandikishwa ikiwa kwenye mabano kama ifuatavyo Igunga 17,844 (11,675), Nzega 16,643 (7,586), Urambo 8,433 (4,517), Sikonge 6,446 (2,227), Uyui 8,206 (4,801), Kaliua 9,944 (5,758) na Nzega Mji 2,376 (1,916). 

 Akizungumzia zoezi la uandikishwaji watoto wa kuanza darasa la kwanza Mhina alisema Mkoa huo umefanikiwa kuandikisha jumla ya watoto 64,642 sawa na asilimia 70.6 wakati matarajio ilikuwa kuandikisha watoto 91,506. 

 Aliipongeza halmashauri ya Manispaa Tabora kwa kufanikiwa kuvuka lengo la uandikishaji ambapo iliandikisha watoto 7,644 sawa na asilimia 110 wakati matarajio yalikuwa kuandikisha watoto 6,924. 

Alitaja takwimu za watoto walioandikishwa darasa la kwanza kwa kila halmashauri idadi iliyotarajiwa ikiwa kwenye mabano kama ifuatavyo Sikonge 2,569 (5,288), Kaliua 10,522 (16,042), Uyui 10,217 (16,571), Urambo 7,301 (8,844), Manispaa 7,644 (6,924), Igunga 11,675 (17,844), Nzega 12,678 (16,898) na Nzega Mji 2,036 (2,111).

No comments: