Pages

KAPIPI TV

Thursday, April 23, 2015

RAIS MSTAAFU MHESHIMIWA ALI HASSAN MWINYI AWASILI JIJINI WASHINGTON DC.

 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiambata na mama Sitti Mwinyi wawasili jijini Washington DC tayari kwa tamasha maalum la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa utawala Lilly Munanka wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, mara alipowasili hotelini.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi Edward Taji.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme.
  Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Emmanuel Swere.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi John Anbiah
     Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiwa ameongozana na mama Sitti   Mwinyi na baadhi ya msafara wake katika hoteli waliyofikia.
                                  PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI

BILLIONAIRE MO TO GIVE AWAY $100M THROUGH MODEWJI FOUNDATION

Mo-Dewji_0310-780x350
Mohammed Dewji, head of the $1.25bn MeTL Group and an MP in Tanzania, is set to launch a foundation in May to give away $100m of his fortune.
Dewji – ranked 31st richest person in Africa last year by Forbes – plans to gift around $2m from his fortune to the Mo Dewji Foundation on its launch, gradually building up the endowment fund to some $100m, he told Philanthropy Age.
“I earned my money in Africa,” said Dewji. “It is my responsibility and priority to give back.
The foundation will start with work across Tanzania, with the aim of extending its reach into other African countries. The focus areas of the foundation are still being developed, but education, healthcare, water access and enhancing purchasing power for the very poor are all being considered. The timeframe by which the foundation will reach its $100m target is still being decided, he added.
Dewji, 39, heads the Mohammed Enterprises Tanzania (MeTL) Group, an industrial conglomerate. Involved in local development for more than a decade through his political office, Dewji wants to use his foundation to extend his philanthropic reach throughout his country
Dewji has worked to improve quality and access to education, water, healthcare and agriculture in his constituency of Singida, central Tanzania, since becoming its MP in 2005.
“Just giving money is not enough,” said Dewji, who grew his father’s successful import-export operation into a sprawling business with interests in manufacturing, agriculture, real estate and textiles. “I’m planning to devote at least 10 per cent of my time to [my foundation] to start with.”
Dewji’s own philanthropic journey started in 2000, when he first sought the nomination for MP from his ruling Chama Cha Mapinduzi party. It was an old man’s hunt for water that prompted him to run for parliament, according to Dewji. “There was a puddle of yellow water and the old man had a bucket and a plate and he was scooping up the water and sand with it,” he said. “I went to see and just 5km outside of Singida I saw young children drinking yellow water from used PET [plastic] bottles.”
Elected in 2005 and again in 2010, to represent Singida district, Dewji has used his MP’s fund to build infrastructure in his constituency, including new bore wells, schools and eye care centres. He has worked with organisations such as the Bilal Muslim Mission, Lions Club and the Helen Keller Foundation to combat cataracts and preventable eye diseases.
Named a young global leader by the World Economic Forum, the billionaire is inspired by philanthropists such as Bill Gates, Warren Buffett and the Aga Khan he said. While he has not ruled out signing the Gates and Warren-backed Giving Pledge – where wealthy individuals commit to giving away more than half of their wealth to philanthropy – Dewji is clear he wants to strike out on his own and focus his efforts on Africa.
“The number of [African philanthropists in Africa] is growing,” said Dewji. “[But] we need the wave to get bigger and bigger and it has to trickle down.” There has been a shift in thinking on the continent as wealthy individuals start to consider giving much earlier on, he adds.
Since 2000, he has become more strategic in the way he uses funds, and says he is keen to apply some of the rigours of running a business to his foundation: “Whatever you do has to be viable, sustainable and for the long-term,” he said.
Source click here

UTIAJI SAINI MANUNUZI YA ENEO LA OFISI KWENYE JENGO LA MOROCCO SQUARE KATI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC NA SOKO LA HISA LA DAR-ES-SALAAM

hc1Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. (Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii) hc2Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. hc3Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. hc4Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. hc5Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa Tuntufye Mwambusi na Meneja wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Willia Genya wakibadiliashana mawazo katika hafla hiyo. hc8Mchechu akibadilishana mawazo na watendaji wa DSE wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. hc9 Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe akiwakaribisha wageni katika hafla hiyo.
hc10 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakifuatilia jambo katika hafla hiyo ya utiaji saini. hc11 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo. hc12 Watendaji wa DSE wakibadilishana mawazo wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. hc13Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akizungumza katika hafla hiyo. hc14 hc15 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. hc16Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. hc17Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.

Kwa mara nyingine Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Jumatano, 22 Aprili 2015 tumefikia makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.

Mkataba unaosainiwa leo baina ya pande hizi mbili utagharimu kiasi cha dola za kimarekani 1,800,000 (bila VAT) kiasi cha shilingi za kitanzania 3.366 bilioni malipo yatakayofanyika kwa awamu nne katika kipindi cha miaka mitatu.

Mradi wa kipee na wa kwanza Tanzania wa Morocco Square wenye ukubwa wa mita za mraba 105,000 unaotarajia kukamilika ndani ya kipindi cha Miaka Mitatu, ni unaotekelezwa kwa kutumia mfumo mpya kabisa wa ujenzi wa (Design and Building). 

Umebuniwa kwa makini kabisa kulingana na mahitaji ya majengo ya sasa na ya baadae na vile vile unajengwa na mkandarasi wa kitanzania. Sambamba na haya, utekelezaji wa mradi huu umezingatia uwepo wa huduma zote muhimu sambamba na miundo mbadala yakujitosheleza.

Sifa nyingine za ziada za mradi huu ni pamoja na uwepo wa majengo pacha mawili makubwa ya ghorofa, moja likiwa na ghorofa 17 na 19.

Jengo hili limebiniwa likiwa na mahitaji muhimu yakiwa sehemu moja (Mixed Development) ikiwepo maeneo maalum ya Maofisi ya kimataifa, Sehemu ya hotel kwa ajili ya wafanyabiashara, nyumba za makazi (Residential apartment), maeneo ya maegesho ya magari, huduma za kibenki, pamoja na sehemu ya huduma za masoko ( shopping mall).

Mradi huu unatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara katika jiji la Dar Es Salaam vile vile ukizingatia mahitaji ya ukuaji na upanukaji wa jiji la Dar Es Salaam. Jengo la Morocco Square lipo karibu kabisa na kitovu cha jiji likiwa limezungukwa na maofisi na makazi muhimu kabisa. 

Eneo la Morocco Square linatoa fursa kwa mkazi kuweza kufika kwa karibu kabisa sehemu mbalimbali muhimu za jiji la Dar Es Salaam kama vile Mikocheni, Oystebay, Masaki,Mikocheni, katikati ya jiji la Dar Es Salaam,Kinondoni, Kawe na Mlimani City.

Makubaliano haya kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Soko la Hisa la Dar Es Salaam ( Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE) yanatoa fursa za kipekee kwa (DSE) pamoja na mawakala wake wa soko la mitaji na tunapenda kulipongeza soko la hisa kwa kuwahi kabla ya mashirika yote ili kuweza kupata fursa ya kipekee katika jengo hili la kisasa kabisa na la kwanza Tanzania.

Tunapenda kutoa wito kwa Mashirika ya kimataifa, yakati ( Medium Enterprises) kuchanmkia fursa hii ya kipekee ususani ukizingatia kwamba miji yote Duniani soko la hisa huwa chachu ya maendeleo ya wadau wote wanaofanya biashara kuzunguka eneo husika.

Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalumu linalowezesha kutua helikopta, eneo kubwa la maegesho ya magari ya ziada, Ofisi ya Meneja wa Usimamizi wa Milki, eneo maalumu la kukusanyia taka, nyumba ya mlinzi, umeme wa uhakika, miundombinu ya zimamoto, mfumo wa vipoza joto, kebo za mtandao wa mawasiliano, lifti, ulinzi wa saa 24 wa Kamera za CCTV na kisima kirefu cha maji chenye mfumo wa kusukuma maji ya kutosha.

Tunawahamasisha wenye kuhitaji maeneo ya ofisi, biashara na nyumba za kuishi wafanye mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.

Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua ofisi au kuwekeza katika mradi huu, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Mauzo, Makao Makuu ya NHC au piga simu namba 0754 444 333; baruapepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya Shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.

Wednesday, April 22, 2015

WATU SITA MBARONI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

Vipande kumi na nane vya meno ya Tembo ambavyo Jeshi la   polisi mkoa wa Tabora ilivikamata mapema wiki hii huko wilayani    Sikonge.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha baadhi ya waandishi wa habari vipande vya  meno ya Tembo ambavyo vilikamatwa na Jeshi hilo.
Hapa akionesha milipuko aina ya Superpower 90 ambayo   ilikamatwa wiki hii huko wilayani Nzega yenye uzito wa kilo 133

 
Na Allan Ntana, Tabora

JESHI la Polisi mkoani Tabora limefanikiwa kukamata watu 6 wakiwa na vipande 17 vya meno 8 ya tembo kutokana na operesheni maalumu inayoendeshwa na jeshi hilo mkoani hapa dhidi ya watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uharifu na waharifu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda amesema watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 18 Aprili 2015 majira ya saa 1.00 za jioni katika barabara ya Sikonge –Tabora jirani na benki ya CRDB tawi la Sikonge.

Alitaja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Baraka Yohana (29) mkazi wa Mnanira, Kigoma, Rashid Chande (28) mkazi wa Kizanga-Sikonge, Keneth France kutoka Ofisi ya Mshauri wa Mgambo Manispaa ya Tabora, Ibrahimu John (25) mfanyabiashara Tabora, Peter Mollel (31) mfanyabiashara Tabora na Anthon Hamisi (42) mfanyabiashara Tabora.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 282 CXJ wakiwa na vipande hivyo 17 ambavyo ni sawa na meno 8 ya tembo.

Kamanda alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na mara baada ya kukamilisha taratibu za upelelezi watafikishwa mahakamani mara moja.

Kamanda aliongeza kuwa katika msako huo unaoendelea mnamo tarehe 13
Aprili 2015 majira ya saa 11.00 za jioni katika maeneo ya stendi ya mabasi wilayani Nzega mkoani Tabora pia walifanikiwa kukamata watu 3 waliokuwa na milipuko aina ya Power 90 ikiwa na uzito wa kilo 133 iliyokuwa ikisafirishwa kwa gari aina ya Toyota Saloon yenye namba T 347 BFH inayofanya shughuli za taxi mjini Nzega.

Aliongeza kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na mara tu baada ya kukamilika upelelezi watafikishwa mahakamani.

UJUMBE WA IMETOSHA UKIWA METRO FM 99.4 MWANZA!


Kutoka kushoto ni Juma Herman(meneja wa Green Palm Hotel, Issaya Mwakilasa aka Wakuvwanga, Jhikolabwino Manyika, Kelvina John, Mwenyekiti Masoud Kipanya na Tonny Alphonce(Mtangazaji Metro fm 99.4

Siku ya Ijumaa ya tarehe 17/04/2015 ujumbe wa Imetosha Foundation ukiongozwa na Mwenyekiti Masoud Kipanya ulifanya mahojiano katika kituo cha redio cha Metro Fm 99.4 kwenye kipindi cha Pambazuko la Metro fm 99.4 ikiwa ni katika mfululizo wa kujitambulisha kanda ya ziwa kwa taasisi hiyo inayopinga mauaji kwa watu wenye ualbino kwa njia ya elimu. Msanii wa vichekesho (comedian) Wakuvwanga ambaye ni mjumbe wa taasisi hiyo alitoa kali alipoulizwa angependekeza adhabu gani kwa watakaopatikana na hatia ya kuua watu wenye ualbino? akajibu "Kwa kuwa hawa si watu bali ni wanyama kutokana na vitendo vyao viovu basi napendekeza serikali iwapeleke Mikumi national park iwafungie ndani ya senyenge ili watalii wawe wanaenda kuwaona kama wanavyoenda kuwaona Simba na wanyama wengine! Kipindi hicho maridhawa kiliendeshwa na watangazaji Tonny Alphonce na Katumba Madua
Mtangazaji wa kipindi cha Pambazuko la Metro Fm, Tonny Alphonce akimuuliza swali Masoud Kipanya.
Masoud Kipanya akijibu swali toka kwa mtangazaji wa Metro Fm 99.4zaji Tonny Alphonce.
Tonny akimpiga swali Wakuvwanga, anayesikiliza kwa umakini wa hali ya juu, soma uone jibu lake!
Kutoka kushoto ni Katumba Madua, Wakuvwanga na  msanii wa muziki wa Reggae Jhikoman

Moja ya studio za Metro Fm 99.4 ambazo wanazo tatu katika jengo hilo lililopo kati kati ya jiji la Mwanza
Picha ya Pamoja ndani ya Metro fm 99.4 toka kushoto ni Juma Herman, Mkala Fundikira, Kelvina John, George Binagi, Tonny Alphonce, Rosier, Sophia George, Wakuvwanga Masoud na Katumba Madua
Jhikoman kushoto, Rosier(receiptionist) na Masoud
Masoud akibadilishana mawazo na Sphia George wa Metro fm 99.4 ya Mwanza wiki iliyopita ujumbe wa Imetosha Foundation ulipotembelea studio za kituo hicho cha redio

Mtandao huu unaomba radhi kwa kuchelewa kurusha habari hii kwa wakati muafaka kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Ahsante!

BALOZI WA RWANDA NCHINI MAREKANI MHE. MATHILDA MUKANTABANA ATEMBELEA OFISI ZA UMOJA WA AFRIKA WASHINGTON DC


Mhe Balozi wa Rwanda Profesa Mathilda Mukantabana akiwa katika pich ya pamoja na Balozi wa AU Mhe. Amina Salum Ali alipotembelea ofisi za Umoja wa Afrika uliopo Washington, DC nchini Marekani .Balozi Profesa Mathilda anachukua uongozi wa mikutano wa mabalozi wa Afrika katika kipindi cha mwezi April hadi July 2015 akiwakilisha kanda ya Afrika Mashariki.

UZINDUZI WA VIDEO YA WIMBO MPYA WA LADY JAYDEE FT MAZET & UHURU KUFANYIKA M.O.G BAR & RESTAURANT IJUMAA HII

IMG-20150421-WA0000

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YASAINI MIKATABA KUPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI

Tuesday, April 21, 2015

KITABU CHA KIGWANGALLA "TANZANIA TUITAKAYO" KUSAMBAZWA NCHI NZIMA

CCiV3FEWIAEKkRE
Na Zainul Mzige wa modewjiblog
Mbunge wa Nzega ambaye amejitokeza kutangaza nia ya kugombea urais nchini ambaye pia amekuwa mtetezi mkuu wa wananchi wa jimboni kwake kupitia migodi mbalimbali Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (Mb) ameandika kitabu kiitwacho "Tanzania tunayoitaka" yakiwa ni mawazo yake binafsi ambacho anatarajia kukisambaza Tanzania nzima.
Kigwangalla katika kitabu chake amezungumzia fikra mpya za kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kutokana na urithi wa rasilimali, utamaduni na utajiri wa nguvu kazi.
“Kuna mambo misingi minane niliyoipendekeza, ambayo yakifanyiwa kazi tutapata Tanzania Tuitakayo”, amesema Kigwangalla.
10649905_10152917376443243_2689156129216005815_n
"Misingi hiyo inaunda mfumo mpya wa politikoikonomi unaoitwa Ujamaa wa Kiafrika wenye Vionjo vya kibepari. Misingi imepewa jina la 'Kigwanomics.', ameongeza Kigwangalla.
Kitabu hicho cha "Tanzania tunayoitaka" kwa mujibu wa Kigwangalla mwenyewe ameeleza kuwa kinapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Iringa huku juhudi zikiendelea kusambaza Tanzania nzima.
Pata nakala ya kitabu cha Kigwangalla ambacho kipo mtaani kwako.

CHADEMA YAPATA MRITHI WA JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI 2015

 
Na Magreth Magosso, Kigoma
 
Mgombea Ubunge  Jimbo  la Kigoma Kaskazini  2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Mkoa wa Kigoma,Dr.Yared Fubusa amesema kuwa,wananchi waishio vijijini watashindwa kujikwamua na kipato duni,ikiwa watadumisha siasa za upepo kwa kuchagua mgombea asiyejali kero zinazowakabili, ilihali mkoa una rasilimali za kutosha zitakazowanufaisha wakazi wake.
 
Akifafanua kauli hiyo Dr.Fubusa alisema kwamba,wananchi wanapaswa kutathimini uwajibikaji wa mgombea katika jimbo husika kwa kigezo cha mahusiano bora yenye maslai kwa jamii hiyo ,ili kuepuka viongozi wanaokimbia kuishi katika majimbo yao baada ya kuukwaa  ubunge kwa hadaa za mjini na kuonya  wasikubali kufanywa madaraja ya wagombea wenye maslai binafsi.
 
Alitaja sifa za mgombea bora ni pamoja na kuwekeza rasilimali mkoani mwake na kuishi jimboni humo  baada ya kumaliza vikao vya Bunge sanjari kutafuta wahisani wa kufadhili miradi mbalimbali ambayo ni chachu ya  kuboresha kero kadhaa ikiwemo ajira , afya,elimu,  miundombinu ya barabara  na nishati kwa lengo la kuondoa  kamba ya umaskini na ufakiri.
 
Alibainisha kuwa,ushirikishwaji wa wananchi katika usimamizi wa maliasili,uchumi na mazingira ni chanzo cha kupunguza adha ya ukosefu wa ajira kwa jamii, kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kutumia fursa hizo ili kujikwamua katika tope la  umaskini  na dhana ya utegemezi wa kipato unatoka serikalini.
 
Dr.Fubusa alisema kipaumbele cha awali ni kuboresha zahanati ya bitale kuwa na hadhi ya hospitali ya wilaya ambapo kwa sasa wilaya haina ,  ujenzi wa sekondari katika  kata 14 , ujenzi wa soko   katika mji mdogo wa mwandiga,sanjari na ujenzi wa viwanda  vya uchakataji wa matunda(nanasi),kahawa na mchikichi ili kuongeza thamani ya bidhaa na kupunguza kero ya ajira .
 
Alisema ahadi hizo si za kubahatisha kwa kuwa anawafadhili kutoka watu wa marekani na kuwasihi wakazi wa vijiji vilivoporwa ardhi na hifadhi ya Gombe mwaka 1968 kufidiwa haki zao ambazo waliondolewa bila kufidiwa na kuongeza chanzo cha mapato katika mwalo wa kijiji cha Kalalangabo kwa kujengwa  forodha ili kuongeza mapato kwa halmashauri.
 
Mbali na hayo alisema kitendo cha halmashauri ya kijijini kutoa huduma katika jimbo la kigoma mjini ni fedheha na chanzo cha kushindwa kutoa huduma bora kwa wananchi wa jimbo la kigoma kaskazini na kushauri  majengo  yanastahili yawepo mji mdogo wa mwandiga.
 
“Raisi Jakaya kikwete ni kiongozi anayeunga mkono uthubutu wa Dr.Fubusa kuwa ni kijana pekee mzalendo ,jasiri na mwenye uchungu wa kuwaondoa watu wa eneo lake katika janga la umaskini kwa kuwa ametoa ajira zaidi ya watu 50 katika shule ya  sekondari Gombe na timu ya Mvuvumwa”alisema Mgombea huyo mwenye Phd ya uchumi,maliasili na mazingira.
 
Mwandishi wetu amezungumza na mkazi wa jimbo hilo Fadhili Hamisi juu ya mgombea huyo,alisema ni kijana pekee mwenye uthubutu wa kuishi kijijini na kuwekeza rasilimali kwa jamii ya kijiji cha kiganza anjari na kusogeza huduma ya elimu ya chuo kikuu mkoani humo na kutaka aongeze jitihada za makusudi kumaliza mgogoro wa ardhi baina yake na walengwa.
 
 Aidha hivi sasa anakabiliwa na  miradi mbalimbali ya elimu hususani ujenzi wa   vyumba  viwili vya madarasa ya kuanzia  na ofisi ya walimu  shule ya msingi mpya kijiji cha Mkabogo ,shule ya Luhobe na buhagala kata ya mkongoro   .Huku shule ya sekondari Gombe ikishika nafasi ya kwanza  kimkoa katika ufaulu kwa  wananfunzi waliomaliza kidato cha sita na Nnne mwaka jana.

MKUU WA KKKT WA ASKOF DR.ALEX MALASUSA AKIMUINGIZA KAZINI MSAIDIZI WAKE MCHUNGAJI CHEDIEL LWIZA

1aMkuu wa KKKT Askofu Dk Alex Malasusa akimuingiza kazini Msaidizi wake Mch. Chediel Lwiza wakati wa Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu la Azania Front jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wachungaji pamoja na waumini mbalimbali wa KKKT.
2aMkuu wa KKKT Askofu Dk Alex Malasusa akimuingiza kazini Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Godfrey Nkini wakati wa Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu la Azania Front jijini Dar es Salaam
4aMkuu wa KKKT Askofu Dk Alex Malasusa akimpongeza Msaidizi wake aliyemaliza muda Mch. George Fupe wakati wa Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu la Azania Front jijini Dar es Salaam
5aMkuu wa KKKT Askofu Dk Alex Malasusa akmkabidhi gari Msaidizi aliyemaliza muda wake Mch. George Fupe
6a Baadhi ya Wachungaji waliohudhuria Ibada ya kumuingza kazini Msaidizi wa Askofu Mch. Chedile Lwiza
7aBadhi ya waumni waliohudhuria sherehe za kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mch. Chedile Lwiza
8aAskofu Mstaafu wa KKKT Dk. Elinaza Sendoro akifuatilia Ibada
9aNaibu Waziri TAMISEMI Aggery Mwanri akiwasalimia waumni
10aWachungaji wakipungia waumini wakati walipokuwa wakitambulishwa.
11 aMkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) Nehemia Mchechu ambaye pia ni muumini wa KKKT akitoa salamu
11aaMkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) Nehemia Mchechu ambaye pia ni muumini wa KKKT akitoa salamu
12a Maaskofu Alex Malasusa mwenye fimbo na Dk Fredrick Shoo wakiwa katika picha ya pamoja na Msaidizi mpya wa Askofu wa DMP Mch Chedile Lwiza (Katikati)