Pages

KAPIPI TV

Friday, July 3, 2015

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LANG'ARA MAONYESHO YA 39 YA SABASABA

NHC YANYANG'ANYA MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI BAADHI YA HALMASHAURI ZILIZOSHINDWA KUTUMIA FURSA

● Mkoa wa Katavi na Rukwa washindwa kutumia fursa ya msaada huo ● NHC yanyang’anya mashine Halmashauri za Mikoa hiyo ● Zatakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara Katika kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatunzwa, kutumika ipasavyo na kuhakikiwa, NHC imeendelea kuwakagua vijana waliopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali yatakayowezesha wananchi kujijengea nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote za Mikoa ya Katavi, Mbeya na kukamilika Mkoani Iringa. Kwa ujumla, vijana wana ari ya kutosha ingawa wana changamoto zinazohitaji msukumo wa Halmashauri zao, hasa za masoko ya matofali yao pamoja na mtaji wa kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa benki ya matofali ya kuuzia wananchi. Katika ziara ya NHC Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya hizo wameomba NHC isiwanyang’anye mashine na wameahidi kuwapa vijana mikopo na kuwasaidia malighafi za kuwawezesha kutengezea matofali hayo ikiwemo mchanga, sementi na udongo maalum kwa kazi hiyo. Hata hivyo, Mikoa ya Rukwa na Katavi muitikio wa vijana na Halmashauri hizo ukiacha Halmashauri ya Mlele ambayo inafanya vizuri, umekuwa hafifu sana na Shirika limelazimika kuzinyang’anya Halmashauri hizo mashine na kuzitaka kuomba upya kama bado wana azma ya kutumia mashine hizo kujiletea maendeleo ya kuwa na nyumba bora na kukuza ajira kwa vijana wao. Fuatilia yaliyojiri katika uhakiki huo katika picha.
New Picture (1)  
Kikundi cha ‘Mshikamano’ katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kikimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC BW. Muungano Saguya akiwaelezea namna ya kukuza ujuzi na kutumia Halmashauri zao kuongeza ufanisi wa kazi alipowatembelea nakusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili. Vijana hao wameshapewe eneo la muda la kuendesheea shughuli zao na wameanza kutengeneza tofali kwa ajili ya kuwauzia wanmanchi.
New Picture (2)
Hii ndiyo hali iliyojitokeza Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda pale NHC ilipolazimika kuzitwaa mashine ilizotoa msaada kwa vijana ili waweze kujiajiri. Kikundi hiki cha Mpanda Hotel ni mojawapo ya vikundi vilivyonyang’anywa mashine Mkoani Katavi na Rukwa kwa Halmashauri sita za Mikoa hiyo ukiacha Mlele inayofanya vizuri, kushindwa kuzitumia mashine hizo ipasavyo. Halmashauri hizo zimetakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara baada ya kubainika kuwa vikundi vya awali vilundwa kisiiasa.
New Picture (3)
Kikundi cha vijana cha ITIMBA kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini kikimsikiliza` Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Kasibi Saguya alipowatembelea ili kujuwa changamoto zinazowakabili. Kikundi hicho kimeshapata kazi za watu binafsi na shule ili kuwajengea majengo mbalimbalia na hivyo kupata fedha za kujiendeleza. Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini imekubali kuwapa vijana hao ardhi na maeneo ya kufanyia kazi.
New Picture (4)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bw. James Milanzi akimsikilza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipofika Ofisini kwake kukumbusha wajibu wa Halmashauri za Wilaya wa kusaidia vijana ili waweze kutengeneza matofali ya kujengea nyumba za gharama nafuu na kujipatia ajira. Halmashauri hiyo imepiga marufuku ukataji miti kwa ajili ya kuchoma matofali na badala yake wananchi wametakiwa kutumia matofali rafiki wa mazingira yanayozalishwa kwa kutumia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana katika Halmashauri zote nchini.
New Picture (5)
Kikundi c ha “CHAPAKAZI” Wilayani Mbarali kikiwa kinamsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea kujuwa changamoto zinazowakabili.Halmashauri ya Mbarali imesaidia vijana vifaa na maeneo ya kutengenezea matofali hayo na vijana wamehamasika baada ya kuhakikishiwa soko la tofali zao.
New Picture (6)
Kikundi cha “JITEGEMEE NA CALVARY “ Wilayani Tukuyu kikiwa tayari kumsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamiii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea ili kujuwa changamoto zinazowakabili. Kikundi hicho kimeishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Tukuyu kwa kuwapa eneo la kufanyia kazi na masoko ya tofali wanazatengeneza. Kushoto ni Meneja wa NHC Mkoa wa Mbeya Bw. Anthony Komba.
New Picture (7)
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ubisimbali Jesiwande alipokutana na timu ya NHC na kuchangia hoja ya namna ya kuondoa changamoto za ajira zinazowakabili vijana nchini. Halmashauri hiyo ambayo vijana wake hawajafanya vizuri imeapa kuwapa vijana wake mikopo na kuwatafutia masoko ya matofali yao.
New Picture (8)
Kikundi cha “Umoja wa matofali imara” Wilayani Iringa Vijijini ambacho kimeshajenga jengo kubwa la kibiashara kwa kutumia mashine kilichopewa msaada na NHC kilipata fursa ya kutembelewa na ujumbe kutoka NHC na kupewa msasa na hamasa ya kuendelea kujiletea maendeleo kwa kutumia mashine hizo.
New Picture (9)
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bi. Sikitu Mwemsi (kulia) akiomba timu ya NHC iliyofanya mazungumzo naye Ofisini kwake kuwapa muda badala ya kuwanyang’anya mashine walizopewa baada ya Halmashauri hiyo kususua kuwasaidia vijana na kusimamia vikundi vyao. Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC ameipa Halmashauri hiyo mwezi mmoja kujiweka sawa na vijana wake kuanza kutumia kikamilifu mashine walizopewa msaada na NHC.
New Picture (10)
Timu ya NHC na Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ikiwa eneo linalotumiwa na kikundi cha vijana cha “Muungano Vijana Kilolo”kilichopewa msaada wa mashine na NHC ambapo walikagua kazi za vijana hao (hawapo pichani) ambapo Wilaya hiyo imeamua kuwapa mkopo vijana hao ili wawe na benki kubwa ya matofali.
New Picture (11)
Kikundi cha vijana cha “Umoja wa Wafyatua matofali” kilichopo katika Kata ya Mkwawa Manispaa ya Iringa kikiwa kimeanza kazi ya kutengeneza matofali kilipotembelewa na timu ya NHC kuona kazi zao. Hiki ni kikundi kinachofanya vizuri katika Manispaa hiyo yenye vikundi vinne vya vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC za kufyatulia matofali ya kufungamana.. UMOJA WA WAFYATULA MATOFALI MANISPAA YA IRINGA
New Picture
Kikundi cha SHIDEPHA ambacho kilipewa mafunzo ya namna ya kutumia mashine za kutengeneza matofali ya kufungamana na NHC kikiwa imara na timu ya NHC iliyowatembelea na kuamua kuwaongezewa uwezo kwa kupewa mafunzo na vifaa vya kufanyia kazi. Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC baada ya kuona juhudi zao aliamuru waongezewe mashine mbili ili wasonge mbele na Halmashauri imekitambua kikundi hicho.

Thursday, July 2, 2015

ZANTEL YATOA SH.MILIONI 5 KUSAIDIA CHAMA CHA MAALBINO TANZANIA KUTOA ELIMU KWA UMMA

Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu ushirikiano wao na chama cha Maalbino Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,  Progress Chisenga, na Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,  Progress Chisenga (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya (katikati), akizungumza katika mkutano huo wakati akiishukuru Zantel kwa msaada huo kwa chama hicho.
Meneja wa Chapa ya Zantel, Arnold Madale (kulia), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu msaada huo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose(wa nne kulia),   akikabidhi mfano wa  hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya (kushoto) kwa ajili kusaidia chama cha Maalbino Tanzania kutoa elimu kwa umma kuhusu changamoto walizonazo. Wengine ni maofisa kutoka chama cha Maalbino na maofisa wa Zantel.

Na Dotto Mwaibale


Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imekisaidia Chama cha Maalbino Tanzania katika mpango wake wa kusambaza elimu juu ya ulemavu wa ngozi kwa jamii pamoja na msaada wa jumla ya shilingi milioni 5 ambao unalenga kusaidia uendeshaji wa shughuli zake hapa nchini.

Zantel kwa kushirikiana na Chama Cha Maalbino kitajikita kutoa elimu hii kwa kusambaza ujumbe mfupi kwa wateja wake pamoja na kutumia vipindi vyake inavyodhamini ili kupeleka ujumbe kwa jamii kiujumla.

Pamoja na hiyo pia, Zantel inajipanga kutumia mikutano ya wafanyakazi pamoja na matamasha ili kuhakikisha ujumbe kuhusu ulemavu wa ngozi unawafikia watu wengi zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Pratap Ghose alisema mchango huo katika kuwawezesha Chama cha Maalbino ni sehemu ya huduma za kampuni yake kwa jamii.

“Tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu miongoni mwa wanajamii, na kwa hakika hatua kubwa imepigwa katika kupambana na tatizo hili tayari, na sisi kama Zantel tunaamini kwa kutumia uwezo wetu kama kampuni ya simu tunaweza kushiriki kulimaliza tatizo hili la mauaji ya ndugu zetu’ alisema Pratap.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Tanzania ina jumla ya watu wenye ulemavu wa ngozi 5,200 na wengi wao wanaishi kanda ya ziwa, na toka mwaka 2009 jumla ya kesi 155 zinazohusu walemavu wa ngozi zimeripotiwa kwa vyombo vya sheria kwa mujibu wa taasisi ya Under the Same Sun.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya, ameipongeza kampuni ya Zantel kwa mchango wao akisema utasaidia sana katika juhudi zao za kupigania haki za walemavu wa ngozi nchini.

‘Watu wenye ulemavu wa ngozi ni kama binadamu wengine wa kawaida, hivyo tunaiomba jamii isiwatenge ndugu zetu hawa’ alisema Kimaya.

Bwana Kimaya pia aliomba wadau wengine wajitokeze kuwawezesha walemavu wa ngozi waweze kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo.


“Jamii yetu ya walemavu wa ngozi ina matatizo mbalimbali, hivyo tunazidi kuwaomba watu binafsi, serikali pamoja na makampuni mbalimbali wazidi kujitokeza kusaidia kundi hili la jamii’ alisisitiza Kimaya.

BOSS WA UN, ALVARO RODRIGUEZ ATEMBELEA SABASABA, ASEMA MAONYESHO NI FURSA YA KUJIFUNZA

IMG_5941
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney Maleko (wa tatu kushoto) akiongozana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_5945
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati wakielekea katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lilipo Karume Hall mara tu baada ya kuwasili.
Na Modewjiblog team, Sabasaba
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa leo katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara Sabasaba amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa miradi na mikakati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa dunia sasa imekuwa kijiji kimoja na Umoja wa Mataifa umekuwepo Tanzania hata kabla ya uhuru, hivyo unakusudia kuendelea kuwepo kushirikiana na watanzania katika kutatua matatizo kwenye Nyanja mbalimbali.
Bw. Alvaro amewataka watanzania kusherehekea pamoja miaka 78 ya Umoja hapa nchini kwa kutoa maoni mbali mbali na kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.
Amesema kwa pamoja tunahitaji kuzungumzia usawa wa kijinsia, masuala ya kisiasa, mabadiliko ya tabia nchi na mambo ya kiuchumi kwa ajili ya ustawi wa taifa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko, ameushukuru Umoja wa Mataifa kwa kufanya juhudi za kusaidia vijana kuanzia ngazi za chini kabisa na kuwawezesha kuwa wajasiriamali.
Amesema kitendo cha Umoja huo kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba sambamba na kijana Amos Mtambala waliyemuwezesha kwa kumpatia mafunzo ya sanaa za uchoraji kumeleta hamasa kubwa miongoni mwa vijana wasio na ajira nchini.
IMG_6027
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_6032
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Umoja wa Mataifa.
IMG_5959
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu, akitoa maelezo jinsi wanavyoelimisha wananchi kuhusiana shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini sambamba na malengo ya millenia yanayofikia kileleni kwa Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambata na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko walipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5962
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akielezea maeneo ya Program mbalimbali za UNDAP yaliyofanikiwa nchini Tanzania kwa Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) aliyeambata na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko.
IMG_5965
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akikabidhi taarifa ya mwaka ya UNDAP kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (katikati) aliyefuatana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) walipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall.
IMG_5973
Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, akitoa maelezo jinsi alivyowezeshwa kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo ndani ya banda la Umoja wa Mataifa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5981
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) nchini, Magnus Minja akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuhusiana na program ya kazi njenje ya mradi wa kufundisha vijana katika shughuli za ujasiriamali inayoratibiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambapo kijana Amos iliweze kumuinua na kujiajiri kupitia sanaa ya uchoraji.
IMG_5995
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko, akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya karatasi inayotoa maelezo ya jinsi ya Watanzania wanavyoweza kushiriki kutoa maoni mbalimbali juu ya utendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kutuma SMS ambayo ni bure bila malipo yoyote na moja kwa moja kumfikia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Jinsi ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Ambapo pia njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kubofya link hii http://gpl.cc/UN2
IMG_6021
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko akizungumza na waaandishi wa habari katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa ambao wanashiriki maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_6038
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko mfuko wenye machapisho na vijarida mbalimbali vya Umoja wa Mataifa.
IMG_6467
Afisa Utawala wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Magoma (wa pili kushoto) akiuliza swali kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama na Wa pili kulia ni Mchumi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vainess Molle.
IMG_6476
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akijibu swali la Bw. Suleiman.
IMG_6494
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akionyesha namna ya kutoa maoni ya utendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kwa njia ya SMS ambayo ni bure kwa mitandao yote ya simu za mkononi nchini kwa wadau waliotembela banda la UN Tanzania.
IMG_6435
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez ajibu maswali mbalimbali yalitumwa kwa njia ya mtandao na wananchi katika banda la Umoja wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
IMG_5997
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaotoa huduma katika banda la Umoja wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
IMG_6456
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja na Mkuu wa UN Tanzania.