Pages

KAPIPI TV

Monday, July 20, 2015

DC WA KINONDONI, PAUL MAKONDA AZINDUA KISIMA CHA MAJI SAFI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA WATOTO WETU TANZANIA KILICHOJENGWA NA KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati), akimkaribisha  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akiwasili kwenye hafla ya kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana.

DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
Mmoja wa vijana wa kituo hicho akiigiza igizo kuonesha changamoto zinazowakabili watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete (kulia), akizungumza katika hafla ya kuzindua kisima hicho. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Naibu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobard Bubelwa (kulia), akiteta jambo na Chief Commerial Officer wa Zantel, Sukwinder Bajwa wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Watoto wa kituo hicho na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Watoto wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akipokea risasi ya watoto wa kituo hicho.
Vijana wa kituo hicho wakitoa burudani.

DC Makonda akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alitoa ahadi ya kuwasomesha baadhi ya wanafunzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akifungua pazia wakati akizindua kisima cha maji katika Kituo cha Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana. Kisima hicho kimejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Simu ya Zantel.
DC Makonda akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa kisima hicho.
Hapa DC Makonda akimtwisha maji mmoja wa wanafunzi wa kituo hicho baada ya kukizindua.
DC Makonda akimkabidhi kitabu, mtoto Yusla Omari kwenye uzinduzi huo.
DC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya kituo hicho.



Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Simu ya Zantel jana ilitoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha  upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.
Kisima hicho kilichokabidhiwa jana kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka

‘Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano hayo, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.

‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.

Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.

Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.


‘Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili’ alisema Tegete. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

KALUNDE BAND KATIKA UBORA WAO, WAFANYA KWELI KLABU YA GMB MBEZI

????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiimba wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika klabu ya GMB Mbezi jijini Dar es salaam Maarufu kwa Mbaga katika siku ya pili ya sikukuu ya Idd , kulia ni mwanamuziki Bijuu wa bendi hiyo.
????????????????????????????????????
Wanamuziki wa bendi hiyo wakiimba katika onesho hilo lililofanyika kwenye klabu ya GMB Mbezi jijini Dar es salaam.
???????????????????????????????????? ????????????????????????????????????
Mwanamuziki Debora Nyangi wa pili kutoka kulia mwimbaji na Meneja wa bendi hiyo akioongoza waimbaji wenzake wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza jana kwenye klabu ya GMB Mbezi.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa bendi hiyo Bijuu akiimba huku wanenguaji wakifanya vitu vyao.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa bendi ya Kalunde Gringo Junior kushoto akishoo Love na wadau wa bendi hiyo Teddy Mwanambilimbi katikati na Fina Mwanambilimbi kulia.
????????????????????????????????????
Gringo Junior akifanya vitu vyake jukwaani.
????????????????????????????????????
Wangenguaji wa bendi hiyo wakifanya vitu vyao jukwaani.

Saturday, July 18, 2015

STARTIMES YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA SHULE YA MSINGI MAALUMU YA AIRWING JIJINI DAR ES SALAAM

Kutoka kulia ni wafanyakazi wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Elena Liu na Paulina Kaka wakifurahia jambo pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili, Bw. Issa Mkasa wakati wa kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengineyo shuleni hapo. Akishuhudia tukio hilo kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bi. Fabiola Malisa.
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (mwenye hijab) akikabidhi moja ya msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Airwing, kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Wakishuhudia tukio hilo kutoka wa pili kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa na Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa (kushoto) akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakati wa kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengineyo kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kitengo maalum cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili shuleni hapo. Akishuhudia tukio hilo katikati ni  Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (mwenye hijab) akikabidhi moja ya msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Airwing, kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Wakijumuika pamoja naye katika tukio hilo wa pili kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa na wa pili kushoto ni Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.


