Pages

KAPIPI TV

Saturday, January 31, 2015

MKURUGENZI MKUU WA NHC NEHEMIA MCHECHU ATEMBELEA MIRADI GEITA NA MWANZA

MADIWANI KUMVAA WAZIRI WA UJENZI BUNGENI -KIGOMA

Na Magreth   Magosso,Kigoma

BARAZA la madiwani halmashauri ya wilaya ya kigoma Mkoa wa Kigoma,wameadhimia kwenda Bungeni mkoani Dodoma kuonana na Waziri wa Ujenzi ,ili kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Chankele,Mwamgongo Kagunga kwa nia ya kuondokana na changamoto ya usafiri wa  ziwani( Ziwa Tanganyika ).

Azimio hilo limetokana na sintofahamu ya ukamilishwaji wa barabara hiyo yenye urefu wa km 65  ambapo kupitia bajeti ya mwaka 2013/14 walitumia kiasi cha sh.milioni 194 kukarabati km 20 kutoka mwandiga ,chankele  na kushindwa kufika mwamgongo,ambapo wakazi wa ukanda wa ziwa Tanganyika wanatabika na usafiri wa majini usiokidhi viwango vya usafiri huo.

Awali diwani wa kata ya mwamgongo Kasim Nyamkunga alihoji baraza uhalali wa barabara hiyo kucheleshwa ujenzi wake,ilihali  Rais Jakaya Kikwete na Waziri mkuu Mizengo Pinda waliahidi kujengwa kwake kabla ya mwaka huu,ambapo wameona adha ya wakazi wa vijiji vya kagunga,mgambazi,kaziba kuwa,wana tija ya mradi na  waziri Pinda kudai atachangia sh.milioni 300.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi na mazingira Habibu Hebeye alisema sheria mpya ya mikataba ya miradi ya ujenzi wa miundombinu inachangia uzoreteshaji wa miradi mbalimbali wa huduma za kijamii kwa kuwa mradi unaoanzia kiasi  cha  milioni 50 katika halmashauri zote nchini lazima mkataba upitiwe na mwanasheria mkuu kitendo kinachokwamisha tija kwa wakati.

Akijibia hilo Mwenyekiti wa halmashauri Hamis Betese alisema Februari,10,2015 akishirikiana na mkuu wa wilaya,na mwakilishi kutoka Tanroada watapanda bungeni kuonana na waziri wa ujenzi ili kukamilisha mchakato wa ujenzi huo kwa kushirikiana na Tanroad kutokana na halmashauri kushindwa kukidhi hitaji la mradi husika.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya Ramadhan Maneno aliwaonya wataalam wa humo,waache uongo katika usimamiaji wa miradi mbalimbali ya wananchi,kutokana na baadhi ya watalam kutoa tarifa za uongo hasa katika ujenzi wa mradi wa maabara ,ambao unasuasua baada ya serikali kuu kuongeza muda wa miezi sita ili kila halmashauri ifanikishe hilo.

Ally Kisala ni mfanyabiashara mkongwe wa vitenge alisema kufunguka kwa barabara hiyo ni fursa kwa wananchi kujimiarisha kiuchumi na shughuli za kitalii kwa kuwa hifadhi ya gombe ipo mwambao mwa ziwa husika na jamii kupata huduma ya afya kwa wakati kuliko usafiri wa majini ni hatari  kwa wajawazito na watoto.

Aidha Katibu wa ccm wilaya hiyo Mobutu Malima alisema changamoto za wananchi wa ukanda wa mwambao utakwisha kwa ushirikiano baina ya jamii na viongozi wa serikali ya mkoa haina budi kushinikiza mradi huo uwe chini ya Tanroad ili kuwakwamua umma kiuchumi,afya na elimu.

Friday, January 30, 2015

BARABARA KWENDA OLOLOSOKWAN TISHIO KWA MAGARI MAKUBWA

DSC_0035
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyemtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kikazi ya siku nne kwenye kijiji cha Ololosokwani na halmashauri ya Ngorongoro kwa ajili ya maandalizi ya mradi wa kijiji cha digitali unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Ki-elektronic ya Samsung unaotarajiwa kuwasili kijijini hapo mwezi februari ukitokea jijini Dar.

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues ameonesha mashaka yake juu ya ubora wa barabara ambazo magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali Ololosokwan yanaweza kupita.

Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali wakati alipomtembelea ofisini kwake.

Akiwa katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya kumwelezea shughuli za Unesco katika wilaya yake, Mkurugenzi Mkazi huyo alipata nafasi ya kuzungumzia haja ya kuboreshwa kwa maaneo kadha ya barabara kuelekea kijiji cha Olosokwan ili kuyawezesha magari hayo makubwa kufika kwa urahisi.

Huku akimuonesha mkuu wa wilaya baadhi ya picha alizopiga akiwa njiani kukagua njia ya kupita magari hayo na kuangalia maandalizi ya mwisho ya mradi huo mkubwa na wa kipekee nchini alisema hali ya barabara si nzuri hata kidogo.

Vifaa kwa ajili ya kijiji hicho vipo bandarini tayari na magari yanayoweza kubeba makontena hayo ni makubwa na barabara za kuelekea kijiji hicho ni mbaya.
DSC_0041
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) aliyeambatana na wataalamu wa elimu, afya na mawasiliano pamoja na Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia (hayupo pichani) . Kutoka kushoto wa kwanza ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias, Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.

Kuwapo kwa kijiji hicho ni matokeo ya mkataba uliotiwa saini kati ya UNESCO na kampuni ya elektroniki ya Samsung mwaka jana.

Katika makubaliano hayo yalitiwa saini na Mwakilishi mkazi Unesco nchini, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Mike Seo katika Kijiji hicho kitakuwa na shule yenye Tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (Telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua kwa ajili ya kijiji hicho.

Mradi huo utawezesha UNESCO kuwapatia vijana wa Kimasai elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
DSC_0096
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wataalam wa Elimu, Afya, Utamaduni na Kilimo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro jijini Arusha. Kushoto pichani ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Peter Kitenyi.

Kupitia kijiji hicho vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao.
Wakati wa utiaji saini Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania alitaja miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika mradi huo wa kijiji cha digitali huko Loliondo ambayo ni pamoja na kuweza kupata nishati rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira.

Alisema kwamba Afrika imekuwa mstari wa mbele katika uanzishaji wa vijiji vya digitali. Aidha kwa kitendo hicho Afrika inaonesha dunia ni kwa namna teknolojia inaweza kutumika kuleta mabadikliko chanya yanayotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi waliopo vijijini.

Kijiji hicho cha Loliondo kitakuwa cha nne katika vijiji vya kidigitali barani Afrika.Inatarajiwa kwamba kijiji kingine kitajengwa mjini Zanzibar kwa ushirikiano wa UNESCO na Samsung Electronics mwaka huu.
DSC_0080
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo na mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kuelekea kijiji cha Ololosokwani kwa ajili ya mkutano na wanakijiji wa kijiji hicho kabla ya kuwasili kwa mradi wa kijiji cha kidigitali mapema mwezi februari.
DSC_0092
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea changamoto za miundo mbinu ya barabara kwa kutumia picha alizopiga akiwa njiani kuelekea kijiji cha Ololosokwan kupitia barabara ya Lake Natron kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali.
DSC_0105
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akielezea jitihada zitakazofanywa na wilaya yake katika kuhakikisha miundo mbinu ya barabara inarekebishwa kuondoa usumbufu kwa magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali cha Ololosokwan yanapita bila kikwazo mapema mwezi februari.
DSC_0136
Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Unesco pamoja na Wizara ya afya wakitazama picha hizo kwenye kompyuta mpakato ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.
DSC_0136

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AZURU KABURI LA ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS HAYATI DR.OMAR ALY JUMA

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA NHC GEITA NA KAGERA YAHAMASISHA MAENDELEO