Na Magreth Magosso, Kigoma
Mgombea Ubunge Jimbo
la Kigoma Kaskazini 2015 kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Mkoa wa Kigoma,Dr.Yared Fubusa amesema
kuwa,wananchi waishio vijijini watashindwa kujikwamua na kipato duni,ikiwa
watadumisha siasa za upepo kwa kuchagua mgombea asiyejali kero zinazowakabili,
ilihali mkoa una rasilimali za kutosha zitakazowanufaisha wakazi wake.
Akifafanua kauli hiyo Dr.Fubusa
alisema kwamba,wananchi wanapaswa kutathimini uwajibikaji wa mgombea katika
jimbo husika kwa kigezo cha mahusiano bora yenye maslai kwa jamii hiyo ,ili kuepuka
viongozi wanaokimbia kuishi katika majimbo yao baada ya kuukwaa ubunge kwa hadaa za mjini na kuonya wasikubali kufanywa madaraja ya wagombea wenye
maslai binafsi.
Alitaja sifa za mgombea bora ni
pamoja na kuwekeza rasilimali mkoani mwake na kuishi jimboni humo baada ya kumaliza vikao vya Bunge sanjari kutafuta
wahisani wa kufadhili miradi mbalimbali ambayo ni chachu ya kuboresha kero kadhaa ikiwemo ajira ,
afya,elimu, miundombinu ya barabara na nishati kwa lengo la kuondoa kamba ya umaskini na ufakiri.
Alibainisha kuwa,ushirikishwaji
wa wananchi katika usimamizi wa maliasili,uchumi na mazingira ni chanzo cha
kupunguza adha ya ukosefu wa ajira kwa jamii, kwa kuwa watakuwa na uwezo wa
kutumia fursa hizo ili kujikwamua katika tope la umaskini
na dhana ya utegemezi wa kipato unatoka serikalini.
Dr.Fubusa alisema kipaumbele cha
awali ni kuboresha zahanati ya bitale kuwa na hadhi ya hospitali ya wilaya
ambapo kwa sasa wilaya haina , ujenzi wa
sekondari katika kata 14 , ujenzi wa soko katika
mji mdogo wa mwandiga,sanjari na ujenzi wa viwanda vya uchakataji wa matunda(nanasi),kahawa na
mchikichi ili kuongeza thamani ya bidhaa na kupunguza kero ya ajira .
Alisema ahadi hizo si za
kubahatisha kwa kuwa anawafadhili kutoka watu wa marekani na kuwasihi wakazi wa
vijiji vilivoporwa ardhi na hifadhi ya Gombe mwaka 1968 kufidiwa haki zao
ambazo waliondolewa bila kufidiwa na kuongeza chanzo cha mapato katika mwalo wa
kijiji cha Kalalangabo kwa kujengwa
forodha ili kuongeza mapato kwa halmashauri.
Mbali na hayo alisema kitendo cha
halmashauri ya kijijini kutoa huduma katika jimbo la kigoma mjini ni fedheha na
chanzo cha kushindwa kutoa huduma bora kwa wananchi wa jimbo la kigoma
kaskazini na kushauri majengo yanastahili yawepo mji mdogo wa mwandiga.
“Raisi Jakaya kikwete ni kiongozi
anayeunga mkono uthubutu wa Dr.Fubusa kuwa ni kijana pekee mzalendo ,jasiri na
mwenye uchungu wa kuwaondoa watu wa eneo lake katika janga la umaskini kwa kuwa
ametoa ajira zaidi ya watu 50 katika shule ya sekondari Gombe na timu ya Mvuvumwa”alisema
Mgombea huyo mwenye Phd ya uchumi,maliasili na mazingira.
Mwandishi wetu amezungumza na mkazi
wa jimbo hilo Fadhili Hamisi juu ya mgombea huyo,alisema ni kijana pekee mwenye
uthubutu wa kuishi kijijini na kuwekeza rasilimali kwa jamii ya kijiji cha
kiganza anjari na kusogeza huduma ya elimu ya chuo kikuu mkoani humo na kutaka
aongeze jitihada za makusudi kumaliza mgogoro wa ardhi baina yake na walengwa.
Aidha hivi sasa anakabiliwa na miradi mbalimbali ya elimu hususani ujenzi
wa vyumba viwili vya madarasa ya kuanzia na ofisi ya walimu shule ya msingi mpya kijiji cha Mkabogo
,shule ya Luhobe na buhagala kata ya mkongoro .Huku
shule ya sekondari Gombe ikishika nafasi ya kwanza kimkoa katika ufaulu kwa wananfunzi waliomaliza kidato cha sita na Nnne
mwaka jana.
No comments:
Post a Comment