Na Mwandishi Wetu 

Serikali yaombwa kutilia mkazo kuhakikisha kila shule ya msingi inakuwa na kitengo maalumu cha wanafunzi wenye ulemavu wa viungo mbalimbali ili kuwapatia na wao fursa ya kupata elimu.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa wakati wa kupokea msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa ajili ya kitengo maalumu cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili.

Bi. Malisa alisema kuwa shuleni kwake wanacho kitengo cha kuwafundisha wanafunzi wenye ulemavu wa akili ambao kwa sasa wapo jumla ya 65, wanafunzi 20 ni wasichana na wanafunzi 45 ni wavulana.

“Hapa kitengo maalumu cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili ukiachana na wanafunzi wengine wa kawaida. Kwa sasa tunalo darasa moja ambalo tunawafundishia kwa kupeana amu na wanafunzi wa darasa la pili. Yaani wao wanaingia asubuhi na kutoka saa tano baada ya hapo wanafunzi wengine hulitumia hilo darasa. Tumeamua kufanya hivi kutokana na uhaba wa madarasa wenyewe.” Alisema Bi. Malisa

“Kuanzishwa kwa kitengo hiki lengo ni kuwafundisha watoto hawa wenye ulemavu wa akili nao waweze kupata stadi mbalimbali za kujumuika pamoja na jamii inayowazunguka. 

Jamii hudhani kuwa motto akizaliwa na ulemavu wa aina yeyote ile anakuwa ni mtu tegemezi. Sisi tunakanusha suala hilo kwani tunao hapa ambao tunawafundisha na wengi wameonyesha maendeleo mazuri. Kwa mfano kuna ambao baada ya kumaliza vipindi darasani hurudi wenyewe majumbani na hata kuja wenyewe shuleni kila siku.” Alisema na kuongezea Bi. Malisa

“Sisi kama uongozi wa shule tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuwasaidia watoto hawa ili wajitambue na kuweza kuishi na jamii. Na tumefanikiwa kwa hilo, kwa mfano tunao wanafunzi wawili ambao baada ya kufundishwa kwenye kitengo hiki na kuonyesha maendeleo mazuri wamejiunga na wanafunzi wa kawaida, mmoja yuko darasa la saba na mwengine la nne,” alisema na kuongezea Mwalimu Mkuu, “Na tena wanasoma bila shida yoyote na wanafunzi wengine wamewazoea wanasoma pamoja nao.”

“Changamoto kubwa tunayokumbana nayo nib ado tuna uhaba wa madarasa kama nilivyoelezea awali tunatumia darasa kwa awamu. Kwani wao wanahitaji muda zaidi tofauti na wanafunzi wa kawaida. Japokuwa tunapokea msaada kutoka serikalini, kwa makampuni na taasisi zingine bado hautoshi. Tunaomba serikali itilie mkazo zaidi kwa kila shule kuwepo na kitengo cha namna hii kwani hali hiyo itapelekea wazazi kutowaficha watoto majumbani. Pia vituo hivi huwapunguzia wazazi mzigo mkubwa wa kuwalea kwani huwa salama mahali hapa na kuwafanya wao kufanya shughuli zingine za kujenga taifa.” Alihitimisha Bi. Malisa

Naye kwa upande wake akiongea kwa niaba ya wafanyakazi, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa wao kama kama kampuni na watanzania wameguswa sana na ustawai watoto hawa ambao jamii huwachukilia tofauti.

“Bado watanzania tunayosafari ndefu ya kubadili mtazamo juu ya watoto wenye ulemavu. Tunatakiwa kuondoa dhana ya bado kufikiria ukiwa na motto mlevu basi atakuwa tegemezi kwa maisha yake yote duniani. Ulemavu unatofautiana na ule ambao unaweza kutibika watoto hawa wasaidiwe. Lakini jambo hili halitowezekana kama serikali haitojenga vituo hivi kwenye kila shule ya msingi na pia wadau nao kujitokeza kuziunga mkono.” Alisema Bi. Hanif

“Na kusema ukweli mahitaji ambayo yanahitajika katika shule hizi yamo ndani ya uwezo wetu watanzania. Bado tunahitaji mwamko wa kutosha kwani si wazazi wote wanao uwezo wa kumudu gharama za kuwahudumia watoto wenye ulemavu. 

Tumekuja hapa tumezungumza na walimu wametupa hali halisi kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi hawa uwezo wao ni mdogo hivyo wanahitaji misaada yetu,” alisema na kumalizia Bi. Hanif, “Hivyo basi kwa msaada wetu huu ambao sisi wafanyakazi wa StarTimes tumejikusanya na kuutoa, tunatarajia pia makampuni na taasisi nyingine wataiga na kufanya hivyo. Ni jukumu letu sote kuwasaidia na kuwalea watoto hawa kwani Mungu ana makusudio yake kuwaumba hivi.”


Msaada wa wafanyakazi wa StarTimes Tanzania uliotolea kwa kitengo hiko cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili shuleni Airwing ni pamoja na sukari, mikate, majani ya chai, blueband, chumvi, sabuni za unga na mche, vibiriti, na mengineyo. Msaada huo umelenga kuwahudumia wanafunzi hao kwa muda ambao wapo shuleni na kwa wazazi na walezi wa wanafunzi hao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

"MWAKASAKA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA TABORA MJINI"AJIVUNIA KUWA KARIBU NA KUWATUMIKIA WANANCHI

Mjumbe wa Mkutano mkuu CCM Taifa  Bw.Emmanuel Mwakasaka akichukua fomu ya kuomba ridhaa kwa chama chake kumteua kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini  ambapo pamoja na mambo mengine Bw.Mwakasaka amesisitiza  umuhimu wa kuwatumikia Wananchi wa Jimbo la Tabora mjini hatua ambayo itazidi kuimairisha Imani ya Wananchi kwa Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi ambayo imefanya mambo makubwa licha ya kukabiliwa na Changamoto mbalimbali ambazo kwasasa zinahitaji mtu makini wa kuweza kufuatilia na kuzifanyia kazi kwa kuwashirikisha wananchi ambao watahamasishwa kuainisha vipaumbele vyao ikiwemo kero mbalimbali.
HISTORIA KATIKA PICHA:_Bw.Mwakasaka  akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda ikiwa ni utambulisho rasmi wa Chama hicho kutokana na namna ambavyo amekuwa akijitolea kukisaidia Chama katika masuala mbalimbali ya Maendeleo mkoani Tabora..Mwakasaka mbali na kuwa ni Mwanasheria ameshika nafasi mbalimbali za uongozi hadi sasa ni Mjumbe wa kamati ya Siasa,Mjumbe wa uchumi na fedha Wazazi mkoa wa Tabora,Mlezi wa Chipukizi na Green Guard pamoja Mlezi wa Chama cha Netball mkoa wa Tabora. 



"BANDORA WA SALU SECURITY ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA TABORA MJINI"ATAJA VIPAUMBELE VYAKE IKIWEMO KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Kada wa Chama cha Mapinduzi Bw.Bandora Mirambo akirudisha fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Ubunge kupitia CCM jimbo la Tabora mjini ambapo alitaja vipaumbele vyake ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi huku akiweka bayana kuwa Wananchi wamekuwa wakikosa fursa ya kupata mtu  sahihi kwa muda wa miaka mitano iliyopita   ambaye  angeweza kusikiliza kero zao na kuziwasilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo kupunguza malalamiko yao dhidi ya Serikali ya CCM.
Baadhi ya wakazi wa Jimbo la Tabora mjini wakimpongeza Bw.Bandora kuchukua na kurudisha fomu ya Ubunge jambo ambalo wamedai limewafariji kwakuwa hivi sasa wanahitaji mabadiliko yatakayoleta maendeleo ya haraka.


MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA UYUI BW.MUSSA NTIMIZI ACHUKUA FOMU YA KUOMBA RIDHAA YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA IGALULA

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Bw.Mussa Ntimizi akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa kwa chama chake kiweze kumteua kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Igalula ambapo ametaja vipaumbele vyake kadhaa ikiwa ni pamoja kutatua kero za wananchi ikiwemo tatizo la maji,miundo mbinu ya huduma za Afya pamoja kilimo cha tumbaku kwa wakulima wa wilaya ya Uyui.
Ntimizi akisaini kuchukua fomu ya kuomba ridhaa  kwa CCM ya kuwania Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mussa Ntimizi akionesha fomu kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari mjini Tabora.




RAIS WA CHAMA CHA WAAJIRI AFRIKA BW.ALMAS MAIGE ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA TABORA KASKAZINI

Rais wa Chama cha Waajiri Afrika na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi  ya Ulinzi nchini  Bw.Almas Maige achukua fomu ya kuwania Ubunge kupitia kura za maoni CCM jimbo la Tabora Kaskazini,ambapo moja kati ya vipaumbele vyake endapo CCM itampa ridhaa na kufanikiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini atashughulikia kero mbalimbali zikiwemo za ukosefu wa maji pamoja na matatizo ya Wakulima wa zao la tumbaku.


Friday, July 17, 2015

BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE WA VITI MAALUM,VIJANA MBEYA ATOA VIPAUMBELE VYAKE

Bi. Chikulupi Njelu Kasaka 
Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Mbeya Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) akikabidhiwa Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Mbeya na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu
 Kushoto ni Bw. Moses Mwakibinga Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Chunya, Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto)  na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu Baada ya kukabidhiwa Fomu

                  MFAHAMU BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA


*Anaitwa Chikulupi Njelu Kasaka.

*Ni Mwanasheria (wakili) kitaaluma.


*Ni mfanyakazi wa Bunge la JMT
.
*Sasa anawania Ubunge wa Viti-maalum (vijana).


*WASIFU WA MGOMBEA: BI. CHIKULUPI KASAKA

ELIMU:
Chikulupi Kasaka ni mzaliwa wa Chunya na babu na Bibi ni wakazi wa Kijiji cha Mtanila katika Wilaya ya Chunya.

 Chikulupi alizaliwa mwaka 1986 na kuanza elimu ya msingi mwaka 1994 katika shule ya Chunya Kati. Chikulupi alimaliza elimu ya msingi Mkoani Tabora na kuchaguliwa kwenda shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo Dodoma ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 2000-2004. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Loleza iliyopo Mkoani Mbeya. Alishaguliwa kijunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2007 kusomea Shahada ya Kwanza ya Sheria na kumaliza mwaka 2011. Mwaka 2013 alijiendeleza kwa kujiunga na mafunzo ya uanasheria kwa vitendo na kumaliza mwaka 2014 katika chuo kiitwacho Law School of Tanzania ambapo baadaye niliapishwa kuwa wakili.

UZOEFU KATIKA UONGOZI:
Chikulupi aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi akiwa anasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alikuwa Mbunge katika Serikali ya wanafunzi - DARUSO.

 Chikulupi alichaguliwa mwaka 2009 kuwa Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Afrika Mashariki uitwao East Africa Community Students Union -EACSU.

 Pia alikuwa Afisa Mahusiano ya Umma katika Taasisi ya wanafunzi wa Sheria iitwayo University of Dar es Salaam Human Rights Association –UDHRA. Mwaka 2010 alishiriki mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yaliyofadhiliwa na Shirika la Kijeruman liitwalo Friedrich Ebert Stiftung –FES.

 Pia mwaka 2014 alishiriki mafunzo ya Viongozi Vijana toka barani Afrika nchini Marekani ambao alisomea masomo ya Public Management katika chuo cha Howard kilichopo Washington. Pia nilipata fursa ya kukutana na Rais Barack Obama ambae ni mwanzilishi wa mafunzo haya.

UZOEFU NDANI YA CHAMA/UVCCM:
Chikulupi Kasaka alijiunga na CCM hasa katika jumuiya ya UVCCM mara tu baada ya kumaliza elimu ya sekondari 2006. 
Alipokuwa anasomea Shahada ya Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alijikita katika shughuli mbalimbali za kuimarisha chama na mwaka 2010 alichaguliwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi ya Abiyan-Chuo Kikuu. Na mjumbe wa Shirikisho la Vyuo Vikuu wanaCCM, Mkoa wa Dar es Salaam.

KAZI:
Mara baada ya kumaliza chuo kikuu Julai 2011 Chikulupi alifanya kazi katika Shirika la Wakimbizi katika Mradi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uitwao International Migration Management Program (IMMP). 

Mwaka 2012 aliajiriwa na Serikali kama Hakimu Mkazi daraja 2, katika Mahakama ya Mwanzo Makongorosi-Chunya, Mbeya. Mwishoni mwa mwaka 2012 nilijiunga na utumishi wa Chama Makao Makuu ya CCM Dodoma. 

Nilipangiwa kufanya kazi za Chama katika Upande wa Bunge hasa za kisheria. Tangu kipindi hicho mpaka sasa Chikulupi anafanya kazi kama Msaidizi wa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, Bungeni Dodoma.

VIPAUMBELE:
Chikulupi Kasaka anaomba ridhaa yako ili aweze kuwawakilisha vijana wa Mkoa wa Mbeya katika nafasi ya Uongozi wa Kitaifa kupitia ngazi ya Ubunge wa Viti Maalum-Vijana. 

Kama mkazi wa Mbeya naamini vijana wa Mbeya wanauwezo, nguvu, bidii na jitihada katika shughuli zao za kila siku. Lakini mimi nitapigania kuwapatia vijana wa Mbeya fursa nyingi zaidi katika vipaumbele vifuatavyo: 

ELIMU, AJIRA, MICHEZO, UTALII na AFYA.
ANAOMBA UMUUNGE MKONO KWA FURSA ZAIDI KWA VIJANA WA MKOA WETU WA MBEYA.


ANSWAR-SUN WASWALI IDD EID FITRI JANGWANI DAR ES SALAAM LEO

 Amiri wa Jumuiya ya Answari Suna Tanzania, Shekh. Juma Omari Poli (kulia), akiswalisha Swala ya Iddi katika viwanja hivyo.
 Shekh Hamid Abdallah, akitoa mawaidha wakati wa ibada ya Swala ya Idi katika Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam leo.

Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Waumini wa madhehebu ya Anwar-Suni wakiswali katika viwanja hivyo.

SKYLIGHT BAND YAENDELEA KUUNGURUMA NDANI YA KIOTA KIPYA CHA LUKAS PUB MASAKI,USIKOSE LEO

 
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (wa pili kutoka kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Lukas Pub jijini Dar.
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight Shuu akiimba pamoja na msanii mwenzake Kasongo Junior haya ni Majembe mapya ya bend ya Skylight
Ilikuwa noma sana siku ya Ijumaa iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight
Mashabiki wa Bend ya Skylight wakiendelea kuserebuka.
Sony Masamba akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake ndani ya kiota kipya cha Lukas kilichoko Masaki jijini Dar.
Sakata rhumba na Skylight band hapana chezea hatareee ukigusa lazima unase
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight Shuu akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ( hawapo pichani) uku akisindikizwa na waimbaji wenzake Sony Masamba (kushoto) pamoja na Ashura Kitenge.(kulia)
Katika bend ya Skylight ni full burudani.
Skylight Band ni mwendo wa kutoa raha sana tukutane Ijumaa hii ndani ya kiota cha Lukas pub Masaki jijini Dar kwa kuburudika na band hii
Ndani ya Skyligt band ni full burudani.
Ilifika time ya Nigeria Flavour….. Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu kwenye ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Mashabiki wakiendelea kuserebuka nyimbo za Skylight